Zifahamu sheria zako za msingi ukikutana na Polisi; Fanya haya uwapo mikononi mwa Polisi

sky walker

JF-Expert Member
Feb 3, 2018
1,160
824
police.jpg

IMEANDALIWA NA MAWAKILI

1. Askari akikuweka chini ya ulinzi muulize kitambulisho ni haki yako.

2. Askari akikukamata akuoneshe kitambulisho chenye muhuri wa mahakama kama anasema ametumwa na mahakama kukumata, ni haki yako.

3. Askari akikukamata akwambie kwanini anakukamata na anakupeleka kituo gani, ni haki yako.

4. Unaruhusiwa na sheria kukataa kukamatwa hata kutumia nguvu kama hukuambiwa sababu ya kukamatwa.

5. Askari anapokiuka taratibu za ukamataji anageuka na kuwa mhalifu ni haki yako kujikinga naye.

6. Askari haruhusiwi kukuvuta shati, kukukaba koo, kukushika suruali kama hujakataa kutii amri halali.

7. Askari haruhusiwi kuondoka na mtu mwingine baada ya kumkosa mtuhumiwa halisi.

8. Askari haruhusiwi kupekua nyumba ya mtu bila kibali cha kupekua.

9. Askari lazima akuoneshe kibali cha kupekua na ukisome.

10. Kibali kieleze jina la aliyekitoa, kituo kilipotolewa,jina la mtu au sehemu ya upekuzi, au uchanganuzi wa mtu au sehemu.

11. Hairuhusiwi kupekuliwa usiku kuanzia saa 1 jioni mpaka saa 12 asubuhi.

12. Ni haki yako kumpekua askari kabla hajakupekua ili asipandikize kitu.

13. Usipekuliwa nyumbani bila kuwapo kiongozi wa mtaa.

14. Kila kitakachochukuliwa katika upekuzi lazima kiandikwe na askari aweke sahihi.

15. Mali iliyochukuliwa katika upekuzi lazima ibaki salama.

16. Mwanaume haruhisiwi kumpekua mwanamke na mwamke haruhisiwi kwa mwanaume.

17. Unaruhusiwa kukataa kupekuliwa iwapo taratibu hizi hazikufuatwa.

18. Askari haruhusiwi kukutukana wala kukupiga.

19. Unaruhusiwa kutozungumza lolote mpaka unayemuamini afike uwapo chini ya ulinzi, ni haki yako.

20. Usilazimishwe kuongea au kuandika ambacho hutaki, ni haki yako.

21. Usitoe maelezo bila uhakika yatatumika mahakamani yatakuletea shida.

22. Unaruhusiwa kukaa kimya na usizungumze kitu uwapo chini ya ulinzi.
 
usije ukajaribu kubishana na polosi Wa bongo wakati wanakukamata. utapigwa kama mbwa koko.

hawachelewi kukupa shaba na kwenye press ukapandishwa cheo na kuwa jambazi limeuawa wakati Wa majibizano ya risasi. tulimrenga mguu lakini kukwa na mawimbi lisasi ikawaza kumtoboa kisogoni.
 
Ndugu wanasheria.

Haya mliyoandika ni ya kweli na mazuri sana maana yanatupa mafasi kunifunza sheria inasimamia upande gani kwa raia.

Tatizo kubwa na la msingi, ni wapi askari wa kitanzania aliwahi kufuata sheria/utaratibu huu?

Zaidi ya yote mnamtafutia kilema na majonzi kwa watanzania watakaojitia kwa kumuuliza ndg AFANDE nioneshe kitambulisho chako.
 
Siku wakijua kutofautisha kati ya "kill him not, let him go vs kill him, not let him go". Hapo ndo nitauliza maswali pendekezwa hapo juu kama mleta mada alivyosema.
*Fear thou not, for the law is with thee"
 
Hao ni Askari wa nchi gani mkuu?

Askari ninaowafahamu mimi wa kule nchini bangaladeshi, ukibishana naye tu yafuatayo yatafuata.
1. Wewe ni mvutaji na muuza Bangi pamoja na madawa ya kulevya.
2. Wewe ni jambazi ulikuwa na silaha

Bora tu kuendelea na maisha yaliyopo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Waliniletea ujinga wa kulazimisha kunikamata eti nakunywa pombe SAA tano asubuhi, kitu ambacho siyo kabisa na eneo tulilokuwepo tulikuwa tunafanya makubaliano ya chumba cha biashara.

