Zitto amtaka Waziri Mkullo apishe uchunguzi - Taarifa kwa vyombo vya habari

He Mh. Nkulo onyesha uungwana uachie ngazi ili uchunguzi ufanyike. Hii itakuongezea heshima angalau kidogo
 
Kama ameshindwa kumfukuza Ngeleja ataweza kwa Mkullo hivyo JK anapaswa yeye mwenyewe kupigiwa kura ya kutokuwa na imani naye kwa kuwa vitu vyote anavijua vizuri sana kuhusu madudu yote na mambo yote haya yapo chini yake na Hongera sana Zitto
 
Hayo ndiyo mambo sasa, Mhs Zito alitakiwa kufanya hivyo siku nyingi kufunua uozo wa hii serikli na mawaziri wake ili watu wapate ukweli wa hii serikali dhalimu!

Hilo pia la waziri wa fedha liwekwe kwenye kampeini ya maandamano. Ukombozi TZ ni muhimu!
 
Masikitiko makubwa kwa watanzania ni kwamba pamoja na uozo wote anaofanya mkulo, raisi Kikwete atanyamaza as if hajui wala hakusikia kinachoendelea kati ya CHC na waziri mkulo. Atanyamaza kimya na mkulo ataendelea na nafasi yake ya uwaziri na hatimaye ataharibu ushahidi na kujinasua na kadhia hii.

Hapa ndipo huwa tunatamani rais Kikwete atumie mamlaka yake japo kidogo tu, kuonyesha wananchi kwamba yuko kwa maslahi yao, lakini wapi bwana hili nalo litapita hivi hivi!
Si chama CHADEMA kitishe maandamano ili huyu Bwn JK ASIFIKIRI AKINYAMAZA WATU WATANYAMAZIA HUO UOZO!

CHADEMA chukua hizo initiative ni loose ball kazi ni kufunga magoli tuu!
 
Mkulo kalikoroga kitendo cha kuvunja bodi kinyemela kinadhihirisha kuna jambo limejificha nyuma yake. Ningelikuwa JK hiyo ni sababu tosha ya kumtaarifa mkulo aachie ngazi kwani tayari ameshajitia kitanzini. Inanikumbusha hadithi ya mama Meghji na barua ya Balali!!!Kazi nzuri Zitto wacha tuangalie JK atafanya nini!

Mkulo anashabihiana dini na mkubwa wa nji hii na ni marafiki pia, haendi kokote tuko naye mpaka 2015.
 
Zitto kawatega tena! Anataka PCCB wafanye uchunguzi, akili yangu haikubali kama kweli Dk Hosea na PCCB wanaweza kuichunguza na kutoa taarifa ya kumuunga mkono Zitto, never! Na Zitto analijua hilo na hapo ndipo anapowatega.
 
Kazi nzuri mh.Zitto

Huyu mkulo tangu amekuwa waziri wa fedha tumeshuhudia hali ngumu sana ya maisha. Bei ya bidhaa inapanda kila kukicha, mishahara ya wafanyakazi wa serikali inachelewa isivyo kawaida na kubwa kuliko vyote miradi mingi ya maendeleo kama si yote imesimama kama si kufa kabisa kwa kukosa fedha.

Kuna taarifa kwamba pamoja na kwamba bajeti ya serikali imepitishwa tangu mwezi wa sita, takriban miezi minne sasa bado taasisi na idara za serikali hazijapokea mafungu yao, hivyo kusababisha shughuli nyingi za kimaendeleo kukwama. Mkulo asipotimuliwa wizara ya fedha tujue tunapalilia janga la kitaifa.

Ndg yangu Mwita Maranya fedha za kodi za serikali hazikusanywi labda za chunvi mafuta na viberiti (TRA)! Kodi za Dhahabu, Tanzanite na makampuni makubwa wanasamehewa kodi!

Serikali itaendeshwa vipi bila ya fedha za kodi? Mkulo bomu yupo kufilisi nchi!
 
