Zain waanzisha xtreme sms

Mkimbizi

JF-Expert Member
Aug 23, 2008
222
34
Taarifa zimefika punde, ZAIN wameanzisha xtreme SMS kama tiGO! Hii inaonyesha kabisa kupevuka kwa huduma za mawasiliano Tanzania. Hii mitandao nayo ni ya kujadiliwa maana..... kuna mambo kama ya kifisadi. Ni tangazo tu
 
kiasi gani wao? pia waanzishe extreme ya kupiga tutajua nao ni wanaume wa shoka!!!
 
kiasi gani wao? pia waanzishe extreme ya kupiga tutajua nao ni wanaume wa shoka!!!

Chuma !! Watz tunapenda sms kuliko kupiga kwa sababu ya issues zetu zileeeeeee, kumbuka hata mzee wa kaya Muungwana JK kwa sms ni kiboko, I doubt kama mtandao wao utahimili capacity load. Kuna watu wamezoea keypad za simu hata huwa hawaziangalii na vidole vimepinda wakati wa kusms...Big up Zain
 
Mambo ya Kelvin Twisa hayo, huyu jamaa ndo marketig manager wao kwa sasa. Jamaa alianzia Voda, Tigo wakapanda dau wakambeba, kafanya mambo kweli Tigo nyie wenyewe mmeshudia, naona Zain wakashtuka jinsi walivyodorora pamoja na kuwa na coverage kubwa wameamua kupanda dau la voda na kumbeba. jamaa anatisha kwa marketing kwenye area hiyo.
 
Taarifa zimefika punde, ZAIN wameanzisha xtreme SMS kama tiGO! Hii inaonyesha kabisa kupevuka kwa huduma za mawasiliano Tanzania. Hii mitandao nayo ni ya kujadiliwa maana..... kuna mambo kama ya kifisadi. Ni tangazo tu

Kama kweli zain wameiga it means that tiGO ni noma,wako juu saaana
express ur self
 
Kibaya tu ni kwamba hawawezi fikia level za tiGO. Jana nimeingia Jiachie na Extreme SMS... Kuanzia saa tatu mpaka saba asubuhi nilikuwa nimemaliza SMS 100 za Zain ikawa inaendelea nikata pesa kama kawaida sasa sijui siku nzima wanayoongelea katika matangazo yao ni ipi...

Ila upande wa tiGO... aaah kama kawaaaaaaaaaaaaaa!
 
Mambo ya Kelvin Twisa hayo, huyu jamaa ndo marketig manager wao kwa sasa. Jamaa alianzia Voda, Tigo wakapanda dau wakambeba, kafanya mambo kweli Tigo nyie wenyewe mmeshudia, naona Zain wakashtuka jinsi walivyodorora pamoja na kuwa na coverage kubwa wameamua kupanda dau la voda na kumbeba. jamaa anatisha kwa marketing kwenye area hiyo.

Acha kuongea pumba, kama huna data kaa kimya!..

Huyu jamaa hajawahi kufanya kazi Vodacom.

Ngoja nikupe historia fupi.

Jamaa alifanya kazi FCB ambayo ilikuwa advertising agency wa Vodacom, baadaye FCB ilinunulia na LOweScanad East africa (wahindi hawa jamaa) wakampiga chini kimtindo akaenda TiGO, kule kapiga kazi badaye akaiba wakamtimua, na sasa hivi siyo marketing manager wa ZEIN, marketing manager wa ZEIN ni Costantin Magavilla yeye yuko chini ya Costa.
 
Mkuu Mambo Jambo,

Nilikuwa naanza kutype kumjibu mkulu wa juu nikakutana na majibu yako mazuri! jamaa amekosa data za kujitosheleza lakini hajaandika pumba kwahilo umekosea!

Thanks kwa kutuhabarisha anyway!
 
