Zanzibar kunufaika na ufadhili wa masomo Uturuki

Ojuolegbha

JF-Expert Member
Sep 6, 2020
754
485
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi amekutana na Rais wa Jumuiya ya Waturuki waishio Ughaibuni, Abdullah Eren na ujumbe wake Ikulu Zanzibar tarehe 7 Desemba, 2023.

Katika mazungumzo yao wamegusia ushirikiano katika sekta elimu ikiwemo ufadhili wa masomo kwa wanafunzi 50 kila mwaka kwa ngazi ya shahada, shahada ya uzamili na shahada ya uzamivu nchini Uturuki kuanzia mwakani 2024 pamoja na mafunzo kwa walimu wa vyuo vya amali na mengineyo.

Rais huyo aliambatana na Balozi wa Uturuki nchini Tanzania Dkt. Mehmet Gulluoglu.

IMG-20231207-WA0007.jpg
IMG-20231207-WA0005.jpg
IMG-20231207-WA0006.jpg
IMG-20231207-WA0004.jpg
IMG-20231207-WA0008.jpg
IMG-20231207-WA0003.jpg
 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Hussein Ali Mwinyi amekutana na Rais wa Jumuiya ya Waturuki waishio Ughaibuni, Abdullah Eren na ujumbe wake Ikulu Zanzibar tarehe 7 Desemba, 2023.

 
Back
Top Bottom