Zitto: Serikali isipowataja walioficha mabilioni nje, CHADEMA itawataja hadharani!

Say what you like but Zitto amejijengea heshima ya umakini bungeni. For that case, anachokifanya Zitto ni sahihi kwasababu ikiwa kama serikali haitaki kuwataja na kuwalazimisha kurudisha upinzani wanaweza kutumia nguvu ya bunge. Ikishindikana bungeni basi kwa kupeleka malalamiko UN na UN kwa kutumia security council na organs kuwalazimisha nchi wanachama kama Switzerland kurudisha hizo fedha nchini. Niliwahi kusema hivi mafisadi wasikimbilie kuficha hela nje kwani ulimwengu wasasa ni kama kijiji. Zitajulikana tu na pindi upinzani wa kweli ukishika nchi hizo hela zitarudi tu!!!!. Safi sana Zitto wewe ndio rais wangu wa 2015 najua unapambana na maadui wakali sana ila mmungu subhanawataala yuko pamoja nawe. Komaa nao tu sisi wanajeshi wa kujitolea tupo nyuma yako.
 
Ndugu yangu hutoi tu orodha ya majina. Kuna taratibu za kimikakati za kutoa majina hayo. Hili sio suala langu peke yangu, ni suala la kambi ya upinzani Bungeni na ni suala la CHADEMA. Mimi ni msemaji tu wa chama katika eneo hili. Nalifanyia kazi kwa niaba ya Kambi na chama na tutatoa orodha Bungeni. Hakuna haja ya haraka na kuanza kusema maneno yasiyo na maana dhidi yangu. Haisaidii. Inavunja moyo.

Hata orodha ya Mafisadi (List of Shame) tuliyotoa MwembeYanga mwaka 2007 September 15, hatukukurupuka na kutaja tu majina. Tuliifanyia kazi. Tulitangaza Jangwani wakati wa mkutano wa Buzwagi kwamba Serikali isipochukua hatua tutawataja. Haikuwa tu Katibu Mkuu aliibuka na kuanza kutaja majina. Tuliifanyia kazi na tuli build up momentum kwa zaidi ya wiki 3.

Hili la orodha ya Watanzania wenye akaunti za Benki katika Mabenki huko Switzlerland nalo tutalifikisha mwisho na wala hatuna papara nalo. Tumefuata taratibu za kupata orodha hiyo. Huko tumekumbana na kigingi cha barua ya kutoka TAKUKURU ambayo iliandikwa kwa Serikali ya Swistzerland kwamba orodha wapewe wao tu na baadhi ya maneno ambayo yameudhi mamlaka za huko.

Hii sio kazi rahisi. Badala ya kunibeza katika kazi hii inapaswa kutiana moyo. Kunibeza hakutasaidia kufanikisha moja ya jukumu muhimu kabisa katika vita dhidi ya ufisadi.

Kuna mtu kasema hapa nami nitaje nilizoficha ndani. Napenda kurudia kusema mimi sio tu sina mabilioni, hata mamilioni sina. Ninaishi kwa mshahara wa kazi yangu ya ubunge. Sina biashara na wala sitarajii kufanya biashara nikiwa mbunge. Ninaamini katika miiko ya uongozi, kwamba Kiongozi wa Umma atumikie Umma. Mtu yeyote mwenye ushahidi wa biashara ya Zitto aonyeshe hapa. Mtu yeyote mwenye chembe ya ushahidi wa mabilioni ya Zitto aonyeshe hapa. Wakati mwingine hizi propaganda za kiasiasa zinafunga akili za watu. Sina utitiri wa magari. Nina gari 2 tu sasa, Toyota Vista ninayotembelea na Landrover Freelander ambayo hata sijamaliza kuilipia kodi. Nikiwa Waziri kivuli wa Fedha na Uchumi nimekataa hata kuchukua tax exemption kwenye kuagiza gari kwani ninapinga tax exemptions. Mwenye ushahidi wa gari yeyote niliyonayo tofauti na hizo aweke hapa. Kwanini tuwe na porojo zisizokwisha na bila ushahidi?

