Zitto aliwezaje kusoma vitabu 48 na hapo hapo kukesha twitter?

Huu uzi umenifungua mengi. Nimejifunza mambo yafuatayo:

1. Tuna kundi kubwa la watu wavivu wameshikilia ofisi kubwa. Hawasomi, hawana critical thinking skills na wanaamua by instincts.

2. Taifa letu nimeanza kujaa kizazi cha watu wasiokuwa na maarifa. Watu wasiosoma maandiko mapya na reports mpya hujikita zaidi kwenye historia.

3. Watu wengi wapo nyuma ya wakati. Karne hii mtu anashangaa kusikia kuna mtu kasoma vitabu 48. Ni jambo la aibu sana.

4. Kama watu wa elimu wanaweza ni vema wajikite kusisitiza na kupanda tabia ya usomaji miongoni mwa wanafunzi.
Kwanini tusome wakati kazi yetu ni kusifu na kusema ndiyoooooooooo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa hili kama linaleta mjadala nadhani watanzania wenzangu hususan vijana tunaanza kukosa maarifa ya msingi, kusoma vitabu ni hobby kama walivyo walevi wa pombe na ngono, kuna anayekunywa bia mbili na mwingine pampula.
Kuna wasomaji wazuri tu wa vitabu na wanajulikana huwa wanasoma mpaka zaidi ya vitabu 50.
Kitila Mkumbo na Jaunuary Makamba wanasoma vitabu vingi sana kwa mwaka kwani ndio ulevi wao, mimi mwaka 2018 nimesoma 37 tu.
Na kuna watu mpaka wana group za kushea mafanikio yao ya kusoma vitabu. Hivyo acheni kila mtu afanye addiction yake na maisha yaendele kwani mwisho wa siku unapata maarifa mapya na exposure. Hii siyo siasa ni kusoma vitabu na kupata maarifa
 
Narudia tena, acha utoto kusoma na kukumbuka ni mambo mawili tofauti. Ww vitabu ulivyosoma ukiwa shule hukuelewa? Je bado unavikumbuka vyote hata kama ulivielewa? Ndio maana unakimbiza mwenge kwa kuamini utaleta maendeleo.
Umeongea point moja inayonisikitisha sana.Hivi kwanini tunapoteza hela nyingi kwenye Mwenge? Mwenge una Siri gani,wameweza kuzuia sherehe nyingi ikiwepo ya Uhuru Ila Mwenge imekuwa nongwa.Mwenge una nini?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Dogo,ripoti za kazini ni tofauti na vitabu

Unashindwa kusoma kitabu cha page 250 utaweza kusoma economic outlooks za IMF, AfDB na World Bank? Competitive reports, Development Plans etc. Hizi zote ni thick kama kitabu.

Nawajua staff uchwara huko serikalini wanaosoma dodoso page moja au moja then wanasema wamesoma ripoti. Watu wa aina hii hawawezi kulivusha taifa mbele.

Na nashangaa unamshangaa Zitto, mimi pekee mwaka huu nimesoma vitabu zaidi ya 30.

Mwisho: uwe na adabu, mpuuzi kama wewe huwezi kuniita dogo. Unamuitaje dogo mtu usiyemjua?
 
Kwa Mtanzania kusoma ni adhabu. Anapotokea Mtanzani mmoja akawaambia yeye anasoma vitabu mia kwa mwaka anaonekana mwongo. Jamaa kaweka hadi title za vitabu husika ila mmeshindwa kujiongeza kugoogle vina kurasa ngapi ngapi. Au mkisia vitabu mnaelewa nini?!
 
Kwa hili kama linaleta mjadala nadhani watanzania wenzangu hususan vijana tunaanza kukosa maarifa ya msingi, kusoma vitabu ni hobby kama walivyo walevi wa pombe na ngono, kuna anayekunywa bia mbili na mwingine pampula.
Kuna wasomaji wazuri tu wa vitabu na wanajulikana huwa wanasoma mpaka zaidi ya vitabu 50.
Kitila Mkumbo na Jaunuary Makamba wanasoma vitabu vingi sana kwa mwaka kwani ndio ulevi wao, mimi mwaka 2018 nimesoma 37 tu.
Na kuna watu mpaka wana group za kushea mafanikio yao ya kusoma vitabu. Hivyo acheni kila mtu afanye addiction yake na maisha yaendele kwani mwisho wa siku unapata maarifa mapya na exposure. Hii siyo siasa ni kusoma vitabu na kupata maarifa
kamanda,uhalisia ni muhimu sana.
 
