the locksman
JF-Expert Member
- May 5, 2012
- 1,101
- 350
Habari wakuu, nataka kujua bei ya dekoda ya TING kwa full set ikiwa na satellite dish yake.
Nimepita baadhi ya maduka Kariakoo nimefanikiwa kuona ile inayotumia antenna peke yake nikaambiwa hiyo ya antenna ni 120,000/- 'na malipo kwa mwezi ni 10,000/-. kwa anayefahamu ile ya dish kama pia malipo kwa mwezi ni 10,000/- au ni tofauti.
bei yake laki 2 malipo kwa mwez elf 20
ahsante nashukuru,
unaweza kujua malipo ya mwezi yakiisha channel zipi zinabakia,nikiwa na maana zinazobaki zinaonyesha sana sana za tanzania.
Ni chanel ten,itv,startv,chanel 5 na tbc 1
Ukilipia hiyo elfu 20000,,unaweza kupata channel za kuonyeshea mipira?
TING wenyewe wanasema wanaonyesha baadhi ya mechi EPL.
Ngoja waje wanaotumia hiki king'amuzi watujuze.
Mleta mada plz check king'amuzi kingine, hawa ting ni stress kukaa mwez mzima bila kutoonekana channels ni kitu cha kawaida, mimi ni muhanga natafta king'amuzi kingine, kama usipolipia channels zinazoonekana ni tbc1 na atn bac, hamna cha clouds, Chanel 10, eatv wala itv, sikushauri hata ununie hiki king'amuzi
Mleta mada plz check king'amuzi kingine, hawa ting ni stress kukaa mwez mzima bila kutoonekana channels ni kitu cha kawaida, mimi ni muhanga natafta king'amuzi kingine, kama usipolipia channels zinazoonekana ni tbc1 na atn bac, hamna cha clouds, Chanel 10, eatv wala itv, sikushauri hata ununie hiki king'amuzi
asante mkuu,,pia unaweza nisaidia vinapatikana k/koo sehemu gani
Hata mm Sikutaka kuchangia maana ningeoneka mnafiki ninaua biashara ya watu. Hawa TING hawafai kifurushi kikiisha unabaki na Channel mbili tu TBC1 na ATN hlf mm nimelipia wiki mbili zimepita mpaka sasa kuna channel zaidi ya sita hazipo hewani ukiwauliza wanakwambia ni matatizo ya kiufundi, hakuna cha mpira wala nini ni waongo sana. Hlf king'amuzi chao kinaonyesha wakiamua wanaweza kufunga hata siku nzima hawako hewani. Namshauri mleta mada atafute kingamuzi kingine.
yaani mimi mpaka sasa sina Kingamuzi, nlinunua continental kikaniletea mapicha picture nkakipiga bei...nkataka kununua ting nkaambiwa ni majanga zaidi...
...dstv nyumba za kupanga naona ntahama soon so sijui hata nfanyaje
...mimi ni movie tu.
...daah digital itatuua...!!