Andika chochote Kuhusu Technology hizi (Dolby & DTS)

Hazchem plate

JF-Expert Member
Joined
Feb 25, 2011
Posts
11,059
Reaction score
15,529
Watanzania Wengi hawajui Vionjo vinvyopatiakana kutikana na Technology (Dolby Digital, Dolby Atmos, Dolby pro Logic, Dolby purse, Dolby true HD, Dolby Digital +DTS, DTS primere) linapokuja suala la Cinema/ Movies.

Ni wazi kabisa wengi wamezoea kuyaona hayo maneno katika matangazo, muvies Trailers na Muvies covers lakini hawajui nini yanamaanisha.

Nimefungua uzi huu ili kwa kila anayejua basi aandike chochote ili watu wajifunze kupitia andiko. Hata mm nitaandika kama mchangiaji wa kawaida na kama sio OP

Thread imefunguliwa Karibuni nyote
 
Nyingi hapo zinausiana na mfumo wa sauti.


Hata hivo kibongo bongo wengi hazina mantiki kwani mfumo wa sauti wenye kusapoti hivo vitu hawana. Na hata walionavyo hawajapangilia ili kupata ile ladha iliyokusudiwa.

Mfano dolby atmos (7.1/7.2) 5.1.2=5 (front r & left >center chanel>surrounding right and left.) 1 (subwoofer) 2( ceiling speaker or front high right & left)


Sasa wengi hata hiyo system hatuna zaidi y 2 chanel subwoofer ukijitahidi sana unakuta una 5.1 home theater.

Kwanza ni ghali mno.
Kwa nilivofatilia ili uwe na mfumo mzuri wa sound home wa kusapot hizo features hapo uwe na si chini ya million 2.
 
Nimejikuta namkumbuka Lufufu!!!



 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…