Winga wa zamani wa Yanga SC raia wa Afrika Kusini, Mahlatse ‘Skudu’ Makudubela amejiunga na Wiliete Sport Club de Benguela ya Angola baada ya kuachana na AS Vita ya DR Congo.
Makudubela mkataba wake na AS Vita ulimalizika Juni 30, 2025, na amejiunga na klabu hiyo ya Angola kama mchezaji huru.