Zantel ni moja ya kampuni ya mawasiliano inayojiendesha kiujima sana. Ushahidi huu hapa

James Hadley Chase

JF-Expert Member
Mar 25, 2020
1,578
2,664
Sababu ni hizi

1. Hawnaa vifurushi vya kueleweka, yaani mtu unalipa Tsh 2000 wnaakupa sms 3000 kwa siku 30.
Ongezeni sms zifike hata 5000-10000

2. Hawnaa huduma ya wateja ya kueleweka, ni mwendo wa kupiga 100 ndio muelewane tofauti na wenzako akina TTCL, VodaCom, Tigo na Halotel kwa mbali wakijikongoja huduma kwa wateja ipo mpaka WhatsApp yaani mnachat kishkaji sana

3. Vifurushi vya ovyooo, ukiweka vocha hata kupata kifurushi cha ofa ni mtihan, unapew madakika kibao kuliko sms na mb, punguzeni hizo dakika ongezeen Mb na SMS

4. Vifurush vya chuo, hapa wamejitahid ila tatizo kuna ubaguzi. Hapa kuna vifurushi vya bara na Zanzibar, ukiwa mtu wa bara haupati vifurushi vya Zanzibar, na ukiwa mtu wa Zanzibar hupati vya bara, fanyeni marekebisho kwenye menyu yenu *148*15#

5. Vifurush vimekaa ovyoovyo bila mpangilio maaum kama nguo za watoto kabatin vile

6. Kujibu shida za mteja ni tatizo lingine kwenye customer care, wanajibu wanavyojisikia hawa.

7. Sms kutokufika kwa wakati, muda mwingine sms zinagoma kwenda mpaka urudie mara ya pili ndio inaenda. Kuna siku nilituma sms Ijumaa kwenda namba ya voda ikaja kufika siku ya Jumanne

8. Menyu yenu ya *149*15# kuna muda inagoma kabisa kufanya kazi, yaani unapiga inajicancel unapiga inakubali. Waambieni wataalam wenu wairekebishe

9. Hawashauriki, hata ukiwapa ushauri kiasi gani wanaishia kukuangalia tu ukimaliza kuongea ndio imeisha hiyo kwaheri.

Badilikeni jamani namba zenu za simu zipo vizuri sana yaani 0777 ila huduma za humo ndani ni mbovu tu wanawashindwa hata Airtel.

Airtel hawakuwa na vifurushi vya kueleweka wakamua kukopi kwa wenzao VodaCom Tanzania, wana vifurushi vizuri tatizo ni network yao ipo slow au unaweza ukapata bando zuri ila network ukaitafute mwenyewe.
 
Mitandao yote hayo matatizo yapo.

Kitu cha msingi ni kuangalia sehemu yenye afadhali kwa upande wako.

Mfano kwa upande wangu, ingekuwa tunaruhusiwa kujiundia vifurushi wenyewe, Mimi ningeweka MBs na Dakika tu.
 
Mitandao yote hayo matatizo yapo.
Kitu cha msingi ni kuangalia sehemu yenye afadhali kwa upande wako.
Mfano kwa upande wangu, ingekuwa tunaruhusiwa kujiundia vifurushi wenyewe, Mimi ningeweka MBs na Dakika tu.
Karibu nyumbani kumenoga hilo linawezekana
 
Back
Top Bottom