Simba imemaliza utata wa Dabi ya Kariakoo baada ya kuweka taarifa za kuwa tayari kucheza mchezo huo kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii.
Simba ilikua kimya kwa muda mrefu kuhusu mchezo huo, hali ambayo iliibua maswali kwa mashabiki wengi waliokuwa wanataka kufahamu msimamo wa timu hiyo...