Ulukolokwitanga
JF-Expert Member
- Sep 18, 2010
- 8,396
- 7,968
Zitto Kabwe, mgombea udiwani kata ya Mwandiga kupitia ACT 2015
Kwahiyo anafanyia yake Facebook?
Haya tufanye anatetea maslahi ya wananchi, na wasakatonge wanagawana vyeo, si ndio angewaacha wasinzie ili yeye apate crédit mwenyewe kwa juhudi zake ili mwisho wa siku actions zake ziwe louder kuliko maneno ya Facebook au ya wasaka tonge? Au anataka wamsaidie baada ya kugundua kelele zake pekee kama za matrilion ya Uswis hazina mashiko.
Namuhurumia sana dogo.
Mtoa mada, hii ni nchi huru, Katiba inamruhusu mtu huyu kuexpress mawazo yake. Sio mpaka uongee ili kila mtu akupende, binadamu unapaswa kuwa huru kimawazo. Ukiongea kwasababu unaogopa utaonwa tofauti, huo ni utumwa.
Let him...
Kufuatia Mh zitto kuwakebehi wanaukawa kuwa ni wasaka tonge, Julius mtatiro amemjia juu na kumuambia kuwa ameteleza. Hivi ndivyo ilivyokuwa.
MTATIRO
ZITTO AMETELEZA!
Hii habari ya Zitto kuwaita viongozi wa UKAWA kuwa ni "‪#‎wasakatonge‬" ni ya Ukweli ? is it the real Zitto Kabwe au imetumika ile akaunti feki ambayo wajanja huitumia kujidai wanatoa mikopo ya kitapeli kwa jina lake?
Kama ni yeye kweli na ni akaunti yake "it means, there is something wrong somewhere" (Kuna tatizo mahali). Nimjuavyo Zitto mara nyingi masuala ambayo anaona hayafahamu vizuri walau hukaa kimya.
Mtizamo wangu ni kuwa walau kwa sasa ‪#‎UKAWA‬ ina maana kubwa kwa watanzania na yeyote(hasa mpinzani) ambaye ataidharau anaweza kudharaulika mara mia moja. Ushirikiano wa UKAWA unaitikisa CCM na lazima utapunguza kasi ya ushindi wa CCM katika maeneo yote ya nchi, na hicho ndicho wananchi wanataka. Natabiri kuwa, chama chochote cha siasa kisicho CCM kitakachojitokeza hadharani kupambana na nguvu hi i‪#‎kitaaibishwa‬ vibaya.
‪#‎KUSHINDANA‬ ‪#‎NA‬ #UKAWA ‪#‎NI‬ #KUSHINDANA #NA ‪#‎MIOYO‬ ‪#‎YA‬‪#‎WATANZANIA‬ ‪#‎WALIOICHOKA‬ ‪#‎CCM‬.
Standup brother ‪#‎Zitto‬ ‪#‎Kabwe‬, kuteleza si kuanguka.
ZITTO
Julius Mtatiro niache nifanye yangu. Nina kazi ya kufanya kusimamia Mali za Watanzania. Wengine nao wana kazi yao ya kugawana vyeo. Kwangu Mimi kwa sasa muhimu ni kuokoa Fedha za Wafanyakazi kwenye mifuko ya Hifadhi ya Jamii, kuokoa Wakulima ambao Mahindi yao hayana soko, kuokoa NBC na kuhakikisha wezi wa escrow wanakamatwa.
Tugawane majukumu tu - wengine wagawane vyeo wengine waiwajibishe Serikali
MTATIRO
Zitto Kabwe hakika hakuna shaka juu ya mchango wako kwa mabadiliko katika nchi yetu, kusimamia rasilimali za umma zitumike kuwanufaisha wananchi na kupambana dhidi ya wizi na ubadhirifu...from#Buzwagi to madudu kibao tu uliyoyasimamia.
Unajua mjadala huu wa sasa umekuja kwa sababu #undelea uliacha #hayo #unayoyaita #yako, ukaja kutoa mawazo yako kuhusu #UKAWA. Na sie wengine pia tunatoa mawazo yetu juu ya UKAWA lakini kwa kutofautiana na wewe kidogo tu, najua ni mitizamo na mwisho wa siku kila mtu anaendelea kusimamia anachokiamini.
Kwa hakika ambacho haupaswi kusahau ni kuwa hayo unayoyapigania leo, uwajibikaji, kuhakikisha wananchi wanauza mahindi katika soko la uhakika na bila vikwazo, ufisadi n.k. ni masuala ambayo yamepiganiwa na watu wengi tangu zamani mno na wapo watakaopigana baada yako na wapo wanaopigana hivi sasa kama wewe. Kujaribu kuonesha umma kuwa kuna viongozi wanagawna vyeo mahali siyo jambo sahihi hata kidogo.
Natambua wewe ni mpinzani imara, lakini siku za usoni hautakwepa dhana ya upinzani kufanya kazi pamoja, na ndiyo hii ambayo imeanza sasa. Badala ya kutumia nguvu kubwa kujaribu kuonesha kuwa kinachofanywa na UKAWA ni kugawana vyeo ni bora utumie muda huo kupambana na yale uyaitayo "yako" na kuyaacha haya mengine wenye nayo wayafanyie kazi.
Jambo la pili ni kuwa, ukianza kuwashambulia viongozi wa vyama vya upinzani kwa ujumla namna hiyo na kuwaita #WASAKA#TONGE na #WAGAWANA #VYEO huku wao wakiwa wamekukalia kimya nadhani wanaweza pia kukujibu, na kwa sasa wao ni wengi na wewe ni mmoja, kwa vyovyote vile nyote mtasikika lakini wao watasikika zaidi.
Kwa maoni yangu, huu ni muda wa kukaa kimya na kutizama na kutoongeza malumbano dhidi yako na vyama vya upinzani kwa ujumla. Maana ukiniambia #Maalim#Seif ni msaka tonge sikuelewi, ukiniambia #Lipumba ni msaka tonge sikuelewi, maana nimefanya nao kazi kwa karibu sana.
Hadi leo Maalim Seif ndo anajenga nyumba yake, Lipumba hana hata duka. Pamoja na mapungufu ya kibinadamu ya kila mmoja wetu lakini they dont deserve to be called #WASAKA #TONGE .....I strongly advice you either to keep quite on UKAWA...or JOIN THE TEAM......Sisi wakristo tunafundishwa kuwa "HAKUNA VUGUVUGU, KUNA MOTO NA BARIDI" .
Hivi yale mabilioni ya uswizi yaliishia wapi?
Anataka UKAWA wakanunue mahindi.....
Amesahau JK kapewa uprofesa na chuo cha Kilimo.
Copied Kutoka kwenye ukurasa wake wa INSTAGRAM;
"Taifa limevimba. Wakulima Mahindi yanawaozea na Mpunga bei imeporomoka sababu ya mchele kutoka nje na usiolipiwa Kodi. Wahisani wamezuia misaada ( sababu ya kashfa ya #TegetaEscrow ) Kiasi Serikali haiwezi hata kujiendesha. Unapoona wanasiasa wanagawana vyeo katika nyakati kama hizi ujue Taifa halina Viongozi bali wasaka utawala. Wasaka utawala badala ya uongozi ni #WasakaTonge tu"
My Take;
Jamaa ameamua kuwa mpinzani ndani ya upinzani..Kina kinana na nape hawaoni?!!!
Zitto ana akili kuliko viongozi wote wa UKAWA!
Ameongea Ukweli mtupu!