2020 tukiwauliza viwanda viko wapi msitupige mabomu please

Wazo la kabwela

JF-Expert Member
Joined
Feb 13, 2013
Posts
1,901
Reaction score
1,511
Kwa wale waliomsikiliza Rais kwa Makini jana,baada ya kuomba mabango yasomwe kuna sauti zilisikika zikilalama. Ndipo Rais alipomuuliza RC Gambo "Wanasemaje?" Gambo akamwambia kilichosemwa. Rais alihamaki,akasema! Wapumbavu!!!

Daah! Hapa nadhani wanaarusha walijipambanua mbele ya Rais kwamba wao ni tofauti na watu wa mikoa mingine.

Rais angewasikiliza japo kiasi,mimi nadhani walitaka kumwambia arekebishe kuhusu bei ya sukari haikuwa Tsh. 5,000/= bali ilikuwa Tsh. 1,800/= na leo inauzwa Tsh. 3,000/=.

Rais wangu alikwazika kiasi cha kusahau kama yupo hewani na vipaza sauti vipo ON.

ANYWAY HOJA YANGU NI KUSHAURI RAIS WETU KAMA ALIVYOSEMA URAIS NI MATESO BASI KWA KULIJUA HILO HAPASWI KUKASIRISHWA NA WAKOSOAJI HUO NDIO URAIS WENYEWE.

POVU RUKSA...
 
Tatizo lake hataki kushauliwa na kusikiliza watu wanasema nini.
 
Hahahaha imebidi nicheke tu amesahau Mara hii
 
Hahahahaha sasa sijui 2020 watasemaje maana sipati picha zile ahadi za mil 50 kila kijiji zitatimizwaje??
 
Dah! bora umechokonoa. nimefadhaika sana kushuhudia kiongozi wa namna hii. tena hadharani. nilijua nimesikia vibaya, kumbe ilikuwa mubashara kwa taifa zima... hata kama tuna hasira, kiongozi lazima atafakari kila neno..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…