Yani nimekasirika kinomaa. Wanawake acheni hii tabia

Juzi kati nili Import Dem mmoja toka Dar akaja Mkoa walau Abadirishe mazingira. Tulikubaliana kama atakaa wiki moja na baadae arudi Dar. Dem alifika nikampokea.

Maisha ya kigeto yakawa yanaendelea nikiwa na mwanamke ndani. Maisha yameenda poa sana. Hasa ninaporudi toka vibaruani nakuta msosi, ndani kusafi, nguo zangu zimefuliwa na huduma za usiku napata yani hadi nikaanza kujiona FAZA.

Ishu imefika wiki sioni kama Manzi ana dalili za kuondoka. Kila nikimtrance naona kama ndo kafika. Nikaona sasa hiki ni kisanga. Nikajaribu kutunga safari za kikazi ili walau aseme anaondoka nikaona bado kimya anasema nikirudi ntamkuta. Nikatia figisu weeeeee hadi akaondoka.

Lakini amekaa Almost Mwezi mzima kwangu.
Sasa kipindi yupo hapa getto alikuwa anavaa nguo zangu kama Track suit, T-shirts na baadhi ya suruali zangu.

Yani ameharibu nguo zangu vibaya mnoooo. Nimeumia sana. Yani Tshirt zangu ziwezi kuzivaa tena maana zimetanuka kifuani kwa ajili ya matiti pia zina vile vinukta vya Chuchu.

Suruali zangu zimekuwa na Misambwanda balaaa. Yani zimekuwa kubwa matakoni na kiuno kimekuwa kikubwa balaaa.

Yani Jumla ya Nguo kama 20. Zenye thamani hadi kufikia laki 7 zimeharibika kabisa yani.

Mbaya zaidi wakati anataka kuondoka akasema et hajawai kupanda ndege. Ivyo anataka achukue flight to Dar.

Nikawa sina namna maana nataka aondoke tuu. Nikafanya booking ya siku 4 before nikapata ticket ya fast jet kwa 350k

Wakati namsindikiza akat wanafanya inspection kuna viti walikataa visippande ndege. Ni kama mafuta, perfum na vitu kibao. So ikabidi anipe nirudi navyo

Baada ya kufika home nikagundua kuwa ameacha vitu vyake vingine kama kanga nilizomnunulia maana alikuja na mtandio tu na nguo maa alikuja na pochi tu na huku nilimnunulia baadhi ya vitu.

Kasema mwisho wa mwezi atakuja kuchukua vitu vyake. Yani nimekasirika kinomaaaa

Wanawake acheni maudhi jamani.

Kuna masweta yangu nilinunua Ebay toka uturuki yote ameyaharibu kisa alikuwa anavaa apigie picha/ self ili awe anapost.

Yani nimeumia wajameni balaaa.
Umetuvunjia heshima sana wanaume wa mbasa
 
Mwanaume wa mkoani huyo.
Mie mwanaume wangu nilikuwa namvalia mpaka boksa na singlend ila halalamiki.
Nilikuwa nakumindi sana na nilianzisha uzi Kama huu juu yako,ndo maana nkakuacha.
''acheni maudhi wanawake'' in mtoa uzi voice
 
Mtoa mada kama isingekuwa sheria ya matumizi sahihi ya mtandao, nilitaka nikutukane matusi yote ya duniani ninayoyajua. Naomba tu Mungu akulaani ufe bila mke wala mtoto kwa udhalilishaji huu uliofanya

Sent from my SM-T285 using JamiiForums mobile app
 
Daah hapo ulikuwa umeoa sema tu ulijiongeza vingnevyo asingetoka.
Wengi wanaolewa hivyo hivyo na ungechelewa kuanzisha visa angekwambia kuwa hawez kurudi kule maana hana cha kuwambia pindi atapoulizwa kuwa alikuwa wapi.
Kwa mnaokaa maghetoni mtakubaliana na mm kwakuwa hayo tunayashuhudia kila siku na usipo kuwa makini unaweza kuoa wa kuvusha sku moja akakuharibia kwa mchumba kama ulikuwa nae.
 
Kweli boss nimejifunza
Daah hapo ulikuwa umeoa sema tu ulijiongeza vingnevyo asingetoka.
Wengi wanaolewa hivyo hivyo na ungechelewa kuanzisha visa angekwambia kuwa hawez kurudi kule maana hana cha kuwambia pindi atapoulizwa kuwa alikuwa wapi.
Kwa mnaokaa maghetoni mtakubaliana na mm kwakuwa hayo tunayashuhudia kila siku na usipo kuwa makini unaweza kuoa wa kuvusha sku moja akakuharibia kwa mchumba kama ulikuwa nae.
 
Kwa hyo tshet zimevutwa na vichuchu??/zikaharibika,,vichuchu kweli au zile ngoma nyingine zisizo stahimili kusimama hata kwa brah.. Ngija niendelee kuwaza
 
Mnajisifu wanaume wa mkoani tu kumbe wadada tu wanawapelekesha mpk mnaandika uzi huku je mwanaume itakuaje? Kha ha ha ha
 
Kweli boss nimejifunza
Nami yalinikuta nikaanza kuona dalili za kutoondoka mida ya saa kumi usiku nlichofanya nikamwambia kuwa mm ni kibarua tu na hapa gheto amenipangishia boss wangu na kila siku saa moja asubuhi anakuja kunikagua kuona kama nmelaza mwanamke ndani na ikitokea tu sina kazi na gheto natimuliwa, huwez amini alitoka asubuhi saaana nikawa nmepona
 
Back
Top Bottom