Jaji mstaafu wa Mahakama ya Juu ya Uganda, Profesa George Kanyeihamba, amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 84. Kifo chake kimethibitishwa na msaidizi wake binafsi aliyejitambulisha kwa jina la Denis, ambaye alisema Profesa alifariki katika Hospitali ya Nakasero alipokuwa akipatiwa matibabu...