Ze comed vs Futuhi

Che-lee

JF-Expert Member
Jun 10, 2011
318
88
Nilikuwa sehemu ya wapenzi wa kundi maarufu la vichekesho la ze comedy kipindi likitumia runinga za bwana Mengi, moja ya sababu za kulipenda kundi hili nikuwaigiza viongozi wa serikali kwa mazuri yao na mabaya! Lakini baada ya kundi hili kudai limepata marisho mapya ya kijani kibichi lilitua mikononi mwa tbc ccm, kile kinachotendwa na kundi hilo kimekuwa na walakini kwenyenye macho na akili yangu. Futuhi ni kundi lingine linalorusha vichekesho vyake kupitia Star tv lenye kuuvuta mtima wangu, binafsi kundi hili sioni kama limefungamanishwa na matakwa ya mtu/kundi fulani. Tatizo lake ni mazingira ya utengenezeaji wa kazi zake, mf dhana ya kichekesho utaona inatofautiana na sehemu waliyotengenezea. Hawa wangeweza kutengeneze maene kama dar vile tungewasahau kabisa akina masanja na joti!

Mtazamo wangu Futuhi wapo juu!!!
Jf mtazamo wenu plz!!!
 
Walio juu zaidi ya wote ni akina Mtanga wa EATV kwa sababu hao wa Futuhi unaosema wanamilikiwa na mwanamagamba Antony Dialo aliyeangushwa uchaguzi ulpita
 
Akina masanja wako juu sana, mimi huwa siangalii kingine kama akina jito, mjuni etc wapo hewani. Acha wivu wakijinga na acha uvivu wakufikiria.
 
Akina masanja wako juu sana, mimi huwa siangalii kingine kama akina jito, mjuni etc wapo hewani. Acha wivu wakijinga na acha uvivu wakufikiria.
Huo ulikuwa mtazamo wangu ndio maana nikawaulizeni nyie, hukuwa na haja ya kunitusi ndugu yangu!!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom