Zanzibar - Ofisi Makamu wa kwanza - pili wagongana suala la urais wa kupokezana

Candid Scope

JF-Expert Member
Nov 8, 2010
11,890
6,898
MohamedAbood(1).jpg

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili
Mohammed Aboud Mohammed

Abood apinga urais wa kupokezana


Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili Mohammed Aboud Mohammed amesema ni hatari Rais wa Muungano kupatikana kwa zamu katika mfumo wa Muungano wa Tanganyika Zanzibar. Tamko hilo amelitoa alipokuwa akizungumza katika mahojiano maalum kuhusu maadhimisho ya miaka 48 ya Mapinduzi ya Zanzibar huko Ofisini kwake Vuga mjini Zanzibar jana. Alisema kuwa na mfumo wa kutoa urais kwa zamu ni mwanzo wa kuligawa taifa na kuvuruga umoja wa kitaifa wa Tanzania. "Ni hatari kuwa na mfumo wa kutoa urais wa muungano kwa zamu kwa sababu ni mwanzo wa kuligawa taifa vipande," alisema Waziri Aboud.


Alisema utaratibu unaotumika sasa wa kupata mgombea wa nafasi ya urais kwa kuzingatia sifa na uwezo bila ya kuangalia anatoka upande gani wa muungano ndiyo unafaa kuendelea kutumika kwa sababu umesaidia kuimarisha muungano. Aidha, alisema kwamba mawazo kama hayo hayafai kupewa nafasi kwa sababu ni mwanzo wa kuanza kujenga ubaguzi jambo ambalo kinyume na misingi ya umoja wa kitaifa. "Kama leo tukisema kuwepo na zamu ya urais wa Muungano baina ya Tanzania bara na Zanzibar badaye wataibuka watu wakitaka kuwe na zamu urais wa Zanzibar baina ya visiwa vya Unguja na Pemba". alisema.


Alisema kutokana na Tanzania kuwa na mikoa mingi kutaibuka watu wakitaka zamu ya kutoa urais katika mikoa yao kama Mwanza, Tabora, Rufiji, Kigoma na kuwa mwanzo wa kuzorotesha umoja wa Watanzania. Waziri Aboud alisema utaratibu unaotumika sasa ni mzuri kwa sababu umesaidia kupata viongozi wanaofanyakazi bila ya kuzingatia wanatoka upande gani wa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar. Waziri Aboud alisema katika kipindi cha miaka 48 ya Mapinduzi, Muungano umeleta faida kubwa katika kuimarisha amani na umoja wa kitaifa kwa wananchi wake. Alisema Muungano umesaidia kujenga misingi ya kiuchumi kutokana na wananchi wa Zanzibar wapatao milioni 1.2 kupata nafasi ya kulitumia soko la biashara la Tanzania bara la watu milioni 40.


Hata hivyo alisema wakati huu wa kuelekea mchakato wa mabadiliko ya katiba ya muungano ni vizuri wananchi wakapata nafasi ya kujadili na kuamua wanataka katiba ya aina gani kwa maslahi ya maendeleo ya nchi na vizazi vijavyo. "Upande wangu mie binafsi napendelea mfumo wa serikali mbili ndiyo umesaidia kuimarisha Muungano wetu," alisema.
 
Wiki mbili zilizopita Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar aliongea na vyombo vya habari kwamba urais awamu ijayo ni zamu ya Wazanzibar kwa kufuata mfumo wa kupokezana. Jana Waziri wa nchi ofisi ya Makamu wa pili wa Zanzibar amekuja na tamko tofauti kwamba urais si wa kupokezana ila utaratibu wa sasa wa kumpata rais wa Jamhuri kutokana na sifa za mtu ndio unafaa. Haya matamko ya viongozi waandamizi ngazi ya kitaifa yanatatanisha na pengine kugonganisha vichwa vya wananchi.
 
Ana hoja nzuri.

True ndugu, huu utakuwa mwanzo wa mambo mabaya sana. Tutaenda kwenye kanda, mikoa, wilaya .... Koo na familia. Kama alivyosema Mwalimu hii dhambi ni kama kula ya mtu.

Tena kutimiza matakwa ya haka "kamfumo ka kupokezana" itabidi tupunguze hata muda wa rais kukaa madarakani ili wote tufit.... Very bad.
 
