Watanzania wengi wanatabia ya upendo na huruma.Hizi ni tunu zetu tumepewa na Mungu mwenyewe.Inapotokea una gari na Iko barabarani ukamuona mtu au rafiki anakuomba lift ni jambo jema kumsaidia.Sasa inatokea huyo jamaa ameketi kiti Cha nyuma kwa Raha kabisa na kuanza mastori ya kukushukuru analifungua dirisha ambalo wewe ulilifunga kwa usalama gari .Anapofika sehemu aliyotaka,anakushukuru pasipo kulifunga dirisha lile pasipo wewe kujua.Matokeo yake unapaki gari ukiamini liko salama lakini ukweli ni kuingia gharama kwa kitendo Cha kumsaidia mtu.Je tufanye Nini tunapotoa msaada unaogeuka kuwa shida?