Zuberi Mtemvu: Mpangaji mikakati wa TANU na muasisi wa upinzani

Mohamed Said

JF-Expert Member
Nov 2, 2008
20,925
30,273
ZUBERI MTEMVU: MPANGAJI MIKAKATI WA TANU NA MUASISI WA UPINZANI

o3yh0kDTiNcQlCSz2tfrbZqyvDxMlux2SVEVS9ZPocl0UoqwHRvOovD2nF06NGgWnC9L2hdZ3H9zIxwaNFQBDXoqAnGAs1siwu20fKYl1RaY6N_4FL2drI5PYgcYtDvaHyvmfBEnBH8MFtgU-1NdqLelBQiFYl0R12_0I0SwVlj4noN09YjLHxvbwL2ouyS_EZriHzzEN6kBPPnbob1C2IHRV1pQ7m5bbeNeqdxuGvEwBg5rW0Td8VGJF1MlIZiVt6RY2XxwZizK3ftSx-zjsV3z7XJ5S-9dD-N5WvBFMwtGgb4iVAzI-rfbF9hnsUJvpW8NZD7pcUTgNa6Tg3Ezm_t7p4uA_b0Mz0fY3QvniK0Jc4VU7cGwSSOvpF8-NWJk6IAV9bwxb9Ho71Y6zF3JGuu6tVwwAmfzU5H8eYYrXkqEX6muIiOHbC2HJ5eUEOO6H29b4vbRt61Xx5hNIkVOHB3CN9LbL8IdHcSwR8Puc9-IgMY-4jV8Z8ce4SwyDwntuI9bbpt6v7QthhAhQn104j_LQlq5V2FLFJXb3kT-oZsivOcJ9cVYBZdC5AfdsFw8ZzCBIoYAZO1C1Jtmb24anc9BpbzkeTP78p6Pm18XwQnCI04ZzA=w438-h692-no


IogchVui18NrygovxS4B2Uyzsa-IpdeG7bIax1lHOYLVrJbfLwo0rP3TKEoVdncdc4rtGtnj3lXAJJB2T8UMCuiYu33NvXGYxRgwstlfilgjEUEZ3wtZ87rOJ9x1lFrcpQ3mMjVxrVuOel2PvYaZDpiDxMxRcAE1JD9J2OarCBQKMAkQbZfosIpuSMpHz1h0brNFUE0pt5d5xp9Tce0zTb53rGpntSFmz-ncaXOBdvcHS-AlQQN_8KSYIIL9noZ5TorvOC2fEKFJclwMpINENByrJGjo_eV3AfebetH9n3oYxOU2v9tEZ28mgkOdOv-l6DWvKU59MhAIyMbLsOlqDT2vBhxk_SlOaXowwORnGgo02qwtu-SpJfML8I7Cn_VicTaT6osi6KiL-hmEdeJA5PyyTHkIYbQ3P7ettOpWeOxoNI-uvw75ngKCSci9w2trZCR9MmpxwaS60s3G46nXp1CaNPxFGQa_g9H4EDeGfEFIGESh3rXvmO-fXiAElrcEREpiF9QDg_XkJwiBr9b3p3WTgskGKaAHZNO7LoClLbsuZKzoJU9lk6zSGAZZfuULShGcbrxfnOZDmG_TCVUBSySEUSUZlZoljZA34_Hv_dUA_3ypmQ=w287-h220-no

Rai Oktoba 28 - Novemba 3, 1990

=======

Alhaj Zuberi Mwinshehe Manga Mtemvu
Mpangaji mikakati wa TANU, mhamasishaji wa umma, muasisi wa upinzani na mpinzani wa kweli

Na Mohamed Said
MTEMVU alikuwa mpinzani akipinga TANU na ingawa alirejea TANU baada ya uhuru stigma haikuwaimefutika. Wakati ule TANU ilikuwa na nguvu na kwa mtu kuipinga TANU ni sawa na kujizika mwenyewe ungali hai. Hakuna mtu aliyependa kuwa karibu na mpinzani wa TANU hata kama mpinzani huyo alikuwa kesharejea TANU.