Ukimuuliza kurasa ya 50 na 78 zinasemaje atakuambia nini? Huo siyo usomaji ni kupitia Vitabu . kwenye kusoma kunapoint of internalization with Author Ideas, ambayo ndiyo muhimu kwenye kusoma. Huyu kapitia pitia Vitabu 48.
 
Umeongea point moja inayonisikitisha sana.Hivi kwanini tunapoteza hela nyingi kwenye Mwenge? Mwenge una Siri gani,wameweza kuzuia sherehe nyingi ikiwepo ya Uhuru Ila Mwenge imekuwa nongwa.Mwenge una nini?

Sent using Jamii Forums mobile app

Hilo ni tambiko ili wananchi wasiweza kuhoji chochote zaidi ya kuwatii viongozi. Hiyo ndio siri ya kugeuza nchi hii kuwa masikini. Angalia wote wanaoshabikia mwenge ni washirikina wa hatari na waabudu madaraka.
 
kiukweli hata mie niliwaza sana hiyo jana kuhusu usomaji wa hivyo vitabu... maana kwa uelewa wangu vitabu 48 na kila kitabu lets say kina kurasa mia tuu, hivyo atakuwa amesoma kurasa 4800, na mwaka huu una siku 366 hivyo mimimum alisoma kurasa kumi kila siku hapo hajaingia bungeni, hajaenda ulaya kwenye kongamano la wanaharakati, hajasoma ilani ya chama chake, hajatekeleza majukumu ya kijamii... wakuu huyu jamaa ametulisha matango pori. Ama alikuwa anasoma vijarida ndo anatuhadaa kuwa ni vitabu?
Kwamba akienda ulaya au kwenye kongamano lolote, vitabu anaviacha UJIJI!??

Unatumia nini kufikiri?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nimeamini kuna watu wajinga (sio tusi) either UJINGA wao unatokana na itikadi za vyama Au Hawako exposure Au uwezo WA kufikiri ni finyu. Mbona VITABU 48 NI VIDOGO KWA MSOMAJI? nashangaa kuona watu hawaamini. Zitto ni msomaji mzuri wa vitabu ITS POSSIBLE KUSOMA HIVO VITABU NA ZAIDI. Its matter of timetable hata Kama una majukumu Mengi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
  • Vitabu 48 tuchukulie wastani kila kitabu kina kurasa 200.
  • Inamaana ni jumla ya kurasa 9600.
  • Kwa msomaji wa kawaida anaweza kusoma kurasa moja kwa dakika 2 - 5 kutegemea na maada husika tuchukulie wastani wa dakika 3.5.
  • Ina maana kurasa 9600 zingemchukua dakika 33,600.
  • Dakika 33,600 ni masaa 560.
  • Mwaka una siku 365, kwa kila siku ukitenga masaa 2 kwa ajili ya kujisomea kitabu unapata jumla ya masaa 730...masaa zaidi ya muda ambao unahitajika kusoma hivyo vitabu 48.
Tatizo wengi wetu tunachukulia kusoma kama ni adhabu ama kitu kigumu ndio maana tunashangaa tukisikia kitu kama hicho.

Binafsi nimesoma vitabu 25+ pamoja na kuwa na majukumu mbali mbali.

Ukimsimiliza Zitto pamoja na mapungufu yake ni mtu anayeonekana kuwa na maarifa mengi tofauti na wasomi mbali mbali waliosawa na hata waliomzidi kielimu inawezekana ikawa ni kwa sababu ya kujisomea vitabu mbali mbali na kupata maarifa ya ziada yanayomsaidia wakati wa kujenga hoja iwe ya uongo ama ukweli.
Umeeleza vema sana mkuu....

Nchi imejaa kizazi cha wavivu....vijana wengi wanawaza pombe na mademu...ndiyo maana they can't reason, wanaona vitabu 48 ni impossible task ingawa wana spend hours kwa siku wakiwa kwenye social media.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ukitaka kujua Zitto anasoma vitabu vingi muweke na jiwe kisha wahoji uelewa wao wa mambo mbalimbali na sikiliza majibu utakayopata toka kwao.
mbona alipotaka kuwa mwenyekiti chadema mlimfukuza kwa dhihaka?Zitto na DJ nani muelewa?
 
Back
Top Bottom