Sina nyumba Dar es Salaam wala Dodoma. Ninajenga nyumba kijijini kwangu Kibingo,Mwandiga Kigoma. Dar es Salaam napanga. Dodoma nakaa Hotelini. Sina hata kiwanja Dodoma, sijawahi kuomba kiwanja na wala sitegemei kufanya hivyo maana sina mpango wa kuishi Dodoma wala Dar es Salaam. Nina shamba la Korosho mtwara lenye mikorosho 400 na kiwanja eneo na Mangamba. Nina shamba ekari 3.5 Mbutu Kigamboni.

Nina akaunti NMB na CRDB tu. Mwenye ushahidi wa mimi kuwa na akaunti Benki nyingine yeyote aweke hapa. Tuacheni porojo ndugu zangu. Niacheni nifanye kazi. Nikosoeni ninapokosea. Tushirikiane panapotakiwa. Sio kila siku kushambuliwa tu bila sababu. Wenzetu Greece hii kazi ninayofanya inafanywa na magazeti ya kiuchunguzi.

Soma hii hapa uone wenzetu walichofanya.

Nakuunga mkono 100% dont be pushed by crowed....Kama ulivyosema nenda systematic na kama unabaraka ya system nzima then dont be deceived ukatoka nje ya collectivity hii itakusaidia usiwe attacked kama individual..Remember umoja ni nguvu..Wanaopayuka achana nao just be sober alafu fanya kwa pamoja na kwa uhakika ili kuwaweza hao mafisadi wasio na huruma na damu ya watanzania wanao kufa kila siku hosipitali kwa kukosa 500 ya dozi ya malaria....

Nina uhakika Zitto you are innocent hakuna aliyeniambia hili nalijua na hata naweza thubutu kusema nimelihakikisha..So achana nao..Lakini kimoja tu punguza emotion wasikusumbue mara nyingine wanataka kuku provoke na kusababisha utamke jambo ambalo litakuwa a political pot hole?! kwako..So jaribu tu kuwa mwangalifu.

Goooo ZZK Goooooooo behind you tupo wengi na sala zetu zipo na wewe!
 
Kama hujui MUNGU amewahi kuwa upande wa farao katika harakati za Musa kuwakomboa wana wa israel kutoka misri, ili ukuu na utukufu wake udhihirike kwa wenye shingo ngumu kama wewe peri na Pasco.

Hivi kati ya Farao na Musa nani aliyeshinda na nani alieshindwa?
Nani aliangamizwa na kwanini aliangamizwa?
 
zitto hajui asemalo na asemehewe sasa anaanza kuleta visingizio ooh barua aliyoandika Hosea imemfanya akose taarifa ...unafiki tu hajui atendalo. Kwanza aseme harusi yake na mtoto wa JK lini maana tunajua yanayoendelea bagamoyo
 
zitto go on ur have majority power behind you!! binafsi pia napata walakini na wanaompinga zitto nilazima tukomae kifikra na tuachane na siasa za ushabiki uliojengeka katika misingi ya kiitikadi za siasa uchwara,kikabila na kiegoisim,Mtu anapoonyesha jitihada hatuna budi kumuunga mkono kama juhudi zake ni za heri kwa taifa letu.TUNAHITAJI VIONGOZI WAWANAOWEZA KUFANYA MAAMUZI JUU YA MATUMIZI YA RASILIMALI ZA TAIFA LETU KITUI AMBACHO BINAFSI NAONA ZITTO ANAWEZA KUSIMAMIA ,TUMPE NAFASI HATA YA KUKIONGOZA CHAMA MWAKANI ILI CHADEMA YA MABADILIKO ISIJE IKAPOTEA
 
zitto go on ur have majority power behind you!! binafsi pia napata walakini na wanaompinga zitto nilazima tukomae kifikra na tuachane na siasa za ushabiki uliojengeka katika misingi ya kiitikadi za siasa uchwara,kikabila na kiegoisim,Mtu anapoonyesha jitihada hatuna budi kumuunga mkono kama juhudi zake ni za heri kwa taifa letu.TUNAHITAJI VIONGOZI WAWANAOWEZA KUFANYA MAAMUZI JUU YA MATUMIZI YA RASILIMALI ZA TAIFA LETU KITUI AMBACHO BINAFSI NAONA ZITTO ANAWEZA KUSIMAMIA ,TUMPE NAFASI HATA YA KUKIONGOZA CHAMA MWAKANI ILI CHADEMA YA MABADILIKO ISIJE IKAPOTEA
 
Mimi nadhani ule uswahiba na ..... ndo unaochagiza haya mambo hata watu wengine hawamwamini tena ZZK, pamoja na kuacha kuteam up na Chama katika baadhi ya mambo...
 
ndugu yangu hutoi tu orodha ya majina. Kuna taratibu za kimikakati za kutoa majina hayo. Hili sio suala langu peke yangu, ni suala la kambi ya upinzani bungeni na ni suala la chadema. Mimi ni msemaji tu wa chama katika eneo hili. Nalifanyia kazi kwa niaba ya kambi na chama na tutatoa orodha bungeni. Hakuna haja ya haraka na kuanza kusema maneno yasiyo na maana dhidi yangu. Haisaidii. Inavunja moyo.

Hata orodha ya mafisadi (list of shame) tuliyotoa mwembeyanga mwaka 2007 september 15, hatukukurupuka na kutaja tu majina. Tuliifanyia kazi. Tulitangaza jangwani wakati wa mkutano wa buzwagi kwamba serikali isipochukua hatua tutawataja. Haikuwa tu katibu mkuu aliibuka na kuanza kutaja majina. Tuliifanyia kazi na tuli build up momentum kwa zaidi ya wiki 3.

Hili la orodha ya watanzania wenye akaunti za benki katika mabenki huko switzlerland nalo tutalifikisha mwisho na wala hatuna papara nalo. Tumefuata taratibu za kupata orodha hiyo. Huko tumekumbana na kigingi cha barua ya kutoka takukuru ambayo iliandikwa kwa serikali ya swistzerland kwamba orodha wapewe wao tu na baadhi ya maneno ambayo yameudhi mamlaka za huko.

Hii sio kazi rahisi. Badala ya kunibeza katika kazi hii inapaswa kutiana moyo. Kunibeza hakutasaidia kufanikisha moja ya jukumu muhimu kabisa katika vita dhidi ya ufisadi.

Kuna mtu kasema hapa nami nitaje nilizoficha ndani. Napenda kurudia kusema mimi sio tu sina mabilioni, hata mamilioni sina. Ninaishi kwa mshahara wa kazi yangu ya ubunge. Sina biashara na wala sitarajii kufanya biashara nikiwa mbunge. Ninaamini katika miiko ya uongozi, kwamba kiongozi wa umma atumikie umma. Mtu yeyote mwenye ushahidi wa biashara ya zitto aonyeshe hapa. Mtu yeyote mwenye chembe ya ushahidi wa mabilioni ya zitto aonyeshe hapa. Wakati mwingine hizi propaganda za kiasiasa zinafunga akili za watu. Sina utitiri wa magari. Nina gari 2 tu sasa, toyota vista ninayotembelea na landrover freelander ambayo hata sijamaliza kuilipia kodi. Nikiwa waziri kivuli wa fedha na uchumi nimekataa hata kuchukua tax exemption kwenye kuagiza gari kwani ninapinga tax exemptions. Mwenye ushahidi wa gari yeyote niliyonayo tofauti na hizo aweke hapa. Kwanini tuwe na porojo zisizokwisha na bila ushahidi?

Sina nyumba dar es salaam wala dodoma. Ninajenga nyumba kijijini kwangu kibingo,mwandiga kigoma. Dar es salaam napanga. Dodoma nakaa hotelini. Sina hata kiwanja dodoma, sijawahi kuomba kiwanja na wala sitegemei kufanya hivyo maana sina mpango wa kuishi dodoma wala dar es salaam. Nina shamba la korosho mtwara lenye mikorosho 400 na kiwanja eneo na mangamba. Nina shamba ekari 3.5 mbutu kigamboni.

Nina akaunti nmb na crdb tu. Mwenye ushahidi wa mimi kuwa na akaunti benki nyingine yeyote aweke hapa. Tuacheni porojo ndugu zangu. Niacheni nifanye kazi. Nikosoeni ninapokosea. Tushirikiane panapotakiwa. Sio kila siku kushambuliwa tu bila sababu. Wenzetu greece hii kazi ninayofanya inafanywa na magazeti ya kiuchunguzi.

