hekimanyingi
JF-Expert Member
- Jul 12, 2013
- 679
- 573
Chuo kikuu cha dodoma (UDOM) kilitangaza kazi september 2012 na |November mwaka huohuo waliotuma maombi wakaitwa kwenye usahili wa kuandika (Written interview). Mwezi march mwaka 2013 watu waliofanya vizuri kwenye usahili wa awali waliitwa kwenye usahili wa mahojiano.
Jambo la kushangaza na la kustaajabisha ni kwamba mpaka leo kimya hakuna cha kuajiriwa waliyofanya interview bali wanapigiwa simu vijana waliosoma pale na kuitwa kuanza kazi kwa kigezo cha kufaulu bila kufanyiwa usahili. Hatujui zilifia wapi hizo nafasi na wamesahau kuwa waliofanya usahili walitumia gharama pia.
Na hatari ninayoiona mbele ni kitendo cha mheshimiwa rais Kikwete kuruhusu vyuo vikuu kuajiri wenyewe bila kuweka sheria kali au utaratibu mzuri wa kuajiri watu kulikoni hivi sasa wanaajiri watu kiholela kisa tu mkuu wa chuo (college) au idara kafurahishwa nao.
Kwa style kama hii tutafika kweli?