Zitto ahusishwa na Rostam Aziz - Mwana Halisi

Status
Not open for further replies.
Na Mwisho wa Wafitini ni Kuumbuka tu na ndiyo maana watu wameanza kufuta Post zao humu baada ya Kugundua Kwamba Kuna siku wataambiwa Wazimeze lakini Watashindwa

Kufuta post zangu sio kuwa namuogopa mtu wala kuogopa kitu. Nimefanya hivyo kwa kuwa niliamini kuwa kuna mahala, hata kama ni ukweli niliousema lakini kitendo cha kusema hapa ama style ya kuyasema nilikosea na pia nilitegema huu mjadala ungeisha kwa faida ya wote. Hakuna siku ninayoweza kutakiwa kuyameza niliyoyasema kwani nina uhakika nayo na ninayaamini na nitayasimamia mpaka mwishio............

Tatizo hapa wakati mwengine unajikuta una deal na vichwa maji ambao kwao siasa ni kama kamchezo ama deal fulani na hivyo unapogundua hilo ni busara kukubali kushindwa kama nilivyofanya lakini sio kuwa ninamuogopa yeyote ama kitu chochote...............
 
UPANDE WA PILI. Unasema Mbowe anawatumia akina Kubenea kwa maslahi yake Binafsi. Kimsingi wanachofanya akina Kubenea ni kile ambacho Mbowe anakitaka. Nani asiyejua kuwa hakuna Gazeti ambalo limekuwa likiandika habari za ufisadi wa RA kama Mwanahalisi? Hivi huyu Mbowe ambaye 'anamiliki' Mwanahalisi na wakati huo huo 'anamilikiwa' na RA angewezaje kurusu Mwanahalisi 'limchafue' King maker wake?

Samahani, hakuna aliyesema kuwa Mbowe ni mmiliki wa Mwanahalisi. Wamiliki wa Mwanahalisi ni Anthony Komu (Mkurugenzi wa Fedha wa miaka mingi CHADEMA) na Said Kubenea...
 
face book wanaruhusu kudeactivate account na kuactivate wakati wowote ule unapojisikia, nadhani hilo swali ungemuuliza mhusika mwenyewe zitto angeweza kukusaidia na sio hapa jamvini.. kujitoa fb is personal issue


wengine tumechoka na thread za zitto kila siku humu
 
Kufuta post zangu sio kuwa namuogopa mtu wala kuogopa kitu. Nimefanya hivyo kwa kuwa niliamini kuwa kuna mahala, hata kama ni ukweli niliousema lakini kitendo cha kusema hapa ama style ya kuyasema nilikosea na pia nilitegema huu mjadala ungeisha kwa faida ya wote. Hakuna siku ninayoweza kutakiwa kuyameza niliyoyasema kwani nina uhakika nayo na ninayaamini na nitayasimamia mpaka mwishio............

Tatizo hapa wakati mwengine unajikuta una deal na vichwa maji ambao kwao siasa ni kama kamchezo ama deal fulani na hivyo unapogundua hilo ni busara kukubali kushindwa kama nilivyofanya lakini sio kuwa ninamuogopa yeyote ama kitu chochote...............

hata kufuta kwako hakuna msaada kwa kuwa ninazo kwenye archive.i will be on your face one day
 
Samahani, hakuna aliyesema kuwa Mbowe ni mmiliki wa Mwanahalisi. Wamiliki wa Mwanahalisi ni Anthony Komu (Mkurugenzi wa Fedha wa miaka mingi CHADEMA) na Said Kubenea...

ulisema bana wee!tena in a very provocative and abusive language
 
Inaelekea mngependa sana kuona kuwa Tanzania inasheheni populist politicians mkiamini kuwa hao ndio watawakomboa katika majanga tuliyonayo? Hivi hata baadaya hasara ya mabilioni tunayolazimika kulipa kwa hao DOWANS, Kukosa mitambo na sasa miaka minnne ya kukosa umeme wa kutosha bado mnaamini kuwa msimamo ule wa Zitto hakukupaswa kuwepo kwa kuwa ulikuwa unpopular? Hivi hizo popular politics zenu kuhusu Richmond na Dowans zimemsadia vipi mtanzania hadi leo zaidi ya kuwezesha kuwafanya mahasimu wa siasa za makundi ndani ya CCM kumantain their position na huku watanzania wakiendela kusuffer...

Wameshamtumia hawana shida nae...utajua si muda mrefu
 
Waberoya;1375911[COLOR="red" said:
]Mtani siku ukionyeshwa check ya RA kumkopesha Mbowe million 133 naona tutakupa nyundo ya kilo kumi hiyo haikutoshi![/COLOR]

Ni hivi: haondoki mtu chadema, piga ua, na ya kuwa walioanzisha hili sakata tutacheza nayo na mwisho wao ni aibu!!

Kama vipi tukutane kwenye uchaguzi, watu wajaze fomu na kura zipigwe dhahiri, hakuna kupendelea!

Unakumbuka zile ngumi za utotoni! vua viatu kwanza, usiume(using'ate), usishike mawe! hakunakutukana matusi, MSTARI UNACHORWA CHINI!!

Believe me tofauti na wengi unavyowadhania humu JF, ZK anapendwa na ordinary members wengi sana, kama mnamtuhumu aliweza kuwabadili mawazo wabunge-I mean wabunge 10 je hao wanachama! HIKI KICHWA NI THREAT WAnajuuuuuuuta kumtambua!

Haki uinua taifa na uinua chama

Mbowe abaki mshauri tu na mfadhili wa chama-au loan requestor, Tundu Lissu (baada na yeye kuacha unafiki) katibu mkuu, chair ZK, Slaa nje!!!maana kama ameshindwa kutatua matatizo ya chama kidogo angepewa nchi je!!
Kaka hapo kwenye nyekundu. Ni vizuri ukaiweka ili iwe ni ushahidi.
 
Imetosha Mmeshamsema sana Zitto jamani,mmejaa roho mbaya na chuki, mwenzenu yupo zake jimboni Kigoma anakutana na watu wake nyinyi majungu tu!
 
amani iwe kwenu ma-great thinkers!

Hii leo gazeti la mwanahalisi limetoa ripoti ya kina kuhusiana na maongezi ya simu ya mara kwa mara kati ya Rostam Aziz na zitto kabwe. Hata hivyo gazeti halikuweza kupata mada waliyokuwa wanaongea akina zitto hivyo limetoa tu muda wa maongezi kati ya watu hao. Mfano zitto akitumia simu no. +255756809535 na rostam no. +255754555555 walifanya mawasiliano tarehe 11/08/2010 saa 7:08, saa 22:09, saa22:28, saa 22:49, saa 22:44 na saa 22:45. Wakati mawasiliano hayo ya simu yanafanyika simu ya zitto ilisomeka kuwa yuko uzunguni, dodoma huku simu ya rostam ikisomeka kuwa yuko area d, dodoma. Pia mawasiliano mengine yalifanyika siku mbili kabla ya kikao cha wabunge wa chadema kule bagamoyo huku simu ya zitto ikisomeka yuko ohio, dar.

Huu ni mwendelezo wa machapisho ya wiki iliyopita kuhusiana na maongezi ya mara kwa mara kati ya zitto na jack zoka (bosi wa tiss).

Hebu tujiulize hivi kweli zitto achukuliwe hatua gani za kinidhamu? Kwa sababu gazeti limemnukuu mama mzazi wa zitto akisema mwanawe ni mkorofi na sii msikivu. Karibu great thinker tujadili.

Usipowajua wanasiasa mwisho wa siku aibu itabaki kwako. "WANASIASA SIO WATU WA KUAMINI"
 
Nimeongea na Zitto anasema alikuwa akiwasiliana na Rostam kumtuliza asidai mamilioni yake aliyompa Mbowe katika uchaguzi wa 2005 na ule wa Tarime (by election) baada ya kugundua kuwa Mbowe amekuwa akidai hizo ni fedha zake na kulazimisha CHADEMA wamlipe kutoka katika ruzuku.........Inakutosha hiyo ama unahitaji nyingine.....

:A S-confused1: :A S-confused1: he?
 
By Waberoya Mimi nimekuwa nikimfuatilia mheshimiwa Zitto, tangu alipoongoza mapinduzi ya kupindua serikali ya DARUSO mwaka 2002/2003 wakisaidiana na Ridhwan Kikwete na Omar Ilyas. Kipindi hicho nikiwa mmoja wa mawaziri wa serikali, ambayo ilipona kupinduliwa. Na tumekuwa wote ndani ya bunge la UDSM-USRC

Mimi personally nimekuwa muwazi sana na mkweli katika kila kitu kinacholigusa taifa hili na hasa uhuru wa mawazo na maoni ambao umedhihirika kuwa watanzania wengi sio kuwa hawana, bali huwa wepesi sana kuamini mambo na ni waoga kuonekana wanapingana na hali iliyopo.

Mtazamo huu umenifanya nimpende Zitto na JF members wowote wale ambo huwa wanapenda kufikiria nje ya box, au another direction/angle. Zitto amekuwa akinifurahisha kwa kuleta changamoto za kuleta mawazo tofauti na kile ambacho wengi huwa wanafikiria.

Zitto ni kweli anapenda sifa, kama binadamu mwingine yeyote yule, ila unapotaka sifa kwa kusimamia haki na ukweli na hasa unapopigania haki basi sifa hii ni sifa timilifu na inapendeza. Omar Ilyas naye alikuwa mmoja wao wa wanaopenda sifa ila kwa sasa naona amekua kidogo, nadhani Salim A Salim amemkuza.

Si nia yangu niwaharibie hawa jamaa , ila ni hali yangu kueleza ninachowaza baada ya kuwafuatilia hawa watu tangu enzi hizo. Sijajua status ya Omar Ilyas kwenye issue nzima za udini, siwezi kumtuhumu, personally nimemuona ni mtu mzuri tu na anayependa wote pasi kujali udini ila bado ni rafiki wa Zitto!

Tuendelee: Role model wa Zitto ni Salim A. Salim, rais bora kwake yeye ni Kikwete, MD bora aliyewahi kumsema yeye ni Rashid Idrisa yule wa TANESCO.

Tie, cord, umoja, Urafiki wa Zitto, Ridhwan, Omar Ilyas ni mkubwa sana kuliko maelezo, hili group lililotaka kuipindua serikali ya Kayombo-DARUSO, ili wao wapate madaraka si tu ni la hatari bali la kuangaliwa sana. Ridhwan amekuwa akijitetea sana yeye anataka ku-practise sheria hili hali kutaka uongozi amekuwa akitamani tangu siku nyingi sana.

Ukiwa rafiki na Ridhwan umekuwa rafiki wa Kikwete!!! Huwezi kuwa adui wa JK ukawa rafiki wa Ridhwan, JK si tu anampenda Ridhwan kama motto, bali kama mwanaCCM mwenzie aliye tayari kulinda interest zao.

Si ajabu Zitto kuwa alikuwa mmoja wa wanakamati ya bunge ya kuchunguza madini, maana JK anampenda Zitto, ambaye ni rafiki wa Ridhwan!

Alichotamka Juzi ni mwendelezo wa kumuonyesha JK kuwa yuko ‘NAYE’ na yuko mbali na chadema na kuwa yeye hakuwa na mawazo kama wanachadema wengine!!!. Hakuishia hapo tu bali alisema JK amefanya mengi Kigoma! Hivyo hakuona sababu ya kutoka nje ya bunge, kwa hiyo hakwenda kabisa, Huu ujumbe haukuwa kwa wananchi, ulikuwa unaenda kwa JK rafiki yake! Hata kama JK kafanya mambo mengi huko jimboni kwake Kigoma ni wajibu wake kama rais na haikuwa zawadi.

Kilichonifanya nijiulize je what makes Zitto na JK kuwa marafiki? Je Zitto na JK walikuwa wanajuana kabla ya JK kuwa rais? Definitely Yes!

Je swali gumu na baya ambalo halina ushahidi ni je Zitto kuwa inclined kwa JK, Salim na kuwapenda baadhi ya viongozi wa kiislam je ni mdini?..........I mean chunguzeni hili. May be not! Kindly don’t conclude! What Salim teaches Zito?? Salim is CCM, is Salim and JK close friends? Cause Ommy and Zitto are close friends, Ooh! Ommy ni personal assistant wa Salim, Nauliza Kama Ridh, Zitto, Ommy ni marafiki then Salim and JK ni maadui? Find out please. However, we all know JK ni mdini, maana alianza harakati za udini tangu akiwa UDSM miaka hiyo….na hili fuatilieni

Nani anayejua Zitto ana mtambo wa kusaga kokoto na alipata tender ya barabara ku-supply kokoto? Is he defending his interest indirectly?

Au ni kuwa ni great thinker ambaye anaishi kwa falsafa zake ambazo hatuzijui! Je mnafikiri Zitto kuwaambia waandishi wa habari yaliyojiri ndani ya chadema alikuwa hajui watu watamrudi? Who is greater to him? JK, wananchi wake Kigoma, mali au?

I mean we should be careful na watu kama Zitto yes they are bright, mmh! But they might be dangerous for the opposition existence. But we should examine him carefully and not judge him. Nimegusia tu swala la uislam maana mpaka leo kuna baadhi ya waislamu wanaofikiri kuwa wanaiweza kuigawa nchi hii kidini, na kuna wakristo wanaofikiri wanaweza kuigawa nchi hii kidini.

That’s bringing another bitter question how far do we believe these opposition leaders? I mean all!

That said, I am just thinking
 
Mkuu Mtazamao, umeandika mada nzuri sana hasa kuhusu Zitto katika harakati zake za kutaka kufanya mapinduzi DARUSO. Hivi wakati ule Rais wa DARUSO alikua nani vile?
 
Kumbukumbu za JF ni hatari, Moderator tunaomba mzifunge post zote watu wasihariri ili tuondoe unafiki wa kisiasa.

Ni kweli kabisa mkuu kuna kila sababu ya hizi threads za zamani kulindwa kwakuwa watu wamekuwa wakibadilika kila siku kama vinyonga.

Wanaweza kusoma hapa walichokuwa wakikiandika siku za nyuma wakajiona wamejivua nguo na usalama wao ukawa ni kufuta posts zao kama ambavyo mmoja alistuka siku nyingi na kuanza kuzifuta.
 
Last edited by a moderator:
Mkuu Mtazamao, umeandika mada nzuri sana hasa kuhusu Zitto katika harakati zake za kutaka kufanya mapinduzi DARUSO. Hivi wakati ule Rais wa DARUSO alikua nani vile?

Mkuu hii iliandikwa na Waberoya , huyu jamaa baadae alibadili msimamo na hii stori yake ilitumika sana kuhoji msimamo wake.
 
Last edited by a moderator:
Sasa mkuu itakuwaje kama Zitto atakataa kujiuzulu nyadhifa zake ndani ya chama na bunge? Nasema haya kwsbabu kuna siku ZT mwenyewe alisema hakuomba uongozi ndani ya chama ila ni wao wenyewe walimpa baada ya kujiridhisha kuwa anafaa. Akaongeza, kawa wanaona sifai basi waniondoe lkn sii mimi nijiondoe kwani sikuomba kupewa cheo.

Post hii iliwekwa 15-Dec-2010. Sasa yametimia. Haiwezekani kwa kipindi chote hiki tuhuma Zilezile ziwe zanajirudia na au kufanana.
Naanza kuamini yale aliyosema Pro. Muhongo juu ya huyu jamaa. Mwenye ile clip atuwekee hapa.
 
Great thinker siku hizi wengi wamepunguza kufikiri, kwa kuwa wanaongozwa kwa hisia na jazba nyingi bila kuwa watu wakufikiri.
Kuna mambo ambayo hunishangaza sana kwa kuwa watu hawa ambao wanaongelewa vibaya kwenye jamii hii ndio hao wanaotoa pesa za madawati kwa watoto wetu, wanajenga makanisa, wanainua vikoba kwa wakina mama na mengine mengi tu.
Pili kuna wabunge wengi tu wanao ongea na watu hao, hivyo mwana halisi kama gazeti ningeona ni busara kutuambia watu hao katika uchunguzi wao walikuwa wanaongea na nani na nani ili tufahamu, kwani RA kuongea na ZZK sioni kama ndio mawasiliano pekee yamefanywa na watu hao kwa kipindi chote hiki ambacho mwanahalisi wanasema walikuwa wana wasiliana.
Mimi na jiunga na mchangiaji mmoja ambaye anasema ni vema kufahamu maongezi yalikuwa nini, inaweza kuwa maongezi yalikuwa yana husu utani wa mechi ya simba na yanga au liverpool na arsenal then sioni kama kuna afya kwenye maongezi hayo.
Pili hata kama kuna mawasiliano then hatuwezi kumchagulia mtu marafiki, mbona mnahisi kuwa ZZK ndio anatoa siri za Chama chake mbona humtaki kuamini kuwa labda RA na yeye humpa habari za chama chake.
Mimi na fikiri Mwanahalisi wanatafuta kuuza gazeti lao na hasa wakati huu ambao kuna matatizo ya kisiasa na sivinginevyo.
Kuhusu upande kuwa ana mawasiliano na Jack Zoka , kwanini hawa waandishi wanofatilia haya mambo wasije na habari kamkili mimi na kuwa na mashaka sana na ufanisi wa hawa watu, kwa kuwa kuhukumu mtu inakuwa vigumu sana kwa kuwa kama hakuna maaongezi tunahukumu vipi?
nawakilisha
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom