Mpaka sasa klabu ya Petro de Luanda kutokea nchini Angola ndiyo inayoongoza kwenye msimamo wa Kundi D, michuano ya CAF Champions League hatua ya makundi mara baada ya kuitandika Simba SC chuma moja kwa sifuri katika dimba la Benjamin William Mkapa, Jijini Dar es Salaam.