Yu wapi Benji Cosmo wa Caribian beat kila Ijumaa Clouds FM?

Kibosho1

JF-Expert Member
Dec 12, 2017
2,491
3,999
Napenda rege na miondoko ya Caribian beat nk. Nakumbuka miaka ya 2007 hawa jamaa walikua 🔥 sana,
Alikuwa Cosmo mwenyewe na Dj alikuwa Bula na jamaa mwingine sikumbuki jina lake. Niliipenda sana rege kwa jinsi wajamaa walivyokuwa wanaendesha kipindi hicho.

Nasikitika kwa sasa kipindi hiki hakipo tena siyo clouds FM tu bali stesheni zote za radio. Mziki wa rege Tanzania haupewi kipaumbele kama miziki mingine ila ni moja ya miziki mizuri sana yenye hisia.

Katika pitapita zangu mtandaoni kikakutana na jamaa mmoja Mkenya anaitwa John Maina a.k.a MC fullstop. Anapenda rege, anaijua rege, nimependa sana mikato yake kwani ni kama akina Cosmo.


Download hizi 👇👇


Na hii 👇👇





Hawa jamaa wako wapi kwa sasa? Natamani sana bongo awepo mtu kama huyu anayejua muziki.
 
Back
Top Bottom