Yote ameleta lema, wakati ule hawa watu walipogoma yeye aliwatetea eti wapaki wapi.!? na barabara mbadala zipo ila watu wamegeuza ni mahali pa kupaki magari yao, wamachinga kufanyia biashara zao yote ni lema ameleta.! yaani jiji limekuwa kama zizi, haohao madereva wanakojoa barabarani hovyo na kupaki ndio kabisaa, magari mengine mabovu hayafai kubebea abiria lakini yapo barabarani, dawa iliyopo ni kuondoa daladala zote na kuweka coaster zifanye kazi kama Dar, kero nyingine ni ungaltd daladala ni shida tupu ukiwa ndani utafikiri uko nje, maana gari limetoboka mtindo mmoja mpaka unaona chini, janga la mwisho ni madereva na makonda ni wachafu kupindukia yaani ni kero na lugha mbaya ajabu, mirungi, viroba kwa kwenda mbele, mkuu wa mkoa na kamanda wa polisi mkoa tunaomba mtutatulie hili tatizo, naomba kuwakilisha hoja.