Profesa wa Uchumi, Samuel Wangwe, amesema nchi za Afrika zinapaswa kuweka kipaumbele katika kuongeza thamani ya rasilimali zake ili kunufaika ipasavyo na utajiri uliopo barani humo. Amesema miongoni mwa njia muhimu ni kuwekeza kwa vijana kwa kuwapeleka kujifunza katika mataifa yaliyopiga hatua...