Rekebisha heading yako.
Hiyo ni Idea ya kawaida sana tu,na biashara kama hiyo inafanyika sehem hizo.
Sasa sijaona jipya saana hapo
Pia naomba Uitendee haki Advance Diploma yako in Finance.
Najua utakuwa umesomea Chuo cha Fedha Chwaka,Zanzibar ambacho ni chuo Bora sana.
Nahisi unasumbuliwa na vitu viwili:-
a)Msongo wa Maisha
b)Kuhamisha maandishi ya kwenye kitabu kupeleka kwenye uhalisia
Ushauri ni kwamba,wewe ni msomi,mie sio msomi wa Biashara ila ni mfanya biashara.
Unajua hakuna Buisness Idea yoyote ambayo ni mpya katika dunia hii.Kila unalifikiria basi lilianza kabla hujazaliwa.
Watu wanashindana kwa namna ya kutumia fursa kwenye biashara husika na ubunifu.
Zanzibar kama unakumbuka kabla ya pale Bomba Ice cream kwa mchina na yule Jirani yake hawajaanza kufanya hii biashara,watu walikuwa wamelala sana na hakuna aliestukia.Ila sio kwamba kulikuwa hakuna Ice cream Zanzibar.Ila pale Kuna mmoja ni mjanja zaidi,maana yeye anatengenezea pale pale dukani kwake ni ni msafi sana,na watu wanaona na Mashine kazifunga pale.Anakula Tenda za harusi kama wazim vile.
Watoto wa shule za Mwanakwerekwe,Shah School,Nyuki Military School,wote anabeba.
So,issue ni ubunifu,na sio pesa nyingi sana kama unafikiria wewe.Unaweza kuanza hata na laki nne tu.
Ukawa unanunua rejareja kisha unauza,ukipata pesa unanunua Mashine ya Kutengenezea Mwenyewe.Nahisi inakaribia 6m ila ndongo ya port mbili