14,000 wapata nafasi UDSM

Replica

JF-Expert Member
Joined
Aug 28, 2017
Posts
1,716
Reaction score
9,051

WANAFUNZI 14,000 kati ya 40,000 walioomba kujiunga na masomo ya juu wamechaguliwa kujiunga na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) katika mwaka mpya wa masomo 2017/18 unaoanza wiki hii.

Mkurugenzi wa Shahada za Awali katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Profesa Allen Mushi alisema hayo juzi. Alisema kulikuwa na ushindani mkubwa na waliochaguliwa ni waliopata alama za juu zaidi.

Alisema changamoto waliyokutana nayo katika udahili ni kuwa wanafunzi wengi waliomba chuo zaidi ya kimoja, hivyo pale chuo kinapowakubalia hakijui ni wangapi watakwenda hapo hivyo hilo liliwasumbua.

Alisema kutokana na hali hiyo, chuo kilitoa nafasi kwa wanafunzi waliochaguliwa kuthibitisha kujiunga chuoni hapo. “Hali hii imetufanya tufungue mtandao mara tatu ili watu ambao hawakupata waombe upya kujaza nafasi za ambao hawakuthibitisha kujiunga na chuo baada ya kukubaliwa,” alisema Profesa huyo.

Alisema awamu ya kwanza wanafunzi 2,800 hawakuthibitisha hivyo mtandao ulifunguliwa na ya tatu pia ulifunguliwa ili kutoa haki kwa waliosema mtandao uliwasumbua au walichelewa kupata taarifa hizo.

Alisema mfumo wa mwaka huu wa kutoa uhuru kwa mwanafunzi kuchagua chuo anachokipenda ni mzuri lakini changamoto ni wanafunzi kuomba zaidi ya chuo kimoja kuogopa kukosa kabisa walikotarajia.

Ofisa Mahusiano ya Umma UDSM, Jackson Isdory alisema wanafunzi wa mwaka wa kwanza watafungua chuo Oktoba 28, mwaka huu na wanaoendelea Novemba 4. Alisema wanafunzi wa mwaka wa kwanza wanawahi ili kupewa maelekezo na taratibu za chuo hicho, kuyajua mazingira yake na pia kujisajili chuo.


CHANZO: Habari Leo
 
Madogo hongereni sana mmefanya maamuzi mazuri sana ya kuchagua chuo cha Taifa na kuvipa kisogo vyuo vya tarafa...karibuni sana UDSM madogo
 
Tatizo wamepangia wengi course wasizozipenda, na vyuo vingine wamewapangia course wanazozipenda.
Hii ndio imesababisha wengi wetu kukipenda chuo lakini course sio.
Binafsi nlitamani kusoma udsm ila wamenipanga course ambayo sijaipenda. Namshukuru Mungu nimepata course ninayoipenda mzumbe.
 
Chuo utakaa maximum miaka mitano na kozi utakaa nayo maisha yako yote

Ni mara mia uchague kozi unayoipenda kwenye chuo usichokipenda
 
Kwenda udsm ni kupoteza muda. Hiki chuo siyo cha kusomea kwa sasa
 
Kila chuo kwa sasa kina faculties ambazo kipo vizuri huwez kuta chuo kinatoa faculties zote nondo
 
udsm ni jicho la kila taasisi ya umma,,nasubir wasiwape mikopo ndo vyuo vyote vifungwee
 
Kwa First year UDOM unapokuja kuripoti pale UDOM siku ya Jumamosi Usikose kupata T-shirt yako ya UDOM - BOY and UDOM - GIRL OG kabisa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…