Zumaridi hana kesi ya kujibu

Suley2019

JF-Expert Member
Oct 7, 2019
1,817
4,568
1670328717156.png

Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Mwanza imesema Washtakiwa 81 kati ya 84 akiwemo Diana Bundala maarufu Zumaridi katika kesi namba 12 ya kufanya kusanyiko lisilohalali na shambulio la kudhuru mwili hawana kesi ya kujibu.

Hakimu Mkazi Mwandamizi Clescensia Mushi akisoma uamuzi huo amesema pasina shaka Mahakama imejiridhisha kwamba Washtakiwa walioachiwa huru katika kesi namba 12 hawakuguswa na vipengele muhimu vinavyotakiwa kuthibitisha makosa ya jinai.

Washtakiwa watatu kati ya 84 ndio wamekutwa na kesi ya kujibu kwa mujibu wa sheria ambao ni Juma Khamis mshtakiwa namba 05, Meshack Joseph namba 33 pamoja Daud Manyanda namba 45, ambapo Hakimu Mkazi Mwandamizi Clescensia Mushi akaihairisha kesi hiyo na itatajwa tena December 20, 2022 kwa washtakiwa watatu.

Hata hivyo Diana Bundala maarufu Zumardi bado anakabiliwa na kesi mbili ambazo ni kesi namba 10 Shambulio la kuzuia Maafisa wa Serikali kutekeleza majukumu yao na kesi namba 11 ya usafirishaji haramu wa binadamu.
 
Mahakama ya Hakimu Mkazi mkoa wa Mwanza imewaachia huru washtakiwa 81 kati ya 84 akiwemo Diana Bundala maarufu 'Mfalme Zumaridi' kwenye kesi namba 12/2022.

Katika kesi hiyo Zumaridi na wenzake walikuwa wanakabiliwa na shtaka la kufanya kusanyiko lisilo halali, kosa wanalodaiwa kulitenda nyumbani kwa mhubiri huyo mtaa wa Buguku kata ya Buhongwa jijini Mwanza.

Akisoma uamuzi huo leo Jumanne Desemba 5, 2022, Hakimu Mkazi Mwandamizi wa mahakama hiyo, Clescensia Mushi amesema mahakama imejiridhisha pasi na shaka kuwa washtakiwa walioachiwa huru hawakuguswa na vipengele vinavyotakiwa kuthibitisha makosa ya jinai.

Chanzo: Mwananchi
 
Hawakuwa na shida na sheria bali ni biffu na waliomkamata bila utaratibu
 
Jamani huyu Zumauridi sijui Zumanani si ameachiwa kesi yake imeisha leo au nlikua naota.
 
Mungu wa Wakristo huwa alipiganiwi wala kuhitaji msaada wa Mwanadamu amsaidie, yeye hata ajiite baba yake na mungu atajuana yeye na Mungu,
 
Back
Top Bottom