Nilipokuwa napata akili na kuanza kusomeshwa historia ya uhuru wa Tanganyika nikawa namuelewa Mtemvu kama mpinzani wa Mwalimu Nyerere na mtu aliyetaka kudhoofisha harakati za uhuru kwa kuipinga TANU. Hii ndiyo historia mashuhuri inayofahamika kuhusu Mzee Zuberi Mtemvu. Nilipokuwa mtu mzima na kujua mambo kwa dhahiri yake nikaja kumfahamu Mzee Mtemvu kwa undani zaidi. Mtemvu alikuwa mzalendo na mtu mkweli. Mtemvu alikuwa si kati ya wale "msujudie upate mradi wako".

Zuberi Mtemvu alikuwa kati ya wanachama wa mwanzo shupavu na msomi kabisa kujiunga na TANU na alikuwa mwanachama wa tatu kuacha kazi ya kuajiriwa ili akitumikie chama. (Mwanachama wa kwanza kuajiriwa na chama alikuwa Alexander Tobias aliyeacha kazi na kuajiriwa na TAA wa pili alikuwa Mwalimu Julius Nyerere aliyeacha ualimu na kufanya kazi ya TANU na mzalendo wa tatu alikuwa Zuberi Mtemvu).

Mtemvu alikuwa akiishi Somali Street jirani na nyumba ya akina Sykes. Baba yake Mtemvu, Mzee Mwinshehe Manga Mtemvu, alikuwa amejenga nyumba yake nyuma ya nyumba ya Kleist Sykes. Kwa hiyo Mtemvu hakushikwa na mtu mkono kuingizwa TANU kwa kuwa hiyo mitaa ndiyo chimbuko la TANU. Mwalimu Nyerere alipokuja kufahamiana na Abdulwahid na Ali Sykes, Dossa Aziz, John Rupia na viongozi wengine wa TAA mwaka wa 1952, Mtemvu akawa mmoja wa watu wa mwanzo kuwa karibu na Nyerere.

Mtemvu alikuwa na kipaji cha kuzungumza kama alichokuwanacho Nyerere, halikadhalika alikuwa na kipaji cha kuweza kushawishi na kuwashirikisha watu katika harakati. Takriban mwezi mmoja baada ya kuundwa kwa TANU mwaka 1954, Nyerere na Mtemvu walikwenda kuifanyia kampeni TANU huko Morogoro ambako ndiko ilipokuwa asili ya ukoo wa Mtemvu. Baba yake Mtemvu, Mzee Mwinshehe, alikuwa ameongea na baadhi ya wazee wenzake kuhusu TANU mjini Morogoro.

Ijapokuwa Nyerere alijaribu kwa uwezo wake wote kuwafikishia watu ujumbe wa TANU matokeo hayakuwa mazuri. Mzee Mtemvu ana picha na nyaraka muhimu sana kwa mtafiti yeyote atakaye kufahamu kuhusu historia ya TANU na siku za mwanzo za Mwalimu Nyerere katika siasa. Katika barua ambayo Mtemvu alimwandikia Ally Sykes mnamo tarehe 15 Agosti, 1954 aliwaelezea watu wa kabila lake kama 'wagumu'. Inaaminika hii ndiyo ilikuwa safari ya kwanza kwa TANU kuanza kujitangaza hadharani. Ndani ya barua hiyo Mtemvu alimjulisha Ally Sykes kuhusu mwanachama mpya wa TANU, Ally Mwinyi Tambwe. Wakati ule Tambwe alikuwa Katibu wa Al Jamiatul fi Tanganyika. Mchango wake mkubwa ukiacha kuipa TANU uongozi wa wasomi ilikuwa kutumia ushawishi wake kwa mweka hazina wa Al Jamiatul Islamiyya Ali Jumbe Kiro kuruhusu fedha nyingi sana za jumuia hii ya Waislamu kutumika katika harakati za uhuru na hasa katika kufanikisha safari ya kwanza ya Mwalimu Nyerere kwenda Umoja wa Mataifa kudai uhuru wa Tanganyika mbele ya Baraza la Udhamini mwaka 1955.