Walifika na gari lao wasimama, kiongozi wao akaamrisha kamateni na hao!! Akaja askari mmoja toka kwenye gari lao yuko kiraia akaniambia ingia kwenye gari, nikamuuliza we nani? Akajibu huoni hiyo gari?nikamuuliza kwani INA nini? Akaniambia unaleta jeuri?

Akanishika Tanganyika jerk, nikamuambia niachie, akataka kunisukumizia mbele, nikamsukuma mda huo wenzie kama 8 hivi wanaangalia tu.

Wakaja wawili, nikawablock mikono yao, yule wa mwanzo akarusha ngumi, nikamblock nikampa ngumi ya kichwa akapepesuka, wakajaa kama nyuki, nilipigana siku ile, hawa jamaa hawanaga nguvu kabisaa, nilimchania shati mmoja aliyevaa kiraia mpaka kabaki na vest/singlet.

Wale wenye bunduki wakanionyeshea bunduki nikanyoosha mikono juu kutii amri ya silaha, ilikuwa ni sinema kama yah Hollywood.
Sikukaa hata lisaa wakanitoa mwenyewe baada ya kushauriana wao kwa wao.

Nilipiga hao polisi kipigo cha mbwa koko.

They don't care on arrest tactics, they rely on brutal methods.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
usijaribu hata mara moja tena wanatabia ya kuongozana na mgambo
hawa wanaweza wakakung'oa hata meno tena wengine hao migambo ni wezi
 
police.jpg

IMEANDALIWA NA MAWAKILI

1. Askari akikuweka chini ya ulinzi muulize kitambulisho ni haki yako.

2. Askari akikukamata akuoneshe kitambulisho chenye muhuri wa mahakama kama anasema ametumwa na mahakama kukumata, ni haki yako.

3. Askari akikukamata akwambie kwanini anakukamata na anakupeleka kituo gani, ni haki yako.

4. Unaruhusiwa na sheria kukataa kukamatwa hata kutumia nguvu kama hukuambiwa sababu ya kukamatwa.

5. Askari anapokiuka taratibu za ukamataji anageuka na kuwa mhalifu ni haki yako kujikinga naye.

6. Askari haruhusiwi kukuvuta shati, kukukaba koo, kukushika suruali kama hujakataa kutii amri halali.

7. Askari haruhusiwi kuondoka na mtu mwingine baada ya kumkosa mtuhumiwa halisi.

8. Askari haruhusiwi kupekua nyumba ya mtu bila kibali cha kupekua.

9. Askari lazima akuoneshe kibali cha kupekua na ukisome.

10. Kibali kieleze jina la aliyekitoa, kituo kilipotolewa,jina la mtu au sehemu ya upekuzi, au uchanganuzi wa mtu au sehemu.

11. Hairuhusiwi kupekuliwa usiku kuanzia saa 1 jioni mpaka saa 12 asubuhi.

12. Ni haki yako kumpekua askari kabla hajakupekua ili asipandikize kitu.

13. Usipekuliwa nyumbani bila kuwapo kiongozi wa mtaa.

14. Kila kitakachochukuliwa katika upekuzi lazima kiandikwe na askari aweke sahihi.

15. Mali iliyochukuliwa katika upekuzi lazima ibaki salama.

16. Mwanaume haruhisiwi kumpekua mwanamke na mwamke haruhisiwi kwa mwanaume.

17. Unaruhusiwa kukataa kupekuliwa iwapo taratibu hizi hazikufuatwa.

18. Askari haruhusiwi kukutukana wala kukupiga.

19. Unaruhusiwa kutozungumza lolote mpaka unayemuamini afike uwapo chini ya ulinzi, ni haki yako.

20. Usilazimishwe kuongea au kuandika ambacho hutaki, ni haki yako.

21. Usitoe maelezo bila uhakika yatatumika mahakamani yatakuletea shida.

22. Unaruhusiwa kukaa kimya na usizungumze kitu uwapo chini ya ulinzi.
Yote nimekubali kaka ila sasa kwa kweli polisi wetu akushike alafu ujifanye huongei nadhan kitakachokupata ni dhahir utaenda kuadhithia kwa mkeo na watoto
 
Waliniletea ujinga wa kulazimisha kunikamata eti nakunywa pombe SAA tano asubuhi, kitu ambacho siyo kabisa na eneo tulilokuwepo tulikuwa tunafanya makubaliano ya chumba cha biashara.

