Ajali ya manyoni ukweli wafichwa

Samuel A K

Member
Joined
Mar 31, 2009
Posts
45
Reaction score
1
Habari toka chanzo kinachoaminika zaonyesha kuwa ajali ya gari ya mafuta (Tanker) mali ya kampuni inayoaminika kumilikiwa na mtoto wa mkuu (Liz one) LAKE OIL kugongana na treni imefichwa ukweli hasa juu ya watu waliokufa.
Vyombo vya habari vimetangaza idadi ndogo sana wakiwemo askari 2 wakati ukweli halisi ni watu 36 hadi sasa wakiwemo askari 8 na mmoja akiwa katika hali mbaya.

Ajali hii imesababishwa na uroho wa kujipatia utajiri wa haraka kwa wananchi wakiwemo askari kwenda kuchota petroli iliyokuwa ikumwagika kutokana na tenki kuvuja baada ya ajali hiyo, mmoja wa wananchi alienda kuchomoa betri ya gari na kusababisha nyaya kugusana na kutoa moto uliosababisha mlipuko na kuua watu hao.

Kinachonishangaza zaidi ni kwanini kuficha ukweli? Kama serikali inaona aibu basi iwalipe mishahara mizuri wafanyakazi wake ili wasiingie tamaa kama hizi kuacha kazi zao na kuanza kuiba mafuta. Ni aibu kubwa kwa Serikali
 
Facts and Finn - Unazo picha za ajali yenyewe ilivyokuwa?
 
Tuhuma hii ni nzito tunategemea idara ya polisi itatoa taarifa rasmi juu ya tukio hili ili kuondoa kiwingu hiki.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…