Yuwapi Komredi Benard Membe?

Ni muda mrefu sasa umepita sijamsikia jasusi mbobezi na mwanadiplomasia mahiri ndugu Benard Membe ambaye siku za awali za utawala wa JPM alijitahidi kutoa matamko mbalimbali kadri anavyojisikia. Kwenye sakata kama hili la
sukari nimjuavyo angeshatoa tamko tena zito haswa.
Lakini sasa shushushu huyu hasikiki wala kuonekana kwenye media kama hapo
awali, nini kimemsibu?
Anayejua aje atujuze alipo mbunge huyu mstaafu wa pale Mtama.

Kwann unamuita jasusi?
 
Membe ni kachero wa mda mrefu Sana aki base katika ubalozi wa Tanzania US kama alivyokua RO(current TISS DG) kule London huyu jamaa (Membe)kwa mambo ya espionage and sabotage yupo vizuri , Si unajua tena hiyo kazi hamnaga ku-retire so still is TISS officer like Lyatonga of Vunjo.


Kwann unamuita jasusi?
 
Adui yake mkuu kwenye ile ligi ya kuingia magogoni alikuwa LOWASA, sasa badala ya Lowasa kukimbia nchi, Membe amekimbizwa na kivuli tu cha Lowasa maana Lowasa alisha muacha ndani akatoka nje ila kivuli kikafanya yake now membe ni historia.

Nasikia na yeye alilia kama yule Dr aliyekuwa mkuu wa mkoa morogoro.
 
Hampa mmeleta hili jina lake lijadiliwe ili atoke vipi? Haya tusubiri atatoka mwenyewe au JPM atamtoa?
 
Atakuwa ametulia anakula bata. Chezea uwazir mambo ya nje miaka yote hiyo na Mkuu kikwete alivyo kuwa anashinda nje. Atakuwa ame tengeneza za kutosha kabisa
 
Hili neon Comrade hili; sijui tu. Enzi zile tukiwa vijana wadogo (Enzi ya Ukoministi) sio kila mtu alikua anaitwa kwa jina hilo, ni kama Sir!!! Makocha wa ligi ya Uingereza wapo wengi na wamepita wengi, lakini kumbukumbu zangu zinaonesha walio wahi kuitwa SIR ni Alex Ferguson na Bob Charlton. Na Comrade ni hivyo hivyo tu though kwa zile Enzi zetu, sijui sasa hivi.
 
Atakuwa anaangalia mkulu anapojofunga magoli ya kisigino kwenye nyavu zake. Alipojaribu kumrekebisha mkulu aache kujifunga magoli mkulu akakasirika na kijana aliyetumwa kumtukana na kumshambulia Membe akazawadiwa cheo cha utafutaji na usombaji wa sukari ghalani (Ukuli wa wilaya).
 
Ni muda mrefu sasa umepita sijamsikia jasusi mbobezi na mwanadiplomasia mahiri ndugu Benard Membe ambaye siku za awali za utawala wa JPM alijitahidi kutoa matamko mbalimbali kadri anavyojisikia. Kwenye sakata kama hili la sukari nimjuavyo angeshatoa tamko tena zito haswa.

Lakini sasa shushushu huyu hasikiki wala kuonekana kwenye media kama hapo awali, nini kimemsibu? Anayejua aje atujuze alipo mbunge huyu mstaafu wa pale Mtama.

Ulishasema shushushu, kwani mashushushu wanaonekana?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom