Zifutwe Bungeni kauli zisemazo "Naunga mkono hoja" pia "Siungi mkono hoja"

Nikupateje

JF-Expert Member
Dec 22, 2009
1,334
988
Hujachelewa kuanza utafiti na kugundua kwamba tatizo liko zaidi kwenye wale wabunge wanaotumia kauli ya isemayo "Naunga mkono hoja" kuliko wasemao "Siungi mkono hoja".


Sasa hivi Spika amekuwa serious na muda. Ukizidisha nukta moja tu anakukatisha. Safi. Mbunge anapewa muda wa kuchangia hoja au bajeti. Anainuka kitini anakemea serikali, anaiponda bajeti. Unaona wazi huyu hakubaliani kabisa na bajeti.

Ghafla kengele ya pili ya Spika imamkatiza kwamba muda wake umekwisha. Na hata kwa wale ambao wanamaliza maelezo bila kukatishwa kauli yao ya mwisho inakuwa "Naunga mkono hoja"!

Unabaki unashangaa! Kwani kama asingetamka kauli hii, basi hata mtoto wa kindergatern ajuaye kusoma angeulizwa angesema huyu mbunge hakuwa anaunga mkono hoja.

Au kwa njia nyingine, ukipewa mtihani unao-quote michango ya wabunge wote mle bungeni. Halafu katika kila mchango wa mbunge ukaondoa ile kauli "Naunga mkono hoja" au "Siungi mkono hoja". Kisha ukauliza ni wangapi waliunga mkono na wangapi hawakuunga mkono hoja. Hakika unaweza kusema hiyo bajeti wala haikupita maana asilimia kubwa ya michango itaonekana kutounga mkono hoja.


Kumbe, ikiwekwa kanuni bungeni ya kutotamka kuunga au kutounga mkono hoja na kwamba mbunge ajikite kwenye hoja basi ni wazi atakuwa ametuachia uwanja sisi wenyewe wa kujua wazi kuwa kaunga au hakuunga mkono hoja.


Hahitaji kutuambia, sisi wenyewe tutapia hoja yake. Ukifika wakati wa kusema "ndiyooo" au "siyooo" atautumia ipaswavyo.

Hivyo, napendekeza ikiwezekana iwe marufuku kusema kauli hizi kwani tunachotaka ni content za maelezo ya mbunge.

Sijui wadau mnasemaje.
 
Back
Top Bottom