Apple mbioni kuinunua beats

ManiTek TV

JF-Expert Member
Joined
Jun 3, 2011
Posts
410
Reaction score
159
[h=1]APPLE MBIONI KUINUNUA BEATS[/h]


​
Kampuni ya Apple imo mzungumzoni kuinunua kampuni ya Beats Electronics watengenezaji maarufu wa headphones na watoaji huduma ya ku-stream muziki, ambapo sehemu ya pili ya kampuni hii imesababisha wadau wengi katika Ulimwenguni wa teknolojia kushangazwa na hatua hii ya Apple, hii ni kutokana na ukweli kwamba Apple tayari wanamiliki iTunes na mwaka jana tu Apple wameanzisha huduma sawa na ya Beats inayojulikana kama iTunes Radio.


Beats By Dre ni kampuni changa yenye mafanikio makubwa iliyoanzishwa kwa ushirikiano baina ya Producer wa muziki Jimmy Lovine na msanii maarufu wa Hip Hop Dr. Dre, brand hii ilikuzwa sana kwa kutumia jina la Dr. Dre huku wakitumia waya za kampuni maarufu katika headphones zao inayojulikana kama Monster.


​
Kwa kiasi kikubwa brand hii ya Beats imechangia katika kuleta ughali wa headphones katika Ulimwengu wa leo ambapo moja kati ya headphones za Beats, ambazo ni Wireless Studio huuzwa milioni moja na themanini na mbili elfu. Mazungmzo baina ya Beats na Apple yanasemekana kuwa katika hatua za mwishoni na huenda siku chache zijazo Apple ikamilika asilimia mia moja ya hiza za Beats Electronics.


Dau ambalo limetajwa kuwa mazungumzoni juu ya bei itakayouzwa kampuni ya Beats Electronics ni jumla ya Dola za Kimarekani Bilioni tatu na milioni mia mbili. Iwapo Beats itauzwa kwa thamani hii basi akina Dr. Dre watapata faida kubwa kwani kampuni hiyo inatathminiwa kuwa na thamani ya Dola Bilioni moja tu.


James McQuivey mchambuzi wa Forrester ameeleza haiwezekani kwamba Apple wanainunua Beats wakati kwa upande wa muziki wateja wa Beats na wa Apple iTunes wanaingiliana, hivyo lazima Beats ina siri fulani ya kiteknolojia inayoimiliki. Hata hivyo Headphones za Beats by Dre zimekuwa kivutio kikubwa kwa wapenda muziki kwa vile sio tu hutoa sauti nzuri bali pia inatoa “ujiko” fulani kwa watumiaji kutokana na bei zake.


Mafanikio ya Dr. Dre na Jimmy Lovine kwenye kampuni hii yamesababisha wasanii wengine kadhaa nao kujitosa kwenye uwekezaji wa gajeti akiwemo Curtis Jackson a.k.a Fifty Cent aliyeanzisha kampuni ya Headphones ya SMS Audio na Will.i.am anayetarajiwa kutoa Smartwatch mwaka huu.


Muda mchache uliopita mmoja kati ya wamiliki wa kampuni hiyo Dr. Dre tayari ameshathibitisha kuwa Apple wako njiani kuinunua Beats Electronics. Akaunti ya Apple ina zaidi ya Dola Bilioni mia moja na thelathini na tatu, hivyo kwao huu ni ununuzi pipi tu.


Chanzo: gajetek habari
 
Don't be happy man !
Apple are going to Kill beats value !
We didn't care what Dr Dree will Afford after the acquisition

And Keep in your mind that !
Apple doesn't want to Make android users happy !

R.I.P Jobs ! U see now Android is spreading like Plague !
Rest in peace !

And now your company is going to take over Beats! And minimize it's value according to their policies !
 
Nguvu ya marketing hiyo, mediocre overpriced headphones lakini hakuna anayeweza kuwashika kwenye soko.
 
Tyresse Gibson na Dr. Dre wakisheherekea kuuzwa kwa Beats:

[video=youtube_share;p3jR3nzt_uI]http://youtu.be/p3jR3nzt_uI[/video]
 
Hizi earphones ni over priced huko madukani
 
Mediocre product, great marketing.

I've heard this before, they say exactly the same about Samsung Mobile Division. HTC One is better but Samsung has greater marketing campaign.

Apple is buying a fashion statement, thats what Beats is, and by far better than all headphone manufacturers. As well Beats is not headphones only, there is music streaming service, while iTunes is seriously becoming a thing of the past, Beat streaming service may give Apple a starting point to fight back the domination of Spotify.
 
Sijakuelewa unaposema watumiaji wa headphones za Beats Electronics wanapata ujiko, ni ujiko gani? Wanakodisha hizo headphones kwa kuwa ni ghali?
 
Hivi kuna uhusiano gani kati ya beats audio na beats electronics
 

Siku si nyingi utakuja sikia SMS Audio ya 50 Cent ina nunuliwa na Samsung or other company na Street King (SK) Energy inanunuliwa na Pepsi au Cocacola. Yule jamaa namkubali sanaa anajua kufikiri. Kama mnakumbuka vizuri miaka ya nyuma 50 alikuwa na shares Glaceau Vitamin Water ambayo ilikuja nunuliwa na Cocacola kwa sumthn like $ 4 Billion kama sikosei. Dogo alikula hela ndefu sanaa. I think he is tryna do the same with SMS Audio & SK Energy. Yule jamaa ni mmarekani lakn sumtyms anafikiri kama Mchaga. Lol. Walishakuaga na underground heat / beef na Dr. Dre kuhusu hzo issue za headphones cz wakat akna Dre wanatoa headphones zao muda si mrefu dogo 50 nae akatoa zake zenye ubora kidogo si ajabu ndio sababu ameachana na Shady/Aftermath/Interscope Records and went independent. 50 is a smart kid no lie.
Its really great learning from the moves of successful people like them.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…