Bwana Banzi
JF-Expert Member
- Oct 14, 2014
- 382
- 174
ZIJUE BAADHI YA KOO ZA KIZARAMO, ASILI NA MAANA YAKE.
Wazaramo/ wazaramu ni kabila linalopatikana mkowa wa Pwani, Daresalama na maeneo ya mkowa wa morogoro ( morogoro vijijini, hasa mvua na dutumi). Wazaramu wana koo nyingi sana zisizopungua arobaini (40). Baadhi ya koo hizo (koo zilizonyingi) hufanana na koo zinazopatikana katika kabila la waluguru, wakwere na pia wakutu. Kwa leo tuangalie hizi koo kwa upande wa waluguru na wazaramo. Waluguru hupatikana zaidi mkowa wa Morogoro, na Mkowa wa pwani, na bagamoyo. Zifuatazo ni baadhi ya koo za kizaramo zilizotokana au kufanana moja kwa moja na Waluguru:
1.Ukoo wa Kolelo: huu ni ukoo ambao asili yake ni kule kolelo kwenye mizimu ya asili ya uluguru. Ukoo huu hupatikana katika kabila zote mbili za wazaramu na waluguru, mwanaume anaitwa kolelo n a mwanamke mlakolelo
2. Ukoo wa Wabunga: huu ni ukoo pia unaopatikana katika kabila la wazaramu japo uluguruni pia upo,
3.Ukoo wa Semindu (Wahindu): huu ukoo wa semindu ni ukoo wenye asili ya kutoka mlima mindu, masimulizi ya kale yanasema kwamba hii koo ilihama kutoka mlima mindu uliopo morogoro kwa sababu ya kukimbia majanga ya asili. Huu ukoo wazaramo huita ukoo wa semindu na uluguruni unaitwa wahindu, mwanaume huitwa hindu( mindu) na mwanamke mlahindu au wahindi kwa upande wa uluguruni. Kwa wazaramo mwanamke huitwa mindu na mwanaume semindu
4. Ukoo Wabena: huu ukoo wa wabena asili yake pia ni uluguruni, ina maana kubena ni kuvunja. Hawajamaa walikuwa wanabena ngodi(kuni), wabena migoha( wavunja mikuki). Mwanaume huitwa m’bena na mwanamke kibena au mlam’bena.
5.Wachuma na Wakalagale: ukoo wa wachuma na ukoo wa mkalagale ni koo zinazofanana( mkalagale, chuma kimejigalagaza). Mwanamke huitwa chuma au mlachuma na mwanaume huitwa Luanda( uluguruni). Mwanaume huitwa Chuma na mwanamke Mlachuma ( uzaramoni)
6. Mzeru: huu ukoo asili yake ni uluguruni, ni kwamba huu ukoo unasifika kuwa na watu weupe ( zeru au nzeru kwa maana –upe), kwa upande wa uluguru mwanaume huitwa mogela, na mwanamke ni mzeru/mlamzeru, pia kwa wazaramo mwanamke huitwa mzeru/mlamzeru.
7.Mponda: huu ukoo wa mponda pia unapatikana uluguruni na uzaramuni, ndio hao kina makala (makaa), au mponde
8. Mgombe: huu pia ni ukoo unaopatikana uzaramuni, kina kagombe ndio ukoo wao huu pia uluguruni upo
9. Ukoo wa kihemba/kilewa( Wahemba): huu ni ukoo ambao asili yake pia ni uluguruni, kwa waluguru huita WAKINOGE, kwa upande wa waluguru mwanaume anaitwa kobelo, berege,mwinyigoha, na mwanamke huitwa kinoge au kibua au kihemba... Uzaramoni, mwanaume huitwa kihemba na mwanamke huitwa mlakihemba ( kumbuka uhemba ni mtama kwa kiluguru/kizaramo)
10. Ukoo wa Kisuru: ni ukoo unaopatikana uzaramoni, lakini pia uluguruni hasa maeneo ya mgeta sehemu ya mongwe au nyuma yam lima wa kidiwa huu ukoo hupatikana huko pia.
11.Muhafigwa (Wahafiga): kwa wazaramo huita wahafigwa na waluguru huita wahafiga, kwa upande wa waluguru mwanamke anaitwa kiluwa na mwanaume anitwa mange au mveda
12.Mlali (mulali); huu ukoo kwa wazaramo mwanume huitwa mlali na mwanamke mlamlali, kwa upande wa waluguru mwanaume huitwa mlali au BWAKILA,mindoli, minyeko na mwanamke mlali au mlamlali
13. Mtonga, huu ni ukoo unaopatikana uzaramoni pia, mwanaume ni mtongana mwanamke mlamtonga. Pia asili yake ni uluguruni , kwa upande wa waluguru mwanaume huitwa MSUMI na mwanamke huitwa mtonga.
14. MWELUGURU; huu ukoo wa mweluguru hupatikana uzaramoni, maana yake ni kwamba mimi ni mluguru haswa, hujipambanua kwamba asili yangu ni mluguru. Kwa leo tuishie hapa koo zipo nyingi sana, kama msakuzi, setembe, sekamba, kizigo,setumbi, mponela, mkwayu,msemwa, mhondo, wa pazi, WAKILIMA(husema kwamba sisi ni wa mlimani kwelikweli, humaanisha wakutu/ waluguru), Mavula { kivula, Mwamvua, kibago, hayo majina kwa upande wa uluguruni na uzaramoni hutumika kuwakilisha ukoo wa mavula}.