Zuberi Mtemvu alikuwa kati ya watu wa mwanzo kabisa kufikisha chama kwa wananchi. Katika barua hiyo iliyomwandikia Ally Sykes, Mtemvu aliomba kadi mia mbili ili atafute wanachama. Kitu cha kufurahisha ni kuwa kadi ya Mtemvu ya TANU aliandikiwa na Ally Sykes hii ni pamoja na kadi ya Mwalimu Nyerere ambayo ni kadi namba moja. Inasikitisha sana kuona kuwa nyaraka hizi muhimu katika kumbukumbu ya nchi yetu hadi leo hii bado zimeachwa katika mikono ya watu binafsi badala ya kuwa katika Makumbusho ya Taifa kama kielelezo cha historia ya Tanganyika.

Historia inaonesha kuwa Mtemvu alikuwa mmoja wa wazalendo waliotayarisha mkutano wa TANU wa kwanza uliofanyika Ukumbi wa Arnautoglo ambao haukuhudhuriwa na watu zaidi ya ishirini. Mkutano wa uzinduzi wa TANU ulihudhuriwa na kikundi kidogo cha takriban watu 20 miongoni mwao Julius Nyerere, Abdulwahid na Ally Sykes, Dossa Aziz, John Rupia, Mshume Kiyate, Makisi Mbwana, Jumbe Tambaza, Juma Waziri, Clement Mtamila, Rajabu Diwani, Schneider Abdillah Plantan, Marsha Bilali, Rashid Ally Meli, Frederick Njiliwa, Idd Faiz Mafongo, Idd Tulio, Denis Phombeah na wengineo.

Tangazo la mkutano huu lilichapishwa katika gazeti la Ramadhani Mashado Plantan Zuhra. Lau kama mwaka wa 1954 Mashado na Mtemvu walikuwa pamoja ndani ya TANU wote wakiwa wahamasishaji wakubwa wa umma miaka minne baadae walitupana mkono na Mwalimu Nyerere na kuanzisha vyama vya upinzani. Mtemvu akiongoza Congress na Mashado All Muslim National Union (AMNUT). Hapa ningependa kueleza kuwa katika wanachama wa mwanzo katika TANU alikuwa Mzee Said Chamwenyewe. Huyu alikuwa mwanachama shupavu wa TANU na alikuwa karibu sana na Mtemvu na Mwalimu Nyerere.

Mtemvu alipohama TANU kuunda chama chake cha upinzani, Said Chamwenyewe alitoka TANU na kujiunga na Mtemvu katika Congress. Umuhimu wa Chamwenyewe ni kuwa Msajili wa Vyama alipokataa kuisajili TANU kwa kisingizio kuwa haina wanachama, marehem Abdulwahid Sykes alimpa Chamwenyewe kitabu cha rejesta na kadi za TANU akamuomba aende Rufiji akatafute wanachama. Mpaka hapa msomaji atakuwa ameshaona Mtemvu alikuwa akafanya na watu wa aina gani na yeye alikuwa na mchango gani katika kuijenga TANU.

Katika TANU kulikuwa na kundi la wasomi wengi wakiwa wamezama sana katika nadharia za staili ya Fabian Society. Hawa fikra na kuchanganua mikakati ilikuwa zaidi kuliko kufanya vitendo vyenyewe. Kundi hili lilikuwa likiongozwa na Abdulwahid Sykes, Hamza Mwapachu na Mwalimu Nyerere. Halafu kulikuwa na kundi la wale waliokuwa hawaoni tabu kuandika mada na kufanya michanganuo ya fikra na mikakati lakini waliona ili TANU ifanikiwe wananchi wafundishwe na kuhamasishwa kupinga dhulma kwa dhahiri hata kama itakuwa kwa kufanya hivyo watakuwa wanavunja sheria za wakandamizaji. Huu ulikuwa uwanja wa Zuberi Mtemvu, Ally Sykes na Steven Mhando. Kwa ajili ya msimamo wao huu Waingereza wakawaita "wakomunisti". Taarifa za kijasusi za Waingereza zinamueleza Mtemvu kama "Mkomunisti, mtu asiyejali sheria".

