Zanzibar hiyooo... kidogokidogo!

Wanajaribu bado wako katika Pilot study.

ZNZ sasa hakuna upinzani maana kila mpinzani atakayeshinda ataingizwa ktk mfumo wa serikali ya umoja wa kitaifa.
 
Utabiri wangu kabla ya kuundwa kwa SUK ni kuwa CUF hawatadumu miaka 5 katika serikali hiyo, kama walivyofanya Nationalist Party kule Afrika ya Kusini. Na ikiwa watabakia, tutayarishe jeneza kwa maziko rasmi ya CUF.
 
Umoja wa kitaifa ni one of the big break through katika Zanzibar Political history.Mchakato mzima wa kuunda GNU ndio uliozaa mjadala wa katiba ya Tanzania kufanyiwa marekebisho.

Hivyo sisi huku Zanzibar wote wana CUF na CCM we got nothing to loose.CUF wangetakaa mchakato wa GNU, tusingelikuwa na mabadiliko ya katiba inayoliliwa na CHADEMA leo hii.

Heads up guys, we are heading for big changes here...you should all be happy on this one:smile-big:.

God bless!
 
Bila shaka kuna watu wengi wameshazoea kuona migogoro inaendelea katika jamii..Tumesahau kuwa Zanzibar wamekuwa na migogoro,mipasuko, miafaka, maridhiano? Migogoro ya miaka zaidi 15...hiyo multipatry(monoparty) imesaidia nini?
Hata hapa Tz tuna multipartism, upinzani umesaidia nini katika kuiwajibisha serikali?

tunaweza kuwa na hoja za msingi kabisa," wanandoa","wanalala kitanda kimoja", "CUF kwishnei", "CUF wamejitengenezea jeneza", CUF itakufa with in 5years"...ukweli utabaki kuwa kama huu mfumo wanaofuata hivi sasa utatekelezwa kwa nia njema, na bila kutaka kukomoana basi atakaepata unafuu atakuwa mwananchi wa kawaida. Jee kuna faida ya maana kuliko hiyo?

Kuna nchi duniani zinafuata mfumo huo wanaufuata Zanzibar leo, na katika nchi hizo huwezi kusema hazina demokrasia. Zitafute halafu upime, demokrasia yao na uwajibikaji wao...utagundua wako mbali kuliko sisi na multipartism yetu, isiyo na miguu wala kichwa! ni mivutano tu.

Bila shaka kwa wale wenye hofu ya CUF kufa, ni vizuri hata mukiwashauri nini wafanye, wasiliane nao muwape mawazo yenu yenye nia ya kujenga na sio kuwalaumu tu..bila shaka wao pia wamefikiria sana kabla ya kuamua kufanya wanayoyafanya.

Binafsi yangu sioni kama CUF itakufa ila wana nafasi ya kujitandaza zaidi. Kama walikuwa wanazuiliwa kufanya mikutano baadhi ya maeneo hilo litasita sasa na wataweza kufanya mikutano yao popote Zanzibar.
Zamani Seif na CUF wenzake iliwapasa kukimbizana na polisi, "vibali vya mikutano"..leo polisi wanamlinda Seif hata anapokwenda kufungua matawi ya chama chake! kwa hiyo sioni vipi Chama chao kitakufa.
La kusema kuwa wajifungulie mtandao mkubwa na bara hilo ni la msingi kulifanya.Tukumbuke CUF wamepata majimbo bara mara hii, kwa hiyo wapo bara ila wajitahidi zaidi.

kama wataweza kupata tume huru ya uchaguzi Zanzibar na mahakama huru na CCM kuendesha siasa za kistaarabu basi mfumo wanaofuata Zanzibar kwa sasa unaweza kusaidia TZ katika transition ya kujenga demokrasia ya kweli. CCM hawataona haja ya kuona vyama vya upinzani kuwa ni maadui wao, kwani watakuwa wanajua kuwa inawezekana kufanya kazi na chama chengine ambacho awali kilionekana kuwa ni "hasimu, adui".
Tuwape a benefit of doubt kuwa system yao itafanya kazi vile inavyopasa, kama CCM hawato-sabotage.

Ikifanya kazi kwao pengine ,tutai-adopt na huku bara. na kuacha siasa za uhasama na mieleka. Siasa si lazima iwe ni vita!
 
Baraza la mawaziri kivuli Z`bar lafutwa




Na Mwinyi Sadallah



Baraza la Wawakilishi Zanzibar limetangaza mabadiliko makubwa ya muundo wake ikiwemo kufuta baraza la mawaziri kivuli na nafasi ya kiongozi wa upinzani, baada ya kuundwa kwa Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar (GNU).
Hayo yameelezwa na Katibu wa Baraza hilo, Ibrahim Mzee Ibrahim, wakati akizungumza na waandishi wa habari, Makao Makuu ya Baraza hilo Chukwani mjini Zanzibar jana.
Alisema kwamba kufuatia kuundwa kwa Serikali ya Umoja wa Kitaifa kanuni za Baraza la Wawakilishi zinalazimika kufanyiwa marekebisho kuanzia mkutano wa pili unaotarajiwa kuanza Januari 19, mwaka huu.
Mzee alisema Baraza la Mawaziri Kivuli limefutwa na nafasi ya kiongozi wa upinzani haitokuwepo tena na badala yake kutaanzishwa nafasi ya Mnadhimu Mkuu wa Serikali katika Baraza la Wawakilishi na kila chama chenye wajumbe ndani ya baraza hilo kitakuwa na mnadhimu mmoja.
Alisema mnadhimu mkuu wa Serikali katika Baraza la Wawakilishi atateuliwa na Serikali na Makamo wa pili wa Rais ndiye atakayekuwa mtendaji mkuu wa shughuli za Serikali ndani ya baraza hilo.
Kabla ya marekebisho hayo ya kanuni, Waziri Kiongozi ndiye aliyekuwa kiongozi mkuu wa Shughuli za Serikali, mfumo ambao umebadilika baada ya marekebisho ya kumi ya Katiba ya Zanzibar yaliyokaribisha Serikali ya Umoja wa Kitaifa.
Aidha alisema kwamba kuanzia sasa wakuu wa mikoa hawatokuwa wajumbe wa Baraza la Wawakilishi kwa vile marekebisho ya kumi ya Katiba ya Zanzibar yamewaondoa na watabakia watendaji tu katika mikoa yao.
Alisema kwamba kanuni za baraza la wawakilishi za mwaka 2009 zimefanyiwa marekebisho upya ili ziendane na mazingira yaliyopo sasa katika utendaji wa baraza hilo likiongozwa na Serikali ya Umoja wa Kitaifa.
Katibu huyo alisema kwamba Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi hivi sasa watakaa ndani ya baraza bila ya kuzingatia tofauti za vyama vyao isipokuwa safu ya mbele itaongozwa na mawaziri na manaibu waziri na kufuatiwa na wajumbe wasiokuwa na nyadhifa katika Serikali.



CHANZO: NIPASHE JUMAPILI


Haya ndiyo wasio na macho huyabeza! Hongera Wazanzibari!

Just Another Confusion. Ndo ya CUF na CCM Ilipangwa Tangu Awali. Sharif na JK Walishakaa Kabla ya Uchaguzi 2010. Hakuna Kipya Hapa. Watakaoumia na Mejeraha Makubwa ni CUF - Bara, Lipumba.
 
Hoyee Zanzibar, achaneni na hawa Watanganyika waendelee kuulea ufisadi na kulalama kama hawajala ndiyo Manna Werema aliwaambia wanaongea kama mabata. Sanzibar hoyeee, muungano zii.
 
Hakuna jipya upinzani Zanzibar ulikwisha siku hatuna haja ya kujadili kitu ambacho hakipo ingekuwa vyema kama wangemchukua na Lipumba ili waondoke huku bara.
 
Halafu utawasikia cuf bara wanataka kuwemo kwenye kambi ya upinzani!
 
Back
Top Bottom