John Mnyika
JF-Expert Member
- Jun 16, 2006
- 712
- 1,240
Zitto alia na Mzumbe kuzuia mjadala wa madini
na Nasra Abdalah, Morogoro
MBUNGE wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe, amelaani kitendo cha uongozi wa Chuo Kikuu cha Mzumbe kuzuia kufanyika mjadala wa kitaifa juu ya sekta ya madini na kusema jambo hilo ni aibu kwa taifa.
Mjadala huo uliodhamiwa na Kampuni ya Capital Promoters ulitarajiwa kufanyika jana, chuoni Mzumbe baada ya kufanyika Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustine cha Mwanza.
Kwa mujibu wa tamko lake la kwa vyombo vya habari kulaani utawala wa chuo hicho kuzuia mjadala wa madini kufanyika chuoni, mbunge huyo alisema jambo hilo limemshtua kwani anaamini kuwa mjadala huo ungechochea majadiliano kwa jamii ya wanazuoni kwa lengo la kuibadili sekta hiyo ili kuinufaisha jamii.
Nimeshtushwa na uamuzi wa Chuo Kikuu cha Mzumbe wa kuzuia mdahalo huu katika eneo la chuo, kwani mjadala huu unachochea majadiliano kwa jamii ya wanazuoni ili kuibadili sekta ya madini iweze kufaidisha maisha ya Watanzania, alisema katika tamko lake.
Zitto katika alisema jambo linalofanya maamuzi hayo ya chuo kuwa ya ajabu na aibu kwa taifa linatokana na ripoti ya hivi karibuni ya Action Aid iliyoitwa Breaking the Curse, iliyothibitisha namna ambavyo nchi za Kiafrika zisivyofaidi sekta ya madini, Tanzania ikiwa ni miongoni.
Alisema baada ya Shirika hilo kutoa ripoti hiyo na mapendekezo yake kwa mabunge na serikali, kampuni za madini zimepinga na sasa zimejitokeza na kufanya majadiliano ya wazi juu ya sekta hiyo jambo ambalo awali halikufanyika.
Hivyo mjadala umekuwa wa pande zote, ndiyo maana wanazuoni kama wadau walipaswa kutilia maanani mijadala hii, hivyo Chuo Kikuu kuzuia mjadala wa sekta nyeti na yenye malalamiko makubwa kama hii ni jambo la ajabu na aibu kwa Taifa, alisema.
Akimnukuu hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, katika hotuba yake Chuo Kikuu cha Dar es Salaam aliyoiita Jukumu la Vyuo Vikuu, mwaka 1966 alisema chuo chenye wanafunzi na wahadhiri wake wasioshiriki mijadala hakina faida kwa jamii.
Zitto aliwapa pole wanafunzi hao waliojiandaa kushiriki mdahalo huo na kusema kitendo kilichofanywa na utawala wa chuo hicho unatakiwa kulaaniwa na kwamba kitendo hicho kinadhihirisha taarifa iliyotolewa hivi karibuni kuwa zaidi ya wahadhiri wake 15 wamepata shahada zao za uzamivu katika vyuo visivyotambuliwa.
Naye Mkurugenzi wa Kampuni Capital Promoters International (CPI) ambayo imedhamini mdahalo huo, Gabriel Nderumaki, alieleza kusikitishwa kwa mkutano huo kuzuiwa kwani kampuni yake ilikuwa imetumia kiasi cha sh milioni 20 kwa ajili ya maandalizi.
Alisema taarifa za kuzuiliwa kwa mkutano walizipata juzi jioni wakati wakiwa hatua za mwisho za maandalizi, muda ambao umekuwa mgumu kwao kuwaarifu wawezeshaji ili kuairisha mdahalo huo.