Soma hii hapa uone wenzetu walichofanya.

kwa dhati ya moyo wangu nakupongeza kwa ujasiri ambao umekuwa ukiuonyesha mara zote na kwa hakika umekuwa muhimili muhimu sana kwa chama chetu , kwa hili nakupongeza saana kaka yangu zitto. Niseme hivi : Mimi ni mmoja kati ya walio wengi wanaokuamini kwa ufanisi,ustadi na uweledi mkubwa wa jinsi nchi yetu inavyoenenda ila kuna jambo moja tu nikushauri ili mimi na walio wengi ndani na nje ya jf tuendelee kukuamini na hivyo kuongeza mtaji wa kisiasa

zingatia:
Wakati wako wa kuwa rais wa nchi hii si sasa ( kwa mapenzi mema kabisa ) lakini ni haki yako ya kidemokrasia kuamua ama ugombee ama usigombee. Nakuomba muangalie katibu mkuu kwa sasa ana sifa nyingi zaidi yako ya kukiwakilisha chama na kwa mtizamo wangu wewe utatufaa zaidi ama 2020 ( na hii ikiwa mgombea wetu 2015 ambae naamini atakuwa dr. Slaa atashindwa ktk uchaguzi wa 2015 otherwise allah atujalie maisha marefu zaidi ili 2025 uwe kamanda wetu (hakika nitakuwa mpiganaji wako mahiri insha_allah km nitajaliwa uzima na allah).
Ushauri huu nautoa km moja ya fans wako ktk siasa na msomi mwenye maono chanya. Ukikosea ktk hili hakika utapotea ktk medali za kisiasa labda uwe na agenda ya siri nyuma ya mbio hizi kama wengi wanavyoamini. Chonde chonde dr. Slaa bado ni imara na makini kuliko wewe kwa sasa na naamini wewe ni lulu kwa chama chetu na usikubali kutumika ili isije tokea ukapoteza nafasi yako na ya vijana wengine km icon ktk jamii. Asante km utaisoma,kuilewa lkn kuifuata au kutoifuata ni uamuzi wako kaka yangu.
 
ZZK, kwanza nakupongeza sana kujitokeza mapema na kuweka mambo sawa!. Uwongo ukisemwa na kurudiwa rudiwa bila kukanushwa hatimaye huonekana ni ukweli!, hivyo umefanya vyema kuukanusha!.

Wengi wa washabiki wenu humu jf sio deep kihivyo kwenye issues, hivyo waliposikia Dr. Slaa alipotangaza ile list of shame pale Mwembeyanga, hawakujua its a result of a team work!, hivyo kukaa kwako kimya kuhusu harakati za M4C au kutoonekana onekana, kunatafsiriwa vibaya!, sisi tunaokufahamu, na Chadema wenyewe insiders, wanajua unafanya nini, big up for that, keep up the good job, hawa washabikii maandazi wa humu jf wasikukatishe tamaa wala kukukosesha usingizi!, jf doesn't matter ki hivyo on the ground, hivyo wewe endelea kipiga kazi yako na kutimiza ndoto yako na naamini itatimia!.

Naomba pia nikupe angalizo moja huko niliko bold, jf sio Tume ya Maadili ya Viongozi, hivyo huna haja ya ku disclose too much of your personal details, mfano ulipoeleza una magari mawili tuu hayo uliyoyataja!, nikikufuatilia tangu ulipokuwa mbunge mpaka sasa, umeshawahi kumiliki jumla ya magari mangapi, idadi itazidi 10!, hata kama ulimiliki ukaacha!. Kwa mtu makini kama wewe, ile kitendo tuu cha kumiliki gari fulani la kifahari kama ile Vogue, and then within a short period of time una li dispose!, leaves much to be desired!. Hivyo nakushauri, usiyaweke hadharani mambo yako binafsi, yatafungulia "pandora box" in future!. Hata kumiliki ekari 3.5 Mbutu, kwa market value ya sasa with New Kigamboni City on the pipeline, its not a joke!, hata kama ulifanya aquisition ages ago when that land was worthless!. Nakushauri wewe komaa tuu kuwa mengi yanayosemwa kuhusu wewe sii kweli and don't go into too much details!.
P.


