NtakuwaSikuchukui, Unahoja ya msingi kwenye kutesana huku. Ila sidhani kama huo "uhindi", "uchina", "uzungu",au "ukenya" wao unasababisha huku kutesana, kama siyo usimamizi hafifu na uwajibikaji duni wa taasisi na vyombo husika ndani ya mipaka ya nchi yetu. Maana sheria zipo na watu wanalipwa mishahara kufatilia mambo kama haya, ila 'ndo hivyo tena...!Wezi kichizi jamaa wa india,tuwe macho.
La msingi maneno kama free internet na unlimited internet yasimamiwe na TCRA waakikishe yanatumika ipasavyo sio wananchi wanadanganywa,lugha za kitapele ndani ya ardhi yetu, free wakati unalipia na ataukilipia upati internet saa hiyo hiyo hadi saa nne usiku,sasa huku si kutesana.
Tena tangazo lao hili hapa juu ya threads zetu, waongo na wezi wakubwa hao. Waziri husika kamata mwizi men, au mpaka msubiri bunge liunde kamati jamani. TCRA, TRA mpo? Hao wanaweza kukwepa kodi wakijidai walikuwa kwenye promotions kumbe wanauza bidhaa kama kawa. Wezi haoooooooooooooo, sijui nipige lwange au niache. Kamateni hao haraka sana watueleze sababu za kutuchezea watanzania.
Prof. Nkomo wa TCRA ni mzuri sana wa kuongea kwenye makongamano. Hopefully team yake inayo-monitor kero za watu mitandaoni italitupia jicho hili tatizo na kupatiwa ufumbuzi.
Promotions wa kadhaa tunazosikia na kuona mitandaoni, magazetini, kwenye luninga, n.k. huduma zake haziendani na kile kinachotangazwa. Bila shaka, huu ni mfano mmojawapo wa huduma zinazohadaa jamii.
Am a customer of Airtel modems. I bought one after seeing the advert that the modems cost 30,000/=tshs and have free internet for six months only to realise that the advert is far from the truth. I have to recharge the modem time and again like the other usual modems. Wana jamii Tanzania inachezewa sana. Hawa airtel ni wezi kama wezi wa madini. Wanaahidi mrahaba kwa vijiji vinavyozunguka halafu hawatoi mrahaba huo. Mwenzenu nimenunua modem yao kati ya hizo wanazotangaza lakini haina hiyo internet ya bure. Nilipowauliza wakaniambia inabidi uweke vocha ya shilingi elfu 6, nikaweka hakuna kitu. Nikawapigia customer care yao wakaniambia modem yako haijaunganishwa na internet, wakanishauri niweke vocha japo ya shilingi mia tano ili waniunganishe, nikaweka hamna kitu. Kwa sasa naitumia modem hiyo kama zile za zamani kabla ya hili tangazo yaani kila inapoisha vocha naichaji. Huu sio wizi kwa Watanzania? Tunanyanyasika hivi mpka lini ndugu zangu nchi yetu wenyewe? Saidia wana jamii forum mawazo yenu.
Hili jamaa nalo ni JIIZI na DHAIFU mnooo. Utendaji ni wa KIHUNI tu. Hakutakuwa na jipya mpaka Tanzania kutakapokuwa na mfumo wa uwajibikaji au kuwawajibisha haya MAJIZI kwa manufaa ya UMMA.
Prof. Nkomo wa TCRA ni mzuri sana wa kuongea kwenye makongamano. Hopefully team yake inayo-monitor kero za watu mitandaoni italitupia jicho hili tatizo na kupatiwa ufumbuzi.
Promotions wa kadhaa tunazosikia na kuona mitandaoni, magazetini, kwenye luninga, n.k. huduma zake haziendani na kile kinachotangazwa. Bila shaka, huu ni mfano mmojawapo wa huduma zinazohadaa jamii.