Watanzania tujifunze Kiswahili tuache ujanja ujanja!

UMUGHAKA

JF-Expert Member
Sep 1, 2021
2,240
11,068
Nsikuchoshe na Usinchoshe,tusichoshane!


Nimekuwa nikishangazwa na maneno haya mawili (2) ambayo yamekuwa yakitumika sana na jamii mbalimbali ya watanzania!.

Maneno hayo ni :-

1.Uzuri
2.Urembo

Haya ni maneno mawili tofauti,lakini watanzania wengi wamekuwa wakidhani ni neno moja likilokamilika!.

1. UZURI - Ni neno ambalo limekuwa likutumika sana kwa kusifia au kutoa pongezi!

2.Urembo - Ni neno vilevile ambalo limekuwa likitumika kusifu na kutoa sifa kwa vitu mbalimbali!.



UTOFAUTI!


1.UZURI - Ni kariba au haiba ya kitu ambacho kimeumbwa na asili yake!,Uzuri ni kitu ambacho akihitaji nyongeza ili kukinasibisha au kukiongezea uzuri wake wa asili!.


Mfano!.

Ukimuita Mwanamke "Mzuri" ni lazima mwanamke huyo awe ambaye hajatumia vipodozi au mekapu kuuongezea uzuri wake!.

Mwanamke mzuri ni lazime awe mzuri wa kiasili!.

2.Urembo - Ni kariba au haiba ya kitu ambacho kimeongezwa nakshi nakshi ili kivutie mbele ya kadamnasi!.


Mfano !:-

Ukimuita mwanamke "Mrembo" ni lazima mwanamke huyo atakuwa anatumia vitu ambavyo si vya asili ili kuendelea kuvutia mbele ya kadamnasi!,anaweza kuwa anatumia mawigi,mekapu au wanja ili aonekane mzuri na avutie!.


Kwa kifupi mtu au Mwanamke Mrembo ni yule ambaye anatumia Artificial things ili mradi aonekane anapendeza mbele ya kadamnasi!


Kama kuna sentensi tata,methali, Nahau au Msamiati mgumu,nadhani ni muda wa kuwatumia BAKITA kwa ufasaha na usahihi kwa sababu wanatumia kodi ya watanzania bure na wanaonufaika siyo watanzania bali Wananzengo kutoka KENYA,RWANDA,KONGO na ZAMBIA
 
Back
Top Bottom