Aliyekuwa Mbunge pekee wa Chadema kutoka Nkasi Kaskazini, Aida Kenani amewaaga wapiga kura wake akisema kama atagombea hakuna wa kumshinda. Hata hivyo, amesema hawezi kusaliti mapambano.
Chadema imeweka msimamo wa kuzuia uchaguzi hadi mabadiliko yatakapopatikana, maarufu "No Reforms No Election."