Hapo kwenye red ndo inadhihirisha uelewa mdogo wako. kwani we unadhani hiyo tume ya maadili inafanya kwa niaba ya watu gani km si wananchi na kwa sababu ZZK anaamini yeye ni clean na shutuma dhidi yake zinatolewa humu JF kwa nini asiweke wazi . POOR wewe, Kaka ZZK washauri wengine sijui ndo wale wa Lusinde yule jamaa mlopokaji wa CCM? Anyway utanisaidia kujibu kabla ya vikao vya bunge mwisho wa mwezi huu
 
Ukweli husemwa:

Tatizo siyo watu tu kuwa na uelewa kidogo, Tatizo ni viongozi wa vyama ambao wengi wanataka kujijengea umaarufu wa kibinafsi kwa manufaa yao ya sasa na baadaye. Kwa maneno mengine, wanakuwa na udikteta wa sifa. Wanafanya mambo katika njia ambayo wanapenda wananchi wawaone kama ni maamuzi yao binafsi badala ya chama. Utawasikia majukwaani wanasema, ninataka hiki, ninataka kile badala ya kusema chama kinataka hiki au chama kinataka kile. Hii ni kansa ambayo imeachwa na viongozi waliotangulia ambao waliwaminisha watu kama wao ndiyo mwanzo na mwisho katika maamuzi na utendaji ndani ya chama na serikali.

ZZK kama nilivyosema katika post zangu za mbele, anawachangany'a wengi humu Jf kwa sababu watu wengi wamezoea siasa za mazoea. He's doing sophisticated politics in high level, unfortunate, few Tanzanian understand. ZZK big up, umekata mzizi wa fitina kwa wengi kwa kutaja kile ulichonacho pamoja na kuwa kuna bado wachache hawataamini uliyoyaandika kwa vile hii ndiyo demokrasia.

Hii ndiyo Tanzania ya leo, cha muhimu tu, fanya kama dhamira yako inavyokutuma kufanya.


ZZK, kwanza nakupongeza sana kujitokeza mapema na kuweka mambo sawa!. Uwongo ukisemwa na kurudiwa rudiwa bila kukanushwa hatimaye huonekana ni ukweli!, hivyo umefanya vyema kuukanusha!.

Wengi wa washabiki wenu humu jf sio deep kihivyo kwenye issues, hivyo waliposikia Dr. Slaa alipotangaza ile list of shame pale Mwembeyanga, hawakujua its a result of a team work!, hivyo kukaa kwako kimya kuhusu harakati za M4C au kutoonekana onekana, kunatafsiriwa vibaya!, sisi tunaokufahamu, na Chadema wenyewe insiders, wanajua unafanya nini, big up for that, keep up the good job, hawa washabikii maandazi wa humu jf wasikukatishe tamaa wala kukukosesha usingizi!, jf doesn't matter ki hivyo on the ground, hivyo wewe endelea kipiga kazi yako na kutimiza ndoto yako na naamini itatimia!.

Naomba pia nikupe angalizo moja huko niliko bold, jf sio Tume ya Maadili ya Viongozi, hivyo huna haja ya ku disclose too much of your personal details, mfano ulipoeleza una magari mawili tuu hayo uliyoyataja!, nikikufuatilia tangu ulipokuwa mbunge mpaka sasa, umeshawahi kumiliki jumla ya magari mangapi, idadi itazidi 10!, hata kama ulimiliki ukaacha!. Kwa mtu makini kama wewe, ile kitendo tuu cha kumiliki gari fulani la kifahari kama ile Vogue, and then within a short period of time una li dispose!, leaves much to be desired!. Hivyo nakushauri, usiyaweke hadharani mambo yako binafsi, yatafungulia "pandora box" in future!. Hata kumiliki ekari 3.5 Mbutu, kwa market value ya sasa with New Kigamboni City on the pipeline, its not a joke!, hata kama ulifanya aquisition ages ago when that land was worthless!. Nakushauri wewe komaa tuu kuwa mengi yanayosemwa kuhusu wewe sii kweli and don't go into too much details!.
P.
 
mungu nashukuru kwa kuwafungua watanzania macho now its time to open their minds to see the truth maana nchi inapotea
 
Ndugu yangu hutoi tu orodha ya majina. Kuna taratibu za kimikakati za kutoa majina hayo. Hili sio suala langu peke yangu, ni suala la kambi ya upinzani Bungeni na ni suala la CHADEMA. Mimi ni msemaji tu wa chama katika eneo hili. Nalifanyia kazi kwa niaba ya Kambi na chama na tutatoa orodha Bungeni. Hakuna haja ya haraka na kuanza kusema maneno yasiyo na maana dhidi yangu. Haisaidii. Inavunja moyo....

Soma hii hapa uone wenzetu walichofanya.

