MPIGA ZEZE
JF-Expert Member
- May 16, 2011
- 2,539
- 2,296
Kwahiyo anafanyia yake Facebook?
Haya tufanye anatetea maslahi ya wananchi, na wasakatonge wanagawana vyeo, si ndio angewaacha wasinzie ili yeye apate crédit mwenyewe kwa juhudi zake ili mwisho wa siku actions zake ziwe louder kuliko maneno ya Facebook au ya wasaka tonge? Au anataka wamsaidie baada ya kugundua kelele zake pekee kama za matrilion ya Uswis hazina mashiko.
Namuhurumia sana dogo.
Zitto anasumbuliwa na ugonjwa wa 'egocentrism' (mimi, mimi, mimi mimi ndio mwanzo ndio mwisho!!). Sifa zote za mapambano dhidi ya ufisadi ni zangu na sio zetu! Mfumo wa utawala wa sasa na ambao umehifadhiwa katika katiba inayopendekezwa ndio MUUNDOMBINU MKUU wa UFISADI ambao ndio unaosababisha haya yote ambayo Zitto anadai kupigania (kama kweli anafanya hivyo kwa dhati na si kwa chati. Lakini tu-assume anayapigania kwa dhati). UKAWA walichokifanya kuanzia kususia mchakato chakachuzi wa katiba mpya hadi leo kuamua kuunganisha nguvu dhidi ya CCM lengo ni kuvunjilia mbali ama kufumua huu MUUNDOMBINU FASIDI na kujeanga MUUNDOMBINU mpya unaojali ustawi wa jamii kwa jumla. Kubeza juhudi za UKAWA ni ama kuonesha welewa mdogo ama kudhihirisha kuwa hata hicho anachodai anakipigania ni kwa chati tu. UKAWA wanafanya jitihada za kung'oa mizizi, yeye anajidai kupukutisha majani alimradi watu wote wamsifie yeye tu! Akawanadanganye akina Mtela na Juliana (wasomi wa UDSM wanaosumbuliwa na njaa za mjini)- maana nikisema akawadanganye wakulima na wavuvi Kigoma nitakuwa nawaonea. Nao pia wameishatambua haki zao na utapeli wa 'egotist' kama yeye.
UKAWA
TUMAINI LETU!