Walifika na gari lao wasimama, kiongozi wao akaamrisha kamateni na hao!! Akaja askari mmoja toka kwenye gari lao yuko kiraia akaniambia ingia kwenye gari, nikamuuliza we nani? Akajibu huoni hiyo gari?nikamuuliza kwani INA nini? Akaniambia unaleta jeuri?

Akanishika Tanganyika jerk, nikamuambia niachie, akataka kunisukumizia mbele, nikamsukuma mda huo wenzie kama 8 hivi wanaangalia tu.

Wakaja wawili, nikawablock mikono yao, yule wa mwanzo akarusha ngumi, nikamblock nikampa ngumi ya kichwa akapepesuka, wakajaa kama nyuki, nilipigana siku ile, hawa jamaa hawanaga nguvu kabisaa, nilimchania shati mmoja aliyevaa kiraia mpaka kabaki na vest/singlet.

Wale wenye bunduki wakanionyeshea bunduki nikanyoosha mikono juu kutii amri ya silaha, ilikuwa ni sinema kama yah Hollywood.
Sikukaa hata lisaa wakanitoa mwenyewe baada ya kushauriana wao kwa wao.

Nilipiga hao polisi kipigo cha mbwa koko.

They don't care on arrest tactics, they rely on brutal methods.

Sent using Jamii Forums mobile app
Hii ni hadithi au?
 
police.jpg

IMEANDALIWA NA MAWAKILI

1. Askari akikuweka chini ya ulinzi muulize kitambulisho ni haki yako.

2. Askari akikukamata akuoneshe kitambulisho chenye muhuri wa mahakama kama anasema ametumwa na mahakama kukumata, ni haki yako.

3. Askari akikukamata akwambie kwanini anakukamata na anakupeleka kituo gani, ni haki yako.

4. Unaruhusiwa na sheria kukataa kukamatwa hata kutumia nguvu kama hukuambiwa sababu ya kukamatwa.

5. Askari anapokiuka taratibu za ukamataji anageuka na kuwa mhalifu ni haki yako kujikinga naye.

6. Askari haruhusiwi kukuvuta shati, kukukaba koo, kukushika suruali kama hujakataa kutii amri halali.

7. Askari haruhusiwi kuondoka na mtu mwingine baada ya kumkosa mtuhumiwa halisi.

8. Askari haruhusiwi kupekua nyumba ya mtu bila kibali cha kupekua.

9. Askari lazima akuoneshe kibali cha kupekua na ukisome.

10. Kibali kieleze jina la aliyekitoa, kituo kilipotolewa,jina la mtu au sehemu ya upekuzi, au uchanganuzi wa mtu au sehemu.

11. Hairuhusiwi kupekuliwa usiku kuanzia saa 1 jioni mpaka saa 12 asubuhi.

12. Ni haki yako kumpekua askari kabla hajakupekua ili asipandikize kitu.

13. Usipekuliwa nyumbani bila kuwapo kiongozi wa mtaa.

14. Kila kitakachochukuliwa katika upekuzi lazima kiandikwe na askari aweke sahihi.

15. Mali iliyochukuliwa katika upekuzi lazima ibaki salama.

16. Mwanaume haruhisiwi kumpekua mwanamke na mwamke haruhisiwi kwa mwanaume.

17. Unaruhusiwa kukataa kupekuliwa iwapo taratibu hizi hazikufuatwa.

18. Askari haruhusiwi kukutukana wala kukupiga.

19. Unaruhusiwa kutozungumza lolote mpaka unayemuamini afike uwapo chini ya ulinzi, ni haki yako.

20. Usilazimishwe kuongea au kuandika ambacho hutaki, ni haki yako.

21. Usitoe maelezo bila uhakika yatatumika mahakamani yatakuletea shida.

22. Unaruhusiwa kukaa kimya na usizungumze kitu uwapo chini ya ulinzi.
Mkuu unaongelea Polisi wa Ulaya kama picha zinazoonekana hapo au?? Kwa Afrika naona unataka tuvunjwe miguu au kuuawa kabisa!!
 
Back
Top Bottom