Mh. Zitto, yote nakubaliana nayo na kukupongeza, ila umesema unapinga exemption...unamaanisha ifutwe kwa watu wote au kwa baadhi ya makampu na watu. Please naomba mchanganuo.

Ishu ni kwamba, mimi ni mjasiriamali mdogo sana, sikuwa naelewa ishu ya exemption hadi niliposhirikiana na wenzangu katika kuanzisha biashara ya fulani, tukakwama along, exemption ilituokoa na tukaweza kuagiza vitu na kuanza biashara.
 
WAKATI serikali ikishindwa kuwataja vigogo walioficha mabilioni ya fedha nchini Uswisi, Mbunge wa Kigoma Kaskazini (CHADEMA), Zitto Kabwe, anatarajia kuwasilisha hoja binafsi katika mkutano wa tisa unaotarajiwa kuanza wiki ijayo mjini Dodoma, kutaka serikali irejeshe fedha hizo.

Zitto ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA, amesema tayari hoja hiyo imeshapata baraka za Spika wa Bunge, Anne Makinda. Mbunge huyo wa CHADEMA alisema hayo jana wakati wa akifunga mkutano wa kampeni za uchaguzi mdogo wa udiwani wa Kata ya Nanjarareha, wilayani Rombo, mkoani Kilimanjaro. Katika uchaguzi huo unaotarajiwa kufanyika leo, CHADEMA imemsimamisha, Frank Salakana.

Alisema sh bilioni 349 zilizofichwa Uswisi na baadhi ya vigogo wa serikali ya Chama cha Mapinduzi (CCM), lazima zirejeshwe nchini, huku akimtaka Mkurugenzi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Edward Hosea, kueleza umma barua aliyoituma nchini humo kwa ajili ya kashfa hiyo ilikuwa na lengo gani.

Alisema barua ya Dk. Hosea imesababisha ugumu wa upatikanaji wa taarifa za mabenki ya nchini Uswisi ambayo yameshindwa kutoa ushirikiano kwa kamati inayofuatilia kashfa hiyo.

Huku akishangiliwa na maelfu ya wanachama wa CHADEMA waliofurika kusikiliza mkutano huo, Zitto alisema wizi wa mabilioni hayo umetokana na kuporomoka kwa maadili ya viongozi nchini ambao wengi wanajali zaidi masilahi binafsi badala ya umma.

Mbunge huyo machachari wa CHADEMA, alisema kuna haja kama taifa kurejesha maadili ya uongozi kama enzi za utawala wa Mwalimu Nyerere ili viongozi wachague kitu kimoja, kati ya biashara na siasa.

Alisema CHADEMA imepania kuhakikisha mabilioni hayo yanarejeshwa ili yaweze kutumika kuwasaidia Watanzania katika kujenga na kuboresha miundombinu ya barabara, maji na afya.

Aliwataka viongozi walioficha mabilioni hayo kujitokeza mapema na kueleza jinsi walivyozipata badala ya kusubiri kuumbuliwa.

“Nawataka viongozi waliohusika wajitokeze wenyewe, waeleze walivyozipata na kisha wazirejeshe nchini, vinginevyo patachimbika, kwani nitahakikisha kama chama tunashirikiana na Benki ya Dunia kuhakikisha fedha hizo zinarudi nchini,” alisema Zitto.

Alisema CHADEMA inapigania fedha hizo zirejeshwe kwani zimetokana na wizi wa rasilimali za Watanzania kupitia mikataba mibovu ya mafuta na wizi wa madini na nyingine.

Katika ripoti ya Swiss Central Bank, iliyotolewa hivi karibuni, inaonesha kuwa Tanzania ni miongoni mwa nchi 11 barani Afrika ambazo vigogo wake wa kibiashara, kitawala na kisiasa wameficha kwa siri mabilioni ya fedha katika mabenki ya Uswisi.

Nchini nyingine za Afrika zilizoficha fedha hizo ni Kenya, Uganda, Zimbabwe, Misri, Shelisheli, Afrika Kusini, Rwanda, Sierra Leone, Somalia na Sudan. Kwa upande wa Tanzania, mapesa ambayo yamefichwa huko ni dola milioni 196.87, sawa na shilingi za Tanzania bilioni 315.5!