Chuma !! Watz tunapenda sms kuliko kupiga kwa sababu ya issues zetu zileeeeeee, kumbuka hata mzee wa kaya Muungwana JK kwa sms ni kiboko, I doubt kama mtandao wao utahimili capacity load. Kuna watu wamezoea keypad za simu hata huwa hawaziangalii na vidole vimepinda wakati wa kusms...Big up Zain

Ushirombo,

Umekuwa na observation nzuri kuwa wa-TZ tunapenda sana ku-sms badala ya kuongea, mimi kwa mtizamo wangu nafikiri hili limetokea kutokana na gharama za kuongea kuwa juu kidogo, sijui mawazo ya wengine ni yapi, ila ukiangalia nchi zingine wanakuwa na huduma za kuongea kwa free kabisa hasa weekend na jioni kila siku, kisha unapoongea na mtu wa mtandao mmoja na wewe huchajiwi kitu ila ukiongea na walio nje ya mtandao unachajiwa na kuna kampuni zingine zinakupa dakika kama tuseme dakika 1000 kwa mwezi, hizi zinakuwa ni kwa ajili ya mitandao ya kampuni zingine ukiongea nao badala ya kukuchaji dakika hizo 1000 zinapungua. zikiisha sasa unaanza kuchajiwa tricky inakuwa kuongea nao aidha jioni au weekend au unaweza ongea nao mda wowote ila una-keep tub on your minutes kujua unazitumia vipi. so kwa kifupi mie nafikiri tuna sms sana kwa sababu ya gharama za kuongea ziko juu kidogo.
 
Mi nashauri mbeep tu washikaji wangu. hapo utakuwa umeepuka gharama kubwa za mitandao ya Kitanzania. Si hivyo ni vigumu kumiliki simu ya kiganjani wajameni.
Habari ndio hiyo
 
Acha kuongea pumba, kama huna data kaa kimya!..

Huyu jamaa hajawahi kufanya kazi Vodacom.

Ngoja nikupe historia fupi.

Jamaa alifanya kazi FCB ambayo ilikuwa advertising agency wa Vodacom, baadaye FCB ilinunulia na LOweScanad East africa (wahindi hawa jamaa) wakampiga chini kimtindo akaenda TiGO, kule kapiga kazi badaye akaiba wakamtimua, na sasa hivi siyo marketing manager wa ZEIN, marketing manager wa ZEIN ni Costantin Magavilla yeye yuko chini ya Costa.

We mambo jambo, unawewza kuwa unajua vitu au una data kama unavyodai lakini civilization bado huna, so huna tofauti na mnyama yeyote. Kuna haja gani ya wewe kunitukana niache pumba??? umeshindwa kunirekebisha kistaarabu hadi utoe lugha za kishenzi kama ulivyo we mwenyewe. Mtu mzima hadi ujiheshimu hakuna aliyekuforce kujibu hadi utukane, unatakiwa tu ujue njia mojawapo ya kupata information ni kutoa wrong information ili upewe right one. Sasa kwani wewe unajua kila kitu? you are just another type of a ..................shiit
 
unatakiwa tu ujue njia mojawapo ya kupata information ni kutoa wrong information ili upewe right one. Sasa kwani wewe unajua kila kitu?
Hakuna anayejua kila kitu, JF kama hujui kitu unauliza na wenye majibu watakujibu, hichi ni kijiwe cha kuelimishana na ku-entartain.

you are just another type of a ..................shiit

Hii inaonesha udhaifu wako ni wa juu kiasi gani..

Get a grip
 
Namshangaa "mchukia fisadi" akishikia bango kuwa ili kuepuka gharama ni ku-beep tu. Hivi kila mmoja aki-mbeep mwenzake nini kitaendelea? Nadhani la maana hapa napenda kumpa hi, Mzee Sabodo aliefanya analysis kwenye magazeti kuwa tunaibiwa na haya makampuni ya simu ya Tanzania. Nadhani wameanza kujitokeza na kuleta products nyingi kwenye soko tena kwa kushindana kuficha ufisadi wao. Wanatuibiaaaaa...sisi Watanzania tulio wengi. Mbona hayo makampuni hayaingii kwenye soko la hisa ili tununue shares? Wanahamisha faida na kwenda ku-invest nchi zingine. Serikali iwabane ...
 
Acha kuongea pumba, kama huna data kaa kimya!..

Huyu jamaa hajawahi kufanya kazi Vodacom.

