Bahati Nasibu Ya Taifa Mpo Wapi?

ibanezafrica

JF-Expert Member
Joined
Oct 23, 2014
Posts
7,261
Reaction score
6,557
Ni shirika la Bahati Nasibu la taifa, miaka ya nyuma lilifanya michezo na kila wiki kulikua na draw kubwa moja na draw ndogo kati ya wiki, mabanda yalitapakaa mji wote hususan hapa Dar
Tickets za Mchezo ziliuzwa kwa mpangilio mzuri, ulikuwa unapewa kitabu unachagua ticket unayoitaka au hata kitabu chote,ulikuwa mchezo mzuri
Sasa cjui ni kipi kilichotokea mpaka shirika hili limeshindwa kuendesha michezo Ile na badala yake zimezuka Bahati Nasibu nyingi za kiujanja ujanja lakini cha ajabu zenyewe zinaendelea na kuzidi kuongezeka
Je, walikuwa hawapati Faida? Mbona ni mchezo ambao naona unalipa vizuri kama ukisimamiwa vyema?
Tunaomba shirika lisimame tena kurudisha mchezo ule mitaani tena kwa awamu hii ungepata wafuasi wengi kuliko kuacha hii michezo izidikuongezeka na ukiipima ni kuwa ipo very tricky
Turudishieni mchezo ule cha muhimu siku ya draw tuone au wawepo mashuhuda katika TV live wakati linazungushwa lile gurudumu kutoa washindi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…