Ana hoja nzuri.

Naanza kusoma hoja ya baadhi ya watu kuwa Seif ana uchu wa madaraka kutokana na kung'ang'ania hoja ya urais wa kupokezana bila kuangalia ubora. lakini hoja ya Aboud ina mshiko, ameongea kwa kuona taswira ya uongozi bora badala ya kuendekeza ule wa kukpokezana bila kutazama ubora wa mtu.
 
Hivi maalimu Seif na BAKWATA hata hautofautiani akili wote ni wabaguzi na ndo maana Seif alikubali kuhongwa akauza Uraisi kwa Shein. BAKWATA na SEIF ni wadini. Afadhali abood amawambia ukweli. Mkapa pia 2005 alisema Urais si wakupokezana ila vigezo na masharti kuzingatiwa.
 
Umegundua hili sasa, umeona alivyotulia baada ya kuukwaa umakamu wa rais Zanzibar, na sasa ananogewa zaidi kutaka aje kuukwaa ule wa Muungani, na kama hatafanikiwa walao aupate umakamu wa Muungano, ndo ndoto zake, maana kauli yake si ya upembuzi wa ubora bali kukalia kiti kile.
 
Kuna tetesi nilisikia eti huyu jamaa wanamuandaa kuwa Raisi wa Zenji hapo baadae japo sina uhakika nazo.
 
Kuna tetesi nilisikia eti huyu jamaa wanamuandaa kuwa Raisi wa Zenji hapo baadae japo sina uhakika nazo.
Bitabo sio kweli kuwa jamaa anaandaliwa bali Abood ni presidential material ambaye atalinda na kudumisha muungano wengine ni Dr. Mwinyi na Shamsi Vuai Nahodha!. Na kwa maandalizi ya Mzanzibari kuwa rais wa Muungano kwa sasa ni Dr. Shein pekee!.
 
Ana hoja nzuri.

Siku hizi hatuongozwi tena na hoja...tunapelekana kwa viroja! Huyu jamaa amesema kweli kabisa. Ila nani anataka kuusikia huo ukweli? Eti tupokezane kuongoza nchi hata kama anayetakiwa kupewa kwa upendeleo huo hawezi na hafai.
 
huyu jamaa anajitengenezea ugombea mwenza (umakamo) 2015, duhh kampeni zimeanza mapema, Mungu jaalia muungano uvunjike b4 nxt election tuwaangalie watesema nn?
 
inatia moyo kwamba bado kuna watu wachache wenye fikra pevu toka sehemu hiyo ya muungano
 
huyu jamaa anajitengenezea ugombea mwenza (umakamo) 2015, duhh kampeni zimeanza mapema, Mungu jaalia muungano uvunjike b4 nxt election tuwaangalie watesema nn?


Ukisoma mambo yanavyokwenda CUF na CCM wanazidi kuandaa njia kwa ajili ya Chama makini kinachojongea kwa kasi kuingia Ikulu, ndio maana ukiwaona Chadema wako kama hawaoni kinachoendelea kwa vile kujiingiza katikama mambo yao wasijeangushia kitumbua mchangani kuchika mauchafu yao. Acha
 
Ana hoja nzuri.

Hakuna kitu hapo hofu yake ni kutoweka kwa mfumo wa sasa wa serkali mbili unaoinufaisha zanzibar kwenye huu muungano feki. Watu 1.2 millioni currently with 4 sitting presidents, mawaziri kwenye mabaraza mawili ( zanzibar na muungano) wabunge wa mabunge mawili (wawakilishi na muungano) waajiriwa kwenye serkali mbili (zanzibar na muungano), wanasiasa wa vyama vya siasa (zanzibar na muungano) - chama hakiwezi kusajiliwa hadi kiwe na mzanzibari
Wadanganyika tumeshikwa pabaya na hawa mapopo (Muungano wataka, muungano wakataa) maana chao chao chetu chao. Sisi wadanganyika kwisha kazi tuendelee tu kulipa jizya.
 
kumbe kuna wazanzibar wengi tu wana hoja nzuri ila wametulia..nadahani haya ni mawazo ya wengi..huyu jamaa ana akili sana
 
Back
Top Bottom