Mkuu, kumbuka kuwa waislamu safi huwa hawana hiyana na wakristo, kadhalika wakristo safi hawana hiyana na waislamu, makundi haya mawili huonekana ni maadui kwasababu ya watu wachache walioshindwa kuelewa misingi ya dini hizo mbili, natambua moja ya misingi mikuu ni upendo, kwa taarifa yako Mkuu Rais Ally Hassan Mwinyi amekuwa mlezi wa chombo fulani cha kikristo, kama sijakosea ni CSSC kwa miaka mingi tu, hata huyu Mama ni mwenye hofu ya Mungu.
Kuna kiongozi mmoja tu hapa katikati alitaka kutuharibia uhusiano uliopo kati ya waislamu na wakristo, kumbuka vizuri utatuambia Mkuu