Ilikuwa katika kipindi hiki cha Kuijengea TANU misingi imara ya uongozi ndipo Mwaimu Nyerere alimshauri Mtemvu aache kazi serikalini aajiriwe na TANU. Mtemvu alikubali ushauri ule na akaacha kazi. Mtemvu akawa Katibu wa kwanza wa TANU. Tutaona hapo baadaye kisa cha Mtemvu kutupana mkono na Nyerere na TANU.

Mtemvu akiwa Katibu Mwenezi alikuwa na kazi ngumu ya kuwashawishi na kuwashirikisha watu kujiunga na kusajili matawi ya TANU. Ili kampeni ya kuwaingiza watu ifanikiwe na ujumbe wake uwafikie wananchi ilibidi TANU ifanye mikutano ya hadhara. Kwa bahati mbaya serikali ikawa haitaki kutoa kibali cha TANU ili ifanye mikutano. TANU ilijikuta katika hali ambayo haiwezi kuwasiliana na watu kuwatayarisha katika harakati za kuhamasisha umma. Katika hatua kadhaa za ujasiri Mtemvu alifanya mikutano ya hadhara bila ya kupata kibali cha serikali. Nyerere mtu wa hadhari hakutaka kuonekana anavunja sheria. Alifahamu kwamba vitendo kama hivyo vingesababisha matatizo kutoka serikalini.

Jambo kama hilo lilikuwa sawa na kuikaribisha misukosuko bila sababu ambayo ingeathiri chama na uongozi wake wote. Nyerere, kama Rais wa TANU, alikuwa amepokea barua kadhaa kutoka kwa Chief Secretary, T. Griffith-Jones, kuhusu mikutano isiyokuwa na kibali aliyokuwa akiifanya Mtemvu. Lakini kwa hakika kwa TANU kunyimwa haki ya kuitisha mikutano ilikuwa sawasawa na kuifunga mikono. Hakukuwa na namna nyingine TANU ingeweza kufanya ili iwasiliane na watu. Kuacha kufanya mikutano TANU ingebakia dhaifu na harakati zingekufa. Mtemvu alikuwa akifahaamu kuwa serikali ilikuwa imedhamiria kabisa kuinua TANU ingali bado changa. Akiwa bado amenaswa katika kitendawili hicho cha 'kibali cha kufanya mkutano', Mtemvu alipata nakala ya mkutano wa 674 wa Baraza la Udhamini la Umoja wa Mataifa ambayo Attorney General, Gratten Below, alifafanua juu ya msimamo wa serikali kuhusu suala hilo. Mwanasheria Mkuu aliarifu kwamba watu wanaweza kuanza shughuli za chama mara tu maombi ya usajili ya chama cha siasa yatakapowakilishwa; na wanaweza kuendelea na shughuli za siasa mpaka majibu kutoka kwa Msajili Mkuu yamepokelewa kwamba tasjili imekataliwa.

Uongozi wa TANU katika makao makuu ulisisimka kwa taarifa hiyo iliyofukuliwa na Mtemvu.
 
Mzee Mohamed Said
Mbona maandishi hayaonekani hayo!!?
Halafu pia Mtemvu nadhani alikuwa ni mtu wa upinzani, nafikiri aliunda chama chake cha ANC.
Sababu za kupIngana na TANU ndio sizijui
 
Mzee Mohamed Said
Mbona maandishi hayaonekani hayo!!?
Halafu pia Mtemvu nadhani alikuwa ni mtu wa upinzani, nafikiri aliunda chama chake cha ANC.
Sababu za kupIngana na TANU ndio sizijui
Iceman...
Hiyo nimeweka kama kumbukumbu tu nimeiona jana katika maktaba yangu.

Hizo ni makala ambazo zilichapwa na gazeti la Rai wakati wa kifo cha Baba
wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere.

Unaweza kusoma historia ya Mtemvu hapo chini:
Mohamed Said: ZUBERI MWINSHEHE MANGA MTEMVU MZALENDO ALIYEKUWA NA MSIMAMO MKALI WA “AFRIKA KWA WAAFRIKA”
 
Iceman...
Hiyo nimeweka kama kumbukumbu tu nimeiona jana katika maktaba yangu.

Hizo ni makala ambazo zilichapwa na gazeti la Rai wakati wa kifo cha Baba
wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere.

Unaweza kusoma historia ya Mtemvu hapo chini:
Mohamed Said: ZUBERI MWINSHEHE MANGA MTEMVU MZALENDO ALIYEKUWA NA MSIMAMO MKALI WA “AFRIKA KWA WAAFRIKA”
Nashukuru sana mzee Mohamed Said nimesoma na kuelewa
Swali langu ni je ANC ilichukuwa wana chama wengi kutoka TANU!?
Na je wewe una mjaji Mtemvu kama msaliti wa wapigania uhuru au ungependa historia imuweke mtemvu kwenye kundi lipi!!?
 
Iceman...
Kwa kauli yake mwenyewe Mzee Mtemvu alinambia kuwa TANU ilikuwa na nguvu sana.

ANC haikuweza kupata wanachama wengi.

Mtemvu akimwita Nyerere msaliti na Nyerere pia akimuona Mtemvu msaliti.

Kila mmoja alikuwa na sababu zake.

Mtemvu hakuona kama kulikuwa na haja ya kuwapa nafasi Wazungu na Waasisi Tanganyika.

Nyerere yeye alimtuhumu Mtemvu kwa kuipinga TANU.

Binafsi naona TANU ilifanikiwa sana kwa kufungua milango kwa Wazungu na Waasia.
 
Dah.. nimekusoma Mzee katika website yako

Hivi hawa akina Sykes ndio chimbuko la msanii Dully Sykes? au hawana uhusiano wowote?
 
Al Sady...
Ahsante sana.
Kiukwelii mzee mohammed ..umenitoa katika ujinga niliomezeshwa katika historia zetu za shule ya msingi . Nilianza kufuatilia maandiko yako nikiwa DAR mbagala charambe ...nilikuwa nipo na mwanasheria flani nyumbani kwake nilikuwa najiaandaa kwenda masomoni nje ya nchi ...aliniuliza maswali je taifa lako unalijua vizuri nikaaelezaa nalijua nikamsimulia akanambia ujalijua ...akanipa kitabu chako cha HARAKATI MAISHA YA ABDULLWAHEED SYKES .
kukwelii nilikisoma sana na mwishowe nilikuwa naumia sana hasa selemani takadiri anapokuja kukataria na nyerere .pia nikajua siasa mbaya hasa pale TEWA SAID TEWA anapopelelekwa ubalozi .ili kumuuwa kisiasa ndipo nikajua leo dau wanampa ubalozi ili kumzima tu .
MZEE UNASTAHIRI PONGEZII SANA KWA KUHIFADHI HISTORIA HII YA TAIFA LETU.
 
Kiukwelii mzee mohammed ..umenitoa katika ujinga niliomezeshwa katika historia zetu za shule ya msingi . Nilianza kufuatilia maandiko yako nikiwa DAR mbagala charambe ...nilikuwa nipo na mwanasheria flani nyumbani kwake nilikuwa najiaandaa kwenda masomoni nje ya nchi ...aliniuliza maswali je taifa lako unalijua vizuri nikaaelezaa nalijua nikamsimulia akanambia ujalijua ...akanipa kitabu chako cha HARAKATI MAISHA YA ABDULLWAHEED SYKES .
kukwelii nilikisoma sana na mwishowe nilikuwa naumia sana hasa selemani takadiri anapokuja kukataria na nyerere .pia nikajua siasa mbaya hasa pale TEWA SAID TEWA anapopelelekwa ubalozi .ili kumuuwa kisiasa ndipo nikajua leo dau wanampa ubalozi ili kumzima tu .
MZEE UNASTAHIRI PONGEZII SANA KWA KUHIFADHI HISTORIA HII YA TAIFA LETU.
Al Sadly,
Ahsante sana.
 
Back
Top Bottom