Mwizukulu wa Buganda
JF-Expert Member
- Nov 19, 2024
- 638
- 1,771
Dkt. Samia Suluhu Hassan analiangazia Jiji la Dar Es Salaam kwa miaka 25 ijayo. Anajua Dar Es Salaam ni Jiji la Biashara, anatambua Jiji hili ndiyo kitovu cha uchumi wa nchi hii, amefanya maamuzi, tunaenda kujenga Bwawa la Kidunda, Bwawa ambalo lilikuwa ni ndoto ya Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere. Maamuzi yamebadilika mara kwa mara kwenye Bunge la Tanzania na Watanzania niwaambie Dkt. Samia amesema imetosha, tunajenga kwa fedha zetu wenyewe, zaidi ya shilingi Bilioni 336 anazitoa Dkt. Samia Suluhu Hassan. Mkandarasi yupo site na leo tunazungumza asilimia 32 ya utekelezaji wa mradi wa maji Kidunda.
"Mhe. Mgombea wa Kiti cha Urais Dkt. Samia, sisi tunakuombea mema tarehe 29 Oktoba sio kushinda ni unaenda kupata ushindi wa Kimbunga. Haya maamuzi ambayo umeyafanya utakumbukwa milele na milele katika kuhakikisha unatatua matatizo, sisi sasa hivi tunachopambana nacho ni kuendelea kuboresha huduma kwa wateja, mwananchi anataka kuunganishiwa maji yake, tumeelekeza na ndiyo maelekezo yako isizidi siku 7 mwananchi apate huduma ya maji safi na salama.Maelekezo yako uliyotupatia ni haki ya mwananchi kupata maji lakini pia unachukizwa na haupendi mwananchi anabambikiziwa bili ya maji. Suala la ubambikiziaji wa bili za maji nataka muwaambie wasoma mita kuwa hizo ni zilipendwa, Dkt. Samia maelekezo yake sasa hivi tunakwenda kutumia luku ya maji kama za umeme.
"Ndugu zangu mkimpata kiongozi anawavusha kwenye kiangazi, wewe mvushe kwenye masika. Dkt. Samia ametuvusha kwenye nyakati zote, kuwa na Kiongozi wa aina yake, hawapatikanaji kila mahali na kila wakati, tumempata tumtumie kwa maslahi ya wana Dar Es Salaam na watanzania ili kuijenga Tanzania tuitakayo."- Jumaa Aweso, Mgombea Ubunge Jimbo la Pangani Mkoani Tanga na Waziri wa Maji akimnadi Mgombea Urais wa Tanzania kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi CCM Dkt. Samia Suluhu Hassaneo Jumanne Oktoba 21, 2025 Wilayani Kinondoni Mkoani Dar Es Salaam.