Sorry kwa kuwa mwanasiasa kwa leo...ila kama wale waliokuwa pale ferry jana..WALINIBOAAAAAAAAAA
point pekee niliyoisikia jana ni;
Mwaka 2006 kulikuwa na shule 7 tu za sekondari.
Sasa hivi Kikwete anaondoka kuna shule 30 za sekondari mkoa wa Ilala peke yake.
Kwa bahati mbaya naye aliiharibu hoja yake pale alipotaka kutukumbusha kuwa wakati huo huo (2006) ni wakati Mheshimiwa Sumaye alipoacha kuwa waziri mkuu.
Sikuona umuhimu wa hoja hiyo kabisa maana nilijiuliza je, wakati anaingia madarakani Sumaye zilikuwa ngapi? zilikuwa katika hali gani? je hizo 30 zinaweza kuwekwa na kusifiwa kuwa ni katika shule bora za sekondari au ni majengo 30 yanayoongelewa?
Chama tawala lazima kisimame na kujitambua kama chama tawala...MWAGA FACTS (Umefanya NINI na Utafanya NINI) acha wananchi waamue wenyewe.
In my view, wananchi wanatiwa zaidi hasira na chuki dhidi yake wanapohubiri kukosa amani au kuwaambia polisi ni wabaya au kuwatukana wagombea wengine badala ya kutuambia wamefanya nini kwa miaka 50 waliyoko madarakani.
Yani we jamaa uliyekuwa unaongea jana mida ya 5:15 - 5:40pm uliniboa sana. Unahisi wale askari waliokuwa wanasimamia ulinzi kwenye kampeni yenu walijisikiaje? Wale mapolisi wa kile kituo kidogo pale feryy walijisikiaje? Eti, "Msiwaone hao polisi ni wabaya kweli..watawapigeni na mabomu ya moshi tena siku hizi ni ya maji ya kuwasha ukipulizwa ukajikuna unawashwa na kuvimba mwili mzima... "
Je, ni kweli mapolisi ni wabaya hivyo? Kama ndivyo mmewachukulia hatua gani maana sote tunajua kazi yao sio kuwa wabaya kwa wananchi ni kuwatumikia..kuhakikisha ulinzi wa mali zao na wao wenyewe!
Halafu mkamaliza mkutano wenu saa 6:10pm wanawaangalia tu wala hamkupigwa hata kirungu...bado unahubiri mapolisi ni wabaya!