Hebu jiulize; mapesa haya tuliyoibiwa yangetusaidia kiasi gani kama yangerejeshwa nchini na kutumbukizwa kwenye miradi ya kuboresha huduma za jamii? Pia jiulize swali jingine: Je, hata baada ya Benki Kuu ya Uswisi kuturahisishia mambo kwa kututobolea ukweli kwamba tumeibiwa, na kwamba wezi wetu wameficha hizo fedha nchini mwao, watawala wetu wana dhamira ya kuanzisha mchakato ili wahusika wafikishwe mahakamani na fedha hizo zirejeshwe nchini?

Source: Tanzania Daima Jumapili

Hapa inaonekana kama kiini macho. Kwanza hakuna sheria yoyote inayomkataza mtu kuweka fedha zake katika mabenki ya nje. Pili, hakuna ushaidi uliokwishatolewa wa mhusika yeyote ambaye alipata fedha kwa njia zisizo halali na akazipeleka Uswizi. Sasa hii hadithi ya Mhe. ni nii maana yake kama siyo kutafuta umaarufu wa kisiasa. Ingefaa katumia muda wake vizuri kuliko kutuboa.
 
Maelezo yako yanatia moyo kidogo, ila usiogope kukosolewa na pia ujitaidi kuzingatia ushauri wa wadau mbalimbali wakiwemo viongozi wenzio chamani, kuna jambo naliona ili linanitia shaka kidogo, unaonyesha kama unafanya kazi kivyako vile, hii aipendezi umoja ni nguvu, ningependa nikupe ushauri wangu japo kwa kifupi tu, kipindi iki ningependa nione unapiga kazi ikiwemo hiyo ya kufanikisha kurudi kwa pesa zetu, na kuwaweka kweupe wote waliokwiba na wanaowakingia kifua maana tunaona kuna watu wana haha kufanikisha swala hili lipite kama yalivyopita mengine, na kingine ningependa kwa kipindi iki ujiweke mbali kidogo na swala la uraisi, japo ni haki yako ila tambua uko kwenye nchi gani na watambue uelewa wa watu wa nchi yako, watanzania walio wengi wanayumba ni wepesi wa kutafasri tofauti na lengo, yaani wanaweza kubadilisha nyekundu ikawa njano, na chakumalizia jiweke mbali kidogo na magamba, japo siasa sio uhasama ila sio kwa nchi hii. Ni hayo tu.
 
Thanks zitto,ume ni impress,ni maneno ya busara sana,nadhani naanza kukupenda.Keep it up.
 
Ndugu yangu Zitto unachoshambuliwa hapa sio wewe ni dini yako uliyonayo na huo ndo ukweli hata utende mema mangapi pro chadema wamejaa udini sana.Ona wanavyotukana dini ya kislamu wanaisifia serikali pale inapowadhibu waislamu utafikiri imekuwa ya chadema.

Mawazo ya mtu kama huyu ni hatari kweli kwa amani ya Tanzania. Infact wakristo hatuna muda wa kubagua watu kwa dini zao vinginevyo tusingekuwa na rais mwislamu, makamu wa rais mwislamu na mkuu wa polisi mwislamu. Ingekuwa vise versa sijuwi kama waislamu mngekaa kimya. Mwache Zitto achape kazi wala usimnyweshe hizo sumu zako. Wanaompinga wana hoja zao na wanaomuunga mkono wana hoja zao.
 
Waarabu tuna Usemi " NI VIZURI WATU KUHISHIMIANA NA SI KUVUMILINA".

Kwani siku zote kuvumiliana kunazaa kuleana na kubebana. Lakin kuhishimiana kunajenga nidhamu ya hali ya juu na kufuata sharia.

Hamtaweza kufanya jambo lolote la maendeleo kama mtaendeleza Sera za kuvumiliana.

Poleni sana
 
Hapa inaonekana kama kiini macho. Kwanza hakuna sheria yoyote inayomkataza mtu kuweka fedha zake katika mabenki ya nje. Pili, hakuna ushaidi uliokwishatolewa wa mhusika yeyote ambaye alipata fedha kwa njia zisizo halali na akazipeleka Uswizi. Sasa hii hadithi ya Mhe. ni nii maana yake kama siyo kutafuta umaarufu wa kisiasa. Ingefaa katumia muda wake vizuri kuliko kutuboa.

Inawezekana kabisa na wewe ni mnufaika wa huo wizi. Si bure haya maneno yako.
 
Back
Top Bottom