Nchini Rwanda kuna falsafa muhimu sana inayotumiwa kumaanisha kiwango cha juu kabisa cha Uzalendo na kuwalinda Wananchi na maslahi yao.
Falsafa hiyo inapatikana kwenye neno Inkotanyi. Neno hili linamaanisha nguvu ya pamoja inayofanywa kwa ujasiri ili kulinda Wananchi na kusimamia maslahi mapana...