njiwaji
JF-Expert Member
- Jul 15, 2015
- 279
- 202
Zuhura(Venus) na Mwezi Hilali pamoja kesho Jumatatu Alfajiri kuanzia saa 11.30AM 18.Sept.17
Sayari ya Zuhura na hilali ya Mwezi zitatoa mandhari ya kuvutia zitapoonekana alfajiri kesho. Duara ya hilali inaangalia Zuhura ambayo inang'aa kwa ukali sana.
Kuna nyota moja iitwayo Regulus pia itakuwa jirani zaidi na Mwezi.
Pamoja na hiyo kuna sayari mbili zingine chini karibu zaidi na upeo, Mirhi (Mars) na Utarid (Mercury) ambazo utaziona ukiangalia vizuri katika mwanga wa Jua kabla tu ya kuchomoza upeo wa mashariki. Mirihi itaonekana kwa uwekundu.