Ritz, Faiza Foxy, Mbopo, Mwita25 & GAMA Ongezeni wengine hapa wakishatimia tuanze mjadala Wakimbizi wanaotutesa.

1. Mustapha Mkullo
2. Joseph Mungai
3. Rostam Aziz
4. Daud Balali
5. Jeetu Patel
6. Abdul Kinana
 
hapo ni kumyoa mkulo tu maana kila kitu wao Chadema ni waongo sasa tuone kama kweli kikwete anakibuli basi hii ndio jeuri ya kasi mpya nguvu mya ya kuwafilisi watanzania
 
Wakimbizi wanaotutesa.
1. Mustapha mkullo
2. Joseph mungai
3. Rostam aziz
4. Daud balali
5. Jeetu patel
6.kINANA
7. Idd Simba
8
9
 
masikitiko makubwa kwa watanzania ni kwamba pamoja na uozo wote anaofanya mkulo, raisi kikwete atanyamaza as if hajui wala hakusikia kinachoendelea kati ya chc na waziri mkulo. Atanyamaza kimya na mkulo ataendelea na nafasi yake ya uwaziri na hatimaye ataharibu ushahidi na kujinasua na kadhia hii.

Hapa ndipo huwa tunatamani rais kikwete atumie mamlaka yake japo kidogo tu, kuonyesha wananchi kwamba yuko kwa maslahi yao, lakini wapi bwana hili nalo litapita hivi hivi!
Hapa tatizo ni moja madudu na ufisadi aliyonayo rais jk kikwete na viongozi wengi wa ccm na serikali ni makubwa zaidi wataendelea kulindana mpaka nguvu ya umma itakapowakurupusha kutoka madarakani.Mungu ibariki tanzania!
 
Mimi ni Mtanzania wa kuzaliwa, hivyo ni mwananchi mwenye uchungu na nchi yangu. kila mmoja wetu analalamika kuwa mambo ya
ya uendeshaji wa serikali hayaendisawa na hasa tangu Jakaya ashike Madaraka. In fact, Juzi Jakaya kawaita watendaji wake na mawaziri,
akiwapo Mkulo. Analalamika kuhusu umeme.

Sasa ona madudu anayanya mteule wake, Waziri wa Fedha, bwana Mkulo halafu Jakaya anategemea nini?? Ufanisi wa serikali yake upande wa fedha?

Na hii ni sehemu moja ya serilkali lakini ni uoza mtupu. Watu wajinga utasikia wanasema, watendaji hawamsaidie Rais na ndio wanaomungusha katika serikali yake. Wanaosema hivi hawajui yeye Jakaya ndo anawateua hawa wastaaafu ambao rushwa kwao ndo msingi wa maendeleo yao binafsi. Mustafu Mkulo ni Mstaafu kwa umri. kazi ndo anaharibu ile mbaya lakini kwa Jakaya kama amelishwa dawa hawa ndo wateule wake. na ninauhakika hata mfanye Jakaya atazama na hawa wakina Mkulo.

Angalia wakuu wa mikoa aliowateua juzi, wote ni waastafu; Luteni kanali mstaafu Issa Machibya, Kanali Mstaafu Fabiani Masawe, Kanali mstaafu Joseph Simbakalia, mstaafu Ludovick Mwananzila, mstaafu Mwantumu Mahiza, Mstaafu Joel Bendera na Injinia mstaafu Stella Manyanya. tunasubiri serikali itwe rasmi serikali ya waastafu.

Aibu
 
Mwandishi ajifunze kuweka 'space' kati ya neno na neno. Otherwise, Mhe. Zitto endeleza mpaka kieleweke
 
Kumekuwepo na lengo zuri la kuwakamata njiwa walioko kiotani. Tatizo linakuja kwenye mbinu, maana mara nyingi kama siyo zote imekuwa kamata huyoooo na bahati mbaya/nzuri wanatimua. Kama siyo blaa blaa, basi kazi iliyoko mbele ni kubwa pasi na shakaaaaaa . .:focus:
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom