kyagata
JF-Expert Member
- Oct 18, 2016
- 6,616
- 12,767
Juzi kati nikawa na kijisafari cha kuelekea mikoa ya huko kaskazini mwa Tanzania. Nikasema ngoja nipande Kilimanjaro express, duh kwa kweli nilijuta sana kupanda lile basi.
Cha kwanza tulidanganywa kuwa basi ni luxury hivyo tukakatishwa nauli kubwa ila kiuhalisia hakuna luxury bus pale, bus siti zake zimechakaa, ndani linatoa harufu kama ya uvundo flani hivi, hakuna cha AC wala TV ndani ya basi. Basi lilikuwa limejaza kiasi kwamba abiria wengine wakawa wamekaa pale mbele kwa dereva na tulikuwa tukifika karibu na mizani wanawashusha baadhi ya abiria wanawachukulia bodaboda then tunawakuta mbele ya safari tukishavuka mizani.
Wahudumu wa basi ni kama wamekata tamaa yaani hawana mwamko na kazi yao, wanaongea lugha mbaya kwa abiria, badala yake muda wote wa safari walikuwa wamekaa tu kule mbele wanapiga story pasipo kusikiliza abiria pia bus lilikua linavuja.
Kwa kweli Kilimanjaro express niliyoipanda miaka mitano huko nyuma ina tofauti kubwa sana na hii ya leo. Wakati narudi Dar nikasema ngoja nijaribu kupanda BM coach, kwa kweli nimeinjoy sana kusafiri na BM, huduma nzuri sana na wahudumu wao wakarimu mno.
Kilimanjaro express msipobadilika na kufanyia kazi hizi kero za wateja wenu basi naweza kusema huu ndiyo mwisho wa zama zenu.