Zanzibar na China kushirikiana katika uchumi wa Buluu

Ojuolegbha

JF-Expert Member
Sep 6, 2020
741
479
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Hussein Ali Mwinyi amekutana na Naibu Waziri wa Maliasili wa China Mhe. Sun Shuxian na ujumbe wake Ikulu Zanzibar tarehe: 28 Januari 2024.

Aidha Rais Dk. Mwinyi ameishukuru Serikali ya China kwa misaada ambayo wamekuwa wakiipatia Zanzibar katika miradi mbalimbali ya maendeleo na kudumisha uhusiano wa muda mrefu.

Kwa upande mwingine Rais Dkt. Mwinyi amesema China na Zanzibar zitatiliana saini hati ya ushirikiano katika sekta ya uchumi wa buluu ikiwemo sayansi na teknolojia ya baharini, uchunguzi wa mazingira ya bahari, utabiri wa ufuatiliaji na tahtmini ya maafa , utafiti wa baharini, kujengea uwezo, uwekezaji, uhifadhi wa viumbe hai wa baharini na ulinzi wa mfumo wa ikolojia wa baharini.

Naye, Naibu Waziri wa Maliasili wa China Mhe. Sun Shuxian ameeleza kuwa China inatoa fursa za ufadhili wa masomo kwa wanafunzi wa Kizanzibari katika fani ya bahari na viumbe wa baharini pia itaendeleza ushirikiano na Zanzibar.

IMG-20240128-WA0020.jpg
IMG-20240128-WA0021.jpg
IMG-20240128-WA0024.jpg
IMG-20240128-WA0023.jpg
IMG-20240128-WA0022.jpg
IMG-20240128-WA0018.jpg
IMG-20240128-WA0019.jpg
 
Kwa upande mwingine Rais Dkt. Mwinyi amesema China na Zanzibar zitatiliana saini hati ya ushirikiano katika sekta ya uchumi wa buluu ikiwemo sayansi na teknolojia ya baharini, uchunguzi wa mazingira ya bahari, utabiri wa ufuatiliaji na tahtmini ya maafa , utafiti wa baharini, kujengea uwezo, uwekezaji, uhifadhi wa viumbe hai wa baharini na ulinzi wa mfumo wa ikolojia wa baharini.
Bara itamegewa ngapi
 
Zanzibar "wanalipiza" kwa miaka 30 ya utawala wa bara. Kwa kipindi hicho, dili za Zanzibar zilikuwa zinapigwa pini, naona sasa zimechangamka.

Nadhani sasa hata ule mgao wa fedha kwa mujibu wa mkataba na sheria ya muungano, unazingatiwa sana. Kwa sasa hata ACT wazalendo upande wa Zanzibar hawapigi kelele.

Mwinyi anajenga kila kona, mpaka wazanzibari wanamuita mzee wa mabati.

Wanataka Mwinyi achukue urais wa Muungano 2030. Akipiga kumi nyingine za Muungano, Zanzibar ni Dubai.

Kwa sasa kuna kampeni kubwa ya wazanzibari kununua ardhi Tanga na Morogoro kwa maeneo yanayostawisha karafuu. Punde si punde maeneo hayo yatakuwa Pemba ndogo
 
Non sense! wache wanunue tu, ikiwa wakenya na raia wengine wa nchi jirani wanamiliki ardhi kiaina, itakuwa wazenji? mwisho wa siku ardhi yote ni mali ya serikali ataezingua tunataifisha! na kwa uvivu wa hawa ndugu zako hata wakinunua hakuna kilimo watafanya, Mwalimu si aliwapa kule MAKURUNGE , BAGAMOYO, mbona waliitelekeza na hatimae tukaiitwaa?
 
Back
Top Bottom