Zitto awasilisha hoja binafsi juu ya walioficha fedha Uswiss

mwambie huyo mshikaji wa jk hata akifuta hapa jf tutasema majumbani kwetu na wake zetu na dada zetu nao watawaambia watu wao wa karibu kuwa wafuatao wana pesa akaunt za nje na hasa uswisi
1- edo luwasa
2- mazengo pindu
3- ben mnkapa
4- riz1
5- fred luwasa
6-jenge john
7-
8-
9----
acheni uoga endelezeni list...naandaa majina ya benki walikoweka mzigo

jamii forum we dare to talk openly
karamaji
 
Ana hoja nzuri, ila tatizo sijui kama ana nia ya dhati, maana kwa sasa simwamini sana huy jamaa
 
Basi tu kwa kuwa watu wenyewe wana sura 'ngumu', vinginevyo mashinikizo yataanza kushika kasi...

Hofu yangu ni moja tu, kweli litafika mwisho?
 
Mie nilishasema inapokuja uandaaji wa Taarifa za kiuchunguzi na kitafiti ndani ya cahdema hakuna wajenga hoja zaidi ya ZZK , TUNDU na Mnyika kwa kiasi fulani, uwasilishaji alioufanya ZZK umemsaidia sana kukwepa vigingi vya kisheria na kanuni za Bunge ambavyo baadae vingemrudi au Hotuba yake isingesomwa kabisa.

Na kwa taarifa yako huo mchezo wa kucheza na vizingiti vya kikanuni umeratibiwa na Tundu Lissu. Na ndo maana aliporudishwa kwenye kiti chake ili amalizie kusoma, Lissu alimtonya kuwa aendelee kusoma amalizie ili yaingie kwenye records. Angekuwepo Makinda mtego huu angeubaini mapema, na asingeruhusu.
 
Nimependa namna alivyowasilisha hoja hii. Ni wabunge wachache (kama wapo) wataweza kuiwasilisha hoja hii hivi. I may be wrong. Si sahihi zigo hili kuachiwa Zitto, serikali kama imedhamiria kukomesha ufisadi, basi impe ushirikiano. Upinzani (si lazima CHADEMA pekee) ushirikiane kuhakikisha hili linafanyiwa kazi haraka

Mkuu Invisible, kwa hii kasumba ya "huu ni upepo utapita" nadhani serikali hii sikivu, itasikiliza tu na yatapita. Kwani mpaka sasa tumeona mengi ya ushahidi wa wazi wa akina Chenge lakini serikali ni sikivu tu, inasikiliza na yanapita.
 
Zitto, ni mtu muhimu sana kwenye mustakabali wa taifa letu ana dhamira ya dhati ya kupambana na ufisadi.
 
Last edited by a moderator:
Zitto Kabwe anawasilisha mswaada binafsi kuhusiana na mabilioni yaliyofichwa benk ya uswiss yarejeshwe!
Hii mutu ya kigoma hatarieee? Shida ni magamba wao hata mwenzao akitembea uchi wanaweza wakabisha mno wakisema amevaa nguo. Wasije tu wakmwagia polonium
 
Hongera sana Zitto, kwanini?
  • Umeweza kujua muda muafaka wa kuleta hoja ya uchunguzi wa mabilioni yaliyoibiwa hapa nchini, kwasababu baada ya uchaguzi ndani ya CCM wengi wana hasira za kutokuwa na pesa wakati wa uchaguzi hivyo tunaweza kunaufaika (sisi kama taifa) na hizo hasira na kuweza kunasa hao mafisadi.
  • Kutokata tamaa ya kuwasilisha hoja hii ya mafisadi nchini, manake leo nimeona makofi na wabunge waCCM wakati majina ya wamiliki wa Meremeta wakitajwa utadhani ndo mara yao ya kwanza kuyasikia bungeni
  • Kutuonyesha unafiki wa akina Membe, Sendeka na wengine manake leo wanajidai kushabikia hii hoja wakati siku zote ilikuwa ikiletwa wanaungana kuiminya!
For the Record:
Naendelea kuwa kumbusha ndungu zangu waTz kuwa "Hakuna mbunge wa CCM anayechukia mafisadi kwa maslahi ya nchi yetu". Ukimuona mbunge wa CCM anaongea kwa kuonyesha chuki yake dhidi ya ufisadi ujue katika haya moja limetokea:-


  1. Kakosa mgao katika hilo deal
  2. Anayenufaika na huo mgao ni mshindani wake kisiasa
Hii ya namba mbili ndiyo inawasukuma wabunge waliochangia leo!. Kama wasemavyo wahenga "Vita ya panzi ni furaha ya kunguru" ndivyo sisi watanzania tunakavyonufaika na mbio zao za kuelekea 2015.
 
kama na bunge nalo linaogopa kutaja lina maana gani au huu mpira nia wa kurusha au wa kupiga?
 
ZITTO AMEFANYA KAZI YAKE ATAKUMBUKWA WAKATI WOTE WA MAISHA YAKE AKIWA MBUNGE HAKIKA AMETIMIZA WAJIBU WAKE NI WABUNGE WALEWALE WATAMBEZA LAKINI KUSUDI NI MOJA KUIKOMBOA NCHI HII NIWAOMBE WANAJAMII WEZANGU TUFIKILI NI NAMNA GANI TUNAWEZA SASA KUTUMIA NAFASI ZETU KAMA RAIA WEMA KUIWAJIBISHA SERIKALI KAMA BUNGE LITASHINDWA NAAMINI LITASHINDWA SI MARA YA KWANZA

  • A%20S%20angry.gif

 
WanaJamvi leo nimerudi tena baada ya kupotea kwa muda mrefu

Leo nimesikiliza bunge kwa makini nimeshangazwa na Mh membe kufurahi sana
alipoambiwa aonyeshe uwezo wake wa kuongoza kama atapewa furusa hii ya kuwataja majina
maana siku moja alishawai kuwataja.

Sijapenda kitendo cha membe kufurahi kwa kutingisha kichwa na kuinama kwa HESHIMA ya kukubaliana
aliyokuwa anayaongea mbunge wa Ruvuma(kama sijakosea). Hii inaleta picha mbaya kuwa aliyeandaa hoja hii
na kupewa ZItto ni membe. EBU SOMA KWA UNDANI MANENO ALIYOYASEMA ZITTO ALIKUWA ANAMLENGA NANI?


" kuchunguza kwa kina mali za Watanzania wote waliowahi kushika nafasi za Uwaziri Mkuu kati ya mwaka 2003 mpaka 2010, waliowahi kushika nafasi za Uwaziri wa Nishati na Madini, Uwaziri wa Ulinzi, Ukuu wa Majeshi, Ukatibu Mkuu wa wizara ya Nishati na Madini, Ukatibu Mkuu wa Wizara ya Ulinzi, Uanesheria Mkuu wa Serikali, Ukamishna wa Nishati, Ukurugenzi Mkuu wa TPDC, Uenyekiti na Ujumbe wa Bodi wa TPDC katika ya mwaka 2003 mpaka 2010"


MWISHO: HII HOJA HAITOFIKA POPOTE MAANA IMEINGILIWA NA MAMBO YA URAIS WA 2015
NIKO TAYARI KUPIGWA
LIFE BAN KAMA HII HOJA ITALETA MWANGAZA KUEMIRI UFISADI
 
Back
Top Bottom