Ngoja nikupe historia fupi.

Jamaa alifanya kazi FCB ambayo ilikuwa advertising agency wa Vodacom, baadaye FCB ilinunulia na LOweScanad East africa (wahindi hawa jamaa) wakampiga chini kimtindo akaenda TiGO, kule kapiga kazi badaye akaiba wakamtimua, na sasa hivi siyo marketing manager wa ZEIN, marketing manager wa ZEIN ni Costantin Magavilla yeye yuko chini ya Costa.

Jamiiforum, nakupenda kwa moyo wotee................x2 :)
 
Safi sana kwa kuanzia na hilo. Huenda nao wanaelekea waliko tigo ila wameona waanzie tofauti kwa sms. tigo ni kidume hasa mtu wangu, longa longo, extreme, bado wkend watu wanajirusha na wamekaa muda mrefu sana. kwa ujumla hizi kampuni za simu zinapata faida sana tena saaa hivyo hata voda wakifana kama tigo still watapata faida kubwa tuuuuuu, ila ndo wanatunyonya. wao kila kitu gharama, sms tsh59
 
baada ya wiki 'zain jiachie' ya buma it's all chaos sms haziendi.
 
Ama kweli biashara ni ushindani.

Jirushe! Ruka hewani siku nzima na Zain

Toka - Michuzi blog

KAMPUNI ya simu za mkononi ya Zain yenye mtandao ulioenea katika nchi 22 barani Afrika na Mashariki ya Kati, imezindua promosheni mpya ya Jirushe, itakayowawezesha wateja kutumia pesa kidogo kila siku kwa kupiga simu za mtandao wa Zain kwenda Zain.
Mkurugenzi wa Masoko wa Zain Tanzania, Margareth Kositany, amesema leo Dar kwamba wanachotakiwa kufanya wateja wa Zain ni kuandika neno JIRUSHE kila siku na kutuma kwenda namba 15354 ili kupata huduma hiyo na kuendelea kupiga simu na kuongea bure kuanzia saa 11:00 alfajiri hadi saa 12:00 jioni, siku za wiki.

“Zain leo inafurahia kuzindua ofa mpya ya kupiga simu bure inayojulikana kama JIRUSHE ili kuwawezesha wateja wetu kutumia pesa kidogo na kuendelea kupiga simu bure, na kuweza kuwasiliana kwa urahisi na ndugu, jamaa, marafiki, washirika wao kibiashara, familia na wawapendao,” alisema Mama Kositany.

“Ofa hii ni kwa simu za Zain kwenda Zain pekee na ni kwa wateja wa malipo ya awali. Hakuna mtandao mwingine utakaokuwezesha kuwasiliana kwa urahisi na watu wengi zaidi kuliko Zain,” alisema.

“Hakuna mtandao mwingine unaomwezesha mteja kupata faida zaidi kila siku zaidi ya Zain, na wateja wetu wataendelea kufaidika kupitia promosheni zetu za JIRUSHE na Mambo Wikendi,” aliongeza.

Kupitia promosheni ya Mambo Wikendi, wateja wa Zain wamekuwa wakipiga simu kwa bei ya Tsh 1 kwa sekunde kuanzia Jumatatu hadi Ijumaa kuanzia saa 3 usiku hadi saa 12 asubuhi na saa 24 wikiendi nzima.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam, Meneja Masoko huyo wa Zain, alisema Zain imedhamiria kuboresha maisha ya wateja wake, na hii pia ni namna nyingine ya kuwashukuru wateja wetu kwa kuendelea kuwa nasi.

“Kupitia JIRUSHE na Mambo Wikendi, wateja wetu watanufaika na viwango vyetu ambavyo vitawawezesha kuongea kwa kiasi kidogo cha pesa, nah ii itawafanya wajione wako katika Ulimwengu Maridhawa,” alisema Mama Kositany.

Zain Tanzania ambao ndio mtandao wa simu unaotoa huduma bora zaidi nchini, hivi sasa ina wateja zaidi ya milioni 3 na inatarajia kuwa na wateja zaidi ya milioni 4 kufikia mwishoni mwa mwaka huu.
 
Back
Top Bottom