Zoezi la kuhakiki mali za vigogo kuanza Februari 20

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,318
33,125
VIGOGO wapatao 60 wataanza kukaguliwa mali zao ili kuweza kuhakiki mali hizo walivyozipata ikiwa ni mchakato ulioundwa na serikali kukagua viongozi wote wa watumishi wa Umma wa nchini
Mchakato huo utaanza Februari 20 mwaka huu na kumalizika mapema Machi, ambapo Tume ya Maadili ya Viongozi wa Umma wataendesha zoezi hilo kwa vigogo hao

Hiyo imekuja baada ya kurejeshwa kwa fomu za utalaji kwa viongozi wote wa watumishi wa Umma wa Serikali kukamilika

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana ,Kamishna wa Tume ya Maadili, Jaji Mstaafu Salome Kaganda alisema kuwa, uhakiki huo ni nguzo bora ya kuijenga jamii ya Watanzania, hasa viongozi wa umma katika kuishi kwa kufuata misingi ya uadilifu, iliyowekwa na Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma.

Amewataja baadhi ya viongozi watakaoanza kukaguliwa ni akiwemo Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta , Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano) Hawa Suluhu Mbunge John Mnyika na wengine wengi wakiwemo na wakuu wa mikoa, wilaya, MaMeya wa majiji, madiwani, wabunge na wakurugenzi wa taasisi mbalimbali za Serikali nchini.

Kaganda aliwaambia wanahabari kuwa, si kwamba viongozi watakaonzwa kuhakikiwa wana kashfa wala tuhuma zozote si kweli bali ni sheria kwa viongozi kama hao kuhakikiwa mali zao na kuwaondoa hofu viogozi hao na kuwaomba ushirikiano katika zoezi hilo

Amesema kuwa lengo lingine la kukagua viongozi hao ni kuboresha utumishi wa umma kwa kuwa sasa uadilifu umeonekana kushuka ikiwa na serikali kufanya utafiti wa kisheria zaidi kutaka kutenganisha biashara na uongozi

“Sisi tunachokiomba kutoka kwao ni kutoa ushirikiano wa kutosha kwa maofisa wetu wakati wa zoezi zima la uhakiki wa mali zao,” alisema Kaganda

Chanzo.. Zoezi la kuhakiki mali za vigogo kuanza Februari 20
 
Wanafuja tu hela zetu hiyo tume ya maadili na utumishi wa umma.
Serikali yote kwa ujumla imeoza, kwa kuwa tu uadilifu ni suala ambalo limefumbiwa macho. SHERIA ZIPO NYINGI SANA TATIZO HAKUNA ANAYEZISIMAMIA NA KUZITEKELEZA. Kwa hiyo anayefanya kosa ni sawa tu na asiyefanya kosa kwa kuwa hakuna adhabu yoyote. Hatuwezi kwenda mbele.
 
Tume ya maadili ni JANGA la taifa haifai kitu. Wanalipwa kwa kitu wasichokifanyia kazi. Hivi sasa viongozi wengi wamejitajirisha kifisadi, na wengine wanamiliki mali nyingi kwa majina ya watu wengine. Haya tume inayajua lakini hawamgusi mtu!. Tume hii ife wapewe vijana wenye uchungu na nchi.
 
huyo kaganda mbona kafreeze hata kabla ya zoezi?baada ya kuanza na kina chenge,lowasa,Jairo,manumba wanaanza na kina mnyika,sugu hivi huu si umbumbumbu?
 
Hivi hili zoezi halina shinikizo la wafadhili? Nadhani kuonyesha kama zoezi hili ni serious, basi tume ingeanza na wale watumishi wenye tuhuma kwanza (wananchi wanawajua na wameshasemwa sana). Baada ya kujiridhisha wachukuliwe hatua. Zaidi ya hapo, zoezi hili litakuwa ni suala kuhamisha akili zetu kwenye mambo mengine
 
Back
Top Bottom