Zijue faida za Mmea wa Mlonge, Jitibu magonjwa 300 kwa kutumia mlonge

Usiyaanike juani maana wataalamu wanasema ukianika juani content yake ina-evaporate. Fanya kuyasambaza ndani ambapo jua halipigi, yakikauka unayasigina kupata unga wake
 
mi natafuna sa hizi huwa natafunaga tu bila sababu ila zinanipa hamu ya kula sana njaa itawaka saa hizi mi natafuna mbegu ila sijui jinsi ya kutengeneza unga
 
Majani ya mlonge longe hayaanikwagi juani.
Unachokifanya unayaweka kivulini baada ya kuyachuma na itachukua siku tatu hadi nne kukauka,
Baada ya hapo unayatwanga na kuyachekecha, yatakua unga mlaini sana.

Ukiyaanika juani virutubisho vingi vinapotea kwa sababu ya evaporaion na hivyo unabaki na makapi tu.
Ndio maana haushauriwi kununua kutoka kwa wafanyabiashara maana wengi huwa wanaanika juani kwa sababu ya tamaa ya pesa.
 
Mwenye picha ya mlonge plz au jina lake kwa kilugha cha Google ili tu prove na tulione hilo li mti
 
Mwenye picha ya mlonge plz au jina lake kwa kilugha cha Google ili tu prove na tulione hilo li mti
Unaitwa Moringa Oleifera kwa jina la kitaalamu

images

image001.jpg

image3.jpeg

Fresh_Moringa_Leaf_1.jpg
 
Majani ya mlonge longe hayaanikwagi juani.
Unachokifanya unayaweka kivulini baada ya kuyachuma na itachukua siku tatu hadi nne kukauka,
Baada ya hapo unayatwanga na kuyachekecha, yatakua unga mlaini sana.

Ukiyaanika juani virutubisho vingi vinapotea kwa sababu ya evaporaion na hivyo unabaki na makapi tu.
Ndio maana haushauriwi kununua kutoka kwa wafanyabiashara maana wengi huwa wanaanika juani kwa sababu ya tamaa ya pesa.

Mkuu, yani nashukuru sana kwa maelezo yako yenye kujitosheleza. Swali la nyongeza... kiafya, nitumie vipi huo unga wa majani ya mlonge?

Ahsante
 
Mkuu, yani nashukuru sana kwa maelezo yako yenye kujitosheleza. Swali la nyongeza... kiafya, nitumie vipi huo unga wa majani ya mlonge?

Ahsante
Majani ya mlonge ni chakula tu kama vyakula vingine , wapo wanaopika kama mboga na kula na wanafaidika sana.
Kwa mtu anayetumia kama supplement tu bila ugonjwa wowote inashauriwa atumie unga wake kijiko kimoja kidogo cha chai kwa siku anaweka kwenye chai au uji au mboga, na kwa kuwa hayana ladha kali hauna madhara ya harufu, sana sana utaona tu ule ukijani wake ukiwa umeongezeka.
Kwa mgojwa anayetaka ku-Boost immunity au mama anayenyonyesha ambaye hana maziwa au mtoto mwenye utapia mlo au mgonjwa wa ukimwi inashauriwa kutumia vijiko viwili vikubwa vya chakula kwa siku yaani kimoja asubuhi au mchana na kimoja jioni,
unamix kwenye mboga au chai au uji au juice ya kutengeneza nyumbani.

Kumbuka Mlonge longe hauna madhara kwa binadamu kwa hiyo ukinogewa hata ukala vijiko 100 kwa siku haina shida labda kama mtu ana matatizo binafsi kama allergy.

Ipo mikoa ambayo inatumia majani yake kama chakula kabisa, na zipo institutions nyingi tu za kulea watoto zinawawekea watoto wadogo kwenye uji wao kila siku asubuhi na afya zao ni nzuri kweli kweli na hata uwezo wa watoto kiakili una-improve sana.
 
Mkuu, ahsante na ubarikiwe sana, umeeleza vizuri kila kitu na kwa faida ya wasomaji wengine pia. Sina la ziada.

cheers brother
 
Mlonge au moringa oleifera kwa kiingereza umekuwa ukijulikana kama mti wa miujiza kwa karne nyingi katika baadhi ya nchi za Afrika, Asia na katika nchi za Caribbean. Mti huu umeripotiwa kutibu zaidi ya magonjwa 300 ikiwemo magonjwa mbalimbali sugu.

Karibu kila sehemu ya mti huu hutumika kama dawa. Majani ya mlonge yanaweza kutafunwa mabichi, yaliyochemshwa kama mboga au yaliyokaushwa na kusagwa kuwa unga. Unga wa mlonge unaweza kuhifadhiwa kwa miezi kadhaa bila kupoteza ubora na faida zake za kiafya.

Mbegu za mlonge zimekuwa dili kubwa duniani kwa sasa, zinahitajika kwa kiasi kikubwa katika nchi ya Marekani na China na kwa mujibu wa taarifa ni kuwa zinauzwa mpaka 45000 ya Tanzania kwa gramu 500. Walikuja pia wachina kuzinunua kwa wingi na walikuwepo hapa bei ya mbegu za mlonge ilifika mpaka 11000 kwa kg kwa bei ya jumla yaani kwa anayechukua kg 100 au 500 au 1000 na kwenda juu. Taarifa zisizo rasmi zinadai wachinja hawa walikimbia nchini baada ya serikali kuanza kufuatilia na kuwakamata wakwepaji kodi bandarini. Isingekuwa hivi mpaka leo mlonge ungekuwa umeshatowka wote Tanzania.

Faida za mlonge zimeandikwa na majarida ya afya na lishe kadhaa duniani. Kile ulikuwa hujui ni kuwa viwanda na makampuni mengi ya dawa za hospitalini yamekuwa yakitumia virutubishi vilivyomo kwenye mti huu kutengenezea madawa kwa ajioli ya binadamu na wanyama.

Mlonge una:

Kalsiumu mara 17 zaidi ya ile ya maziwa ya ng’ombe

Potasiamu mara 15 zaidi ya ile ya kwenye ndizi

Una vitamini A mara 10 zaidi ya ile ya kwenye karoti

Una protini nyingi mara 9 zaidi ya ile ya kwenye mtindi

Una klorpfiti (kemikali ya rangi ya kijani ipatikanayo katika mimea) mara 4 zaidi ya ile ya kwenye nyasi au majani ya ngano (wheatgrass)

Una madini chuma mara 25 zaidi ya yale ya kwenye Spinach

Una vitamini A mpaka Z

Una omega 3, 6 na 9

Una asidi amino zile muhimu zinazohitajika na mwili

Una kiasi cha kutosha cha madini ya zinc ambayo ni madini muhimu katika kuongeza homoni za kiume na nguvu za kiume kwa ujumla

Mlonge ndicho chakula chenye afya zaidi juu ya ardhi:

Mlonge una jumla ya virutubishi 92, mmea au mti mwingine wenye virutubishi vingi basda ya mlonge una virutubishi 28. Mlonge una vionsa suku 46 na viondoa uvimbe mbalimbali mwilini 36, una asidi amino 18 na asidi amino muhimu zaidi 9 ambazo miili yetu haina uwezo wa kuzitengeneza.

Unga wa majani ya mlonge unao uwezo wa kutibu magonjwa zaidi ya 300 mwilini, magonjwa hayo ni pamoja na :

1. HUko Afrika magharibi madaktari hutumia mlonge kutibu kisukari.

2. HUko India mlonge hutumika kutibu shinikizo la juu la damu

3. HUtibu matatizo u maumivu ya mishipa

4. Hutuliza mapigo ya juu ya moyo

5. Hutibu kansa

6. Pumu

7. Hutuliza wasiwasi

8. Kikohozi

9. Maumivu ya kichwa

10. Inazuia na kushusha ile lehemu hata ile ya juu zaidi

11. Inapunguza mafuta tumboni

12. Inaweza sawa homoni

13. Inatibu maumivu wakati wa hedhi

14. Unasafisha ini

15. Inasafisha mkojo na kibofu cha mkojo

16. Inarekebisha matatizo kwenye tezi

17. Unatibu kipindupindu na kuharisha

18. Kifua kikuu

19. Kichwa kizito

20. Uchovu

21. Mzio

22. Vidonda vya tumbo

23. Maambukizi kwenye ngozi

24. Maumivu mbalimbali mwilini

25. Huondoa madoa doa meusi kwenye ngozi

26. Husafisha damu

27. Hutibu matatizo kwenye koo

28. Huondoa makohozi mazito kooni

29. Huondoa taka na msongamano kifuani

30. Hutibu kipindipindu

31. Huondoa moto wa jicho au uvimbe kwenye jicho

32. Hutibu maambukizi kwenye macho na kwenye masikio

33. Unatibu homa

34. Maumivu kwenye maungio

35. Huondoa chunusi

36. Hutibu matatizo karibu yote ya ngozi na kinga ya mwili

37. Matatizo kwenye mfumo wa upumuaji

38. Inatibu kiseyeye

39. Huongeza uwingi wa mbegu za kiume na nguvu kwa ujumla

40. Inatibu minyoo

41. Huongeza maziwa kwa wingi kwa mama anayenyonyesha

42. Huondoa uvimbe kwenye utumbo mpana

43. Inatibu ugonjwa wa kuvimba mwili

44. Inatibu kuhara damu

45. Inatibu kisonono

46. Unatibu tatizo la kukosa usingizi

47. Unatibu homa ya manjano

48. Unatibu malaria

49. Unatibu U.T.I na matatizo mengine kwenye mfumo wa mkojo

50. Unasaidia pia kujenga na kuimarisha misuli

51. Unatibu magonjwa ya mifupa

Mlonge uansafisha mwili wako wote, unasafisha ini, figo, moyo, macho, unaimarisha meno, ngozi na nywele. Wakati unatumia mlonge unakufanya ujisikie vizuri, ujisikie mpya na mwenye nguvu. Watu wengi wanaotumia mlonge huwa ni wenye afya nzuri hata kwa muonekano tu hata wanapokuwa na umri mkubwa zaidi ya miaka 90.

Majani ya mti wa mlonge pia yanaweza kutumika kutengeneza biogas. Hutumika pia kama chakala cha wanyama kama sungura , mbuzi, ng’mbe. Mbwa n.k. Sungura wanaonekana kupenda zaidi mlonge kuliko wanyama wote.
 
Tuweke pictures za majani yake na mti tuufahamu vizuri ni jina ngeni kwetu
 
Wakuu kama nilivyoandika hapo juu. Ninahitaji unga wa majani ya mlonge